Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 3,157
- 6,039
Mimi ni muumini wa Kanisa Katoliki na siku ya Leo ni siku ya amri ya kanisa, Kwamba ni lazima kuhudhuria misa ya Ijumaa kuu.
Katika Ibada ya Ijumaa kuu moja ya sehemu ya Ibada ni maombi mbalimbali yanayotolewa kuyaombea mataifa, viongozi wa dini na serikali, walegevu wa imani, wasiomwamini Mungu, Wenye vita, Njaa n.k
Ni kweli kwamba wapo wahubiri wanaoliombea Taifa kwa ujumla lakini hapa ninazungumzia kumwombea yule ambaye anaonekana kutofautiana kwa namna moja ama nyingine kwa zaidi ya mara moja. Tena kwa kumtaja wazi.
Leo katika Ibada moja kati ya maombi yaliyotajwa ilikuwa kuwaombea waumini wote wa madhehebu mengine ya kikristu.
Nikawaza, Moja kati ya kanisa linaloongoza kwa kushambuliwa na madhehebu mengine ni hili la RC likishutumiwa kwa mambo mbalimbali kama vile kubadili Sabato, kuitwa mpinga Kristu n.k Lakini pamoja na yote bado Kanisa linawaombea na kuwakumbuka waumini wote wakristu na madhehebu yao popote walipo.
Jambo hili limenifunza unyenyekevu wa hali ya juu kama muumini wa Kristu ni jambo la muhimu na la pekee sana.Hata pale unapodhulumiwa na kushitakiwa kwa uongo ukiwa kama Mkristu unapaswa kuwa mnyenyekevu kama jinsi Kristu alivyokuwa mnyenyekevu hata pale aliposhtakiwa kwa uongo, Kanisa linatufundisha kuwa wanyenyekevu daima.
Nawatakia Ijumaa Kuu Njema na Maandalizi Mema Ya Pasaka