Nilichokiona jana kwa wachezaji wa Yanga

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Kwanza niweke wazi mimi ni shabiki WA Yanga.

Jana nimeangalia Ile mechi yote nikagundua yafuatayo kuhusu wachezaji wetu.
1. Mukoko: huyu kiungo maridadi nmegundua anaonekana kama Hana furaha kbs uwanjani ni kama anacheza basi Tu Ile hamasa aliyokuwa nayo msimu uliopita na happy face haipo kabisa.

Sjui ni sababu yanga walikataa kumuuza na wakati uwenda angeuzwa angepata mshahara mzuri Kama kisinda. Au sjui anaugulia kutokuwepo rafiki yake kisinda.

Lakini nmegundua mukoko ana shida ya kutokuwa mwepesi WA kufanya maamuzi hasa akiwa na mpira anaweza pewa pasi lakin unashangaa anazubaa kuangalia apeleke WP mpira sasa akikutana na viungo wepesi kama wale WA Jana lazma apotee kbs.
Ajirekebshe kwenye hili pia a relax ni kama kuna Jambo haliko sawa kwake.

2. Kibwana: huyu dogo ni mzuri sana kwenye kukaba lakini dogo huyu Hana uzoefu kbs akikutana na mawinga hatari Hana ujanja kibaya zaidi hajui hata kupga tackling.

Kingine dogo anaonekana kama anataka kuiga uchezaji wa djuma shaaban yaani WA kushambulia Sana kitu ambacho kinaigharimu timu kwani huo uwezo bado Sana na si mzuri WA kupiga krosi kbs. Ingawa watu wanamsfia Sana huyu dogo lakini mtazamo wangu boxer akitulia huyu dogo Hana uwezo kumzd boxer sema majeruhi ya boxer kpnd kile yalimpunguzia Kasi. Dogo ajirekebshe asishindane na Shaban djuma kiuchezaji ye acheze anavyochezaga.

3. Adeyum: huyu jamaa ni beki katili lakini ni mwepesi kupitika hajui Sana kummaaki adui yaani huitaji nguvu kubwa kumpita huyu jamaa na kupga Krosi ni mpambanaji hasa na hachoki tatzo mwepesi kupitika makosa mengi na hajui mpira WA kushambulia hata Krosi Tu hajui kupga.

4. Moloko: huyu dogo muda wote either Yuko offside au Yuko chini na nmegundua anajaribu kucheza kama kisinda lakini mbinu na mbio Hana kama kisinda Ila anajilazmisha kitu ambacho kitamgharimu Sana sioni kama atadumu sana yanga na sioni kama endapo mapinduzi balama akirejea Kwa Kasi ileile sioni kama huyu dogo atatoboa maana ni WA kawaida Sana. Bora hata ambundo namuona atakuwa gharasa mapema Sana sana.

5. Makambo: bonge la mfungaji muona nyavu lakini makambo kama kawaida yake hajui kukokota mpira na kupiga chenga mabeki yaani kuwachachafya mabeki huo uwezo Hana endapo mayele atakuwa na uwezo WA kukimbia na mpira na kupiga chenga na kufungua namuona makambo akisubiri nje na inasemekana mayele uwezo huo anao.

6. Mauya: huyu jamaa Hana uwezo WA kukaba kbs zaidi akikaba ni faulo Ila anajitahidi kupambania Sana huwa anabebwa na mukoko sa mukoko akiwa hovyo Naye anapoteana. Nashangaa Sana ilikuaje makame aliachiwa halafu akasajiliwa mauya huwa naona kama makame ni mzuri sana kuliko mauya. Kifupi huyu Naye hatakiwi kubaki yanga.

7. Mwamnyeto: huyu jamaa Naye ni kama huwa akabia macho Tu wakati mwngn pamoja na mwezie job yaani mshambuliaji anakuja na mpira anapiga chenga beki zote anaingia ndani ya 18 anawavuruga wote anafanya anavyotaka. Wakati mwngn naona ninja ni beki Sana kuliko mwamnyeto.

8. Yacouba: jamaa ni kama anacheza kistar Sana sioni kama huwa anapambana Sana uwanjani zaidi namuona mda mwng kazubaa na kutembea Tu akipata mpira si mwepesi WA kufanya maamuzi Ila anapenda akimbie nao mwisho WA SKU hakuna madhara. Pia kufungu kwake ni nadra sn anaweza pata nafasi mtu unasema kbs hili ni goal lakini unashangaa anapga nje huko. Ajitahidi hasa kwny kutumia nafasi.

