Nilichojifunza leo katika Ibada ya Ijumaa Kuu

Kwamba mkuu unataka kuniambia nikila nyama ijumaa kuu ni dhambi?
Ndiyo ni dhambi. Si hivyo tu, Usipohudhuria misa na sikukuu zilizoamriwa ni dhambi, Usiposhiriki Ekaristi ni dhambi, Usiposali sala ya asubuhi,jioni,usiku ni dhambi, Usipofunga ndoa na kuishi na mwanamke/mwanaume ni dhambi n.k n.k
 
Twende Pole pole mkuu.
Dhambi ni uasi dhidi ya Mungu, maana yake ni kwenda kinyume na maagizo (amri) za Mungu.
Sasa amri za kanisa sio amri za Mungu, Mungu atanihukumu vipi kwamba nimetenda dhambi kwa kula nyama ijumaa kuu wakati katika maagizo yake hakuna hilo? Ukumbuke anayehukumu juu ya dhambi ni Mungu pekee sio kanisa
 
Sifuati sheria za RC maana wao wamebadili sheria nyingi za kwenye biblia hata jumapili sio siku ya kuabudu Sisi siku ya pasaka tumesali leo.
 
Hivi RC si ndilo dhehebu kongwe Tanzania, nyie mlipoanzisha hivi kanisa vyemu hivi vya sadaka, mkatengeneza vipengele vyemu, ili mradi kujiweka kando na ili mkombe hela watu.
 
Twende Pole pole mkuu.
Dhambi ni uasi dhidi ya Mungu, maana yake ni kwenda kinyume na maagizo (amri) za Mungu.
Sasa amri za kanisa sio amri za Mungu, Mungu atanihukumu vipi kwamba nimetenda dhambi kwa kula nyama ijumaa kuu wakati katika maagizo yake hakuna hilo? Ukumbuke anayehukumu juu ya dhambi ni Mungu pekee sio kanisa
Mwalimu wako anapokuagiza ukashike jembe ukalime kisha ukakataa na kumtukana unadhani utakuwa umetenda dhambi au la? Kuna amri ya Mungu inasema Usitukane? Vipi wenye majivuno,dharau,jeuri,kiburi n.k wanaenda kinyume na amri zipi? Mungu amemuagiza na kumruhusu mwanadamu kuwa na kiburi?
 
Nikawaza, Moja kati ya kanisa linaloongoza kwa kushambuliwa na madhehebu mengine ni hili la RC likishutumiwa kwa mambo mbalimbali kama vile kubadili Sabato, kuitwa mpinga Kristu n.k Lakini pamoja na yote bado Kanisa linawaombea na kuwakumbuka waumini wote wakristu na madhehebu yao popote walipo.
Na dini zingine pia
 
Ndiyo ni dhambi. Si hivyo tu, Usipohudhuria misa na sikukuu zilizoamriwa ni dhambi, Usiposhiriki Ekaristi ni dhambi, Usiposali sala ya asubuhi,jioni,usiku ni dhambi, Usipofunga ndoa na kuishi na mwanamke/mwanaume ni dhambi n.k n.k
Umemaliza Mkuu,sitii neno.
 
Sifuati sheria za RC maana wao wamebadili sheria nyingi za kwenye biblia hata jumapili sio siku ya kuabudu Sisi siku ya pasaka tumesali leo.
Ok!!!, Kwani kuna mtu aliyekulazimisha??. Endeleeni kuvaa sare km wanajeshi ambapo hamjaagizwa popote ktk Biblia.
 
Mimi ni muumini wa Kanisa Katoliki na siku ya Leo ni siku ya amri ya kanisa, Kwamba ni lazima kuhudhuria misa ya Ijumaa kuu.

Katika Ibada ya Ijumaa kuu moja ya sehemu ya Ibada ni maombi mbalimbali yanayotolewa kuyaombea mataifa, viongozi wa dini na serikali, walegevu wa imani, wasiomwamini Mungu, Wenye vita, Njaa n.k

Ni kweli kwamba wapo wahubiri wanaoliombea Taifa kwa ujumla lakini hapa ninazungumzia kumwombea yule ambaye anaonekana kutofautiana kwa namna moja ama nyingine kwