Hahahahaaaaaa!!!!...kila mtu anajitoshelezakila mtu humu hakopeshi.. je wanaokopa na wanasumbua kulipa ni kina nani? jamiiforums kila mtu tajiri.. kila mtu ana uwezo.. hakopeshi pesa....
Utamkopeshaje ndugu yako wa damu?Hakika ndugu ndio hovyo kbs, rafiki unaweza kumuharasi hata kuvunja urafiki na ukamshtaki kama ni pesa nyingi. ndugu utamfanyaje? alichonifanyia ndugu wa damu sina hamu kbs!
Mimi nilijifunza siku ndugu yangu alipokuwa na shida. Nikamwonea huruma nikamwazima.
Na yeye akasema baada ya siku tano tu nakurudishia pesa zako. Loh.ndo nilipojuta , kapata hela zake hata alikumbuka kama nilimwazima pesa. , nikasema nimkumbushie baada ya mwezi kupita. Alooo. Nilisimwangwa, we nae unanidai dai tu. Niliishiwa kulipwa elfu tano, kesho kumi., mpaka ilifikia kipindi nikasemehe iliyobaki. Na wala hajajiongeza animalizie.
Nikauchuna. Shida haina adabu. Alikuja analia anashida ile mbaya. Nilimwambia sina hela. Japo nilikuwa nayo. Na nilishajiapiza kama ntampa pesa yoyote ile nampa tu na sio kama deni
Mimi nilimkopesha mwanangua hela kwenye kulipana analeta ubaba na utoto......nikaenda kwake nikamkuta mkwe anapika yeye na mwanaye wanaangalia tamthilia kwenye king'amuzi cha Azam......nikaingia nikasalimia nikachomoa waya wa tv kwenye umeme....nimpa kijana niliyekuja naye akaweka begani huku yeye akibaki mdomo wazi.......baada ya siku mbili akaja akanilipa deni langu na riba juu......
Nikamwambia sisi wapare mtu na mwanaye hatukopeshani ila tunasaidiana...next time ukija kwangu omba msaada sio Mkopo.........
NB;
Kudai deni kwa mtu unayemjua kunataka uwe na ngozi ngumu kama ya kenge na uwe tayari kwa lolote......
kuna taasisi za kifedha iyo ndio kazi yake kuu ya kukopesha.ndugu na rafiki naona mnasema hamtawakopesha sasa je mtawakopesha msiowajua au ndo gia ya kuacha kukopesha watu