9. Fei: sina tatzo naye Kwa kweli huyu dogo anapambana Sana hata Jana ilibidi arudi nyuma kidogo kuwasaidia akina mukoko na wakati mwngn ilibidi awatafutie mpira akina makambo mbele ya mabeki WA rivers.

10. Djgui: kipa huyu kijana Yuko vzuri na anaonekana anaumia Sana juu ya beki zake kuwa butu nilimuona kuna muda tukoswakoswa mpk akapga teke mlingoti WA goli Kwa hasira maana beki zlionyesha uzembe kbs.

Huu ni mtazamo wangu bt all in all tuna wachezaji wazuri Ila hawana maandalizi kbs kwasasa tuwe wavumilivu ila club bingwa tumeshatolewa Kwa kifupi hakuna jipya watafanya yanga kile Nigeria huu ndo ukweli. Ila msimu huu tutafanya vzuri kwenye ligi. Sjawaona Simba Ila sidhan km msimu watakuwa vizuri kutuzidi.
 
Uto ni uto tu ,mpira wa mdomoni ukiwapeleka kwenye pitch sababu kibao .manara mngemuweka midfield champion wa zengwe la mdomoni
 
Uchambuzi safi kabisa, Ninja ni bora sana kuliko Mwamnyeto sijui mtazo wa Kocha lakini yule dogo ni mzuri sana inahitaji kuaminiwa zaidi
 
Yataongewa meeeengi sana,ila sababu kubwa ya timu yetu ni maandalizi hafifu na wachezaji siwezi kuwalaumu....hatukuwa na pre-season ya maana.

NB:Binafsi nashauri tubaki na ligi tu, tutengeneze timu vizuri ila nionavyo mm tukiendelea kuforce tutaumbuka maana tuna wachezaji hatuna timu.
 
Eti mauya hajui kukaba? Duh hivi unajua kazi aliyofanya mauya pale kati au kazi ni kusifia wageni?
au haukucheki mechi jombaa...
yaani mauya ni bonge la kiungo ile mechi mukoko ndo alituuza tena!
nawaona aucho-mauya pale kati mechi zijazo.
 
Mnapofeli misukule ndio hapo! Umechambua vizuri sana ila kumbe mwisho wa siku unataka kufananisha na simba Vipi Azam hukuwaona walichowafanya wale wasomali? Kwanini usiseme Azam ulioiona kuliko simba ambayo hujaiona??
 
Yataongewa meeeengi sana,ila sababu kubwa ya timu yetu ni maandalizi hafifu na wachezaji siwezi kuwalaumu....hatukuwa na pre-season ya maana.

NB:Binafsi nashauri tubaki na ligi tu, tutengeneze timu vizuri ila nionavyo mm tukiendelea kuforce tutaumbuka maana tuna wachezaji hatuna timu.
Sasa mlitaka nani awafanyie maandalizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We will come back stronger than ever
Kama tu Arsenal yangu kila siku wanafungwa tena wanakula tano, basi sina budi kuendelea kusubiri Yanga itakayonipa furaha
 
Kwanza niweke wazi mimi ni shabiki WA Yanga.

Jana nimeangalia Ile mechi yote nikagundua yafuatayo kuhusu wachezaji wetu.
1. Mukoko: huyu kiungo maridadi nmegundua anaonekana kama Hana furaha kbs uwanjani ni kama anacheza basi Tu Ile hamasa aliyokuwa nayo msimu uliopita na happy face haipo kabisa.

Sjui ni sababu yanga walikataa kumuuza na wakati uwenda angeuzwa angepata mshahara mzuri Kama kisinda. Au sjui anaugulia kutokuwepo rafiki yake kisinda.

Lakini nmegundua mukoko ana shida ya kutokuwa mwepesi WA kufanya maamuzi hasa akiwa na mpira anaweza pewa pasi lakin unashangaa anazubaa kuangalia apeleke WP mpira sasa akikutana na viungo wepesi kama wale WA Jana lazma apotee kbs.
Ajirekebshe kwenye hili pia a relax ni kama kuna Jambo haliko sawa kwake.

2. Kibwana: huyu dogo ni mzuri sana kwenye kukaba lakini dogo huyu Hana uzoefu kbs akikutana na mawinga hatari Hana ujanja kibaya zaidi hajui hata kupga tackling.

Kingine dogo anaonekana kama anataka kuiga uchezaji wa djuma shaaban yaani WA kushambulia Sana kitu ambacho kinaigharimu timu kwani huo uwezo bado Sana na si mzuri WA kupiga krosi kbs. Ingawa watu wanamsfia Sana huyu dogo lakini mtazamo wangu boxer akitulia huyu dogo Hana uwezo kumzd boxer sema majeruhi ya boxer kpnd kile yalimpunguzia Kasi. Dogo ajirekebshe asishindane na Shaban djuma kiuchezaji ye acheze anavyochezaga.

3. Adeyum: huyu jamaa ni beki katili lakini ni mwepesi kupitika hajui Sana kummaaki adui yaani huitaji nguvu kubwa kumpita huyu jamaa na kupga Krosi ni mpambanaji hasa na hachoki tatzo mwepesi kupitika makosa mengi na hajui mpira WA kushambulia hata Krosi Tu hajui kupga.

4. Moloko: huyu dogo muda wote either Yuko offside au Yuko chini na nmegundua anajaribu kucheza kama kisinda lakini mbinu na mbio Hana kama kisinda Ila anajilazmisha kitu ambacho kitamgharimu Sana sioni kama atadumu sana yanga na sioni kama endapo mapinduzi balama akirejea Kwa Kasi ileile sioni kama huyu dogo atatoboa maana ni WA kawaida Sana. Bora hata ambundo namuona atakuwa gharasa mapema Sana sana.

5. Makambo: bonge la mfungaji muona nyavu lakini makambo kama kawaida yake hajui kukokota mpira na kupiga chenga mabeki yaani kuwachachafya mabeki huo uwezo Hana endapo mayele atakuwa na uwezo WA kukimbia na mpira na kupiga chenga na kufungua namuona makambo akisubiri nje na inasemekana mayele uwezo huo anao.

6. Mauya: huyu jamaa Hana uwezo WA kukaba kbs zaidi akikaba ni faulo Ila anajitahidi kupambania Sana huwa anabebwa na mukoko sa mukoko akiwa hovyo Naye anapoteana. Nashangaa Sana ilikuaje makame aliachiwa halafu akasajiliwa mauya huwa naona kama makame ni mzuri sana kuliko mauya. Kifupi huyu Naye hatakiwi kubaki yanga.

7. Mwamnyeto: huyu jamaa Naye ni kama huwa akabia macho Tu wakati mwngn pamoja na mwezie job yaani mshambuliaji anakuja na mpira anapiga chenga beki zote anaingia ndani ya 18 anawavuruga wote anafanya anavyotaka. Wakati mwngn naona ninja ni beki Sana kuliko mwamnyeto.

8. Yacouba: jamaa ni kama anacheza kistar Sana sioni kama huwa anapambana Sana uwanjani zaidi namuona mda mwng kazubaa na kutembea Tu akipata mpira si mwepesi WA kufanya maamuzi Ila anapenda akimbie nao mwisho WA SKU hakuna madhara. Pia kufungu kwake ni nadra sn anaweza pata nafasi mtu unasema kbs hili ni goal lakini unashangaa anapga nje huko. Ajitahidi hasa kwny kutumia nafasi.

9. Fei: sina tatzo naye Kwa kweli huyu dogo anapambana Sana hata Jana ilibidi arudi nyuma kidogo kuwasaidia akina mukoko na wakati mwngn ilibidi awatafutie mpira akina makambo mbele ya mabeki WA rivers.

10. Djgui: kipa huyu kijana Yuko vzuri na anaonekana anaumia Sana juu ya beki zake kuwa butu nilimuona kuna muda tukoswakoswa mpk akapga teke mlingoti WA goli Kwa hasira maana beki zlionyesha uzembe kbs.

Huu ni mtazamo wangu bt all in all tuna wachezaji wazuri Ila hawana maandalizi kbs kwasasa tuwe wavumilivu ila club bingwa tumeshatolewa Kwa kifupi hakuna jipya watafanya yanga kile Nigeria huu ndo ukweli. Ila msimu huu tutafanya vzuri kwenye ligi. Sjawaona Simba Ila sidhan km msimu watakuwa vizuri kutuzidi.

dah kaka hebu wape mechi kadhaa walau.. yaan umesimanga team nzima.. kumbuka hawana fitness bado miili haijakaa sawa ... na bado pattern za uchezaji bado hazijakubali

kwangu mie yanga wana bonge la team kilichokosekana no fitness na chemistry yaan wajajuana wachezaj uchezaj wao.. so kila mtu alikuwa anachezea kipaji na uzoefu

ndo maana unaona kila mtu kafanya makosa.. ukiangalia beki zilivyopanda unajiuliza hawa hawafanyi hata coordination wanapanda kwenye mstar ulio flat wakipitwa wanapitwa wote hii inakuonyesha kuwa pattern za uchezaj hazijakaa sawa. ki team

ila wakishapata chemistry winga zikajua mikimbio na speed ya strikers beki zikajuana zenyewe kwa zenyewe then team itakuwa na uwezo wa kupambana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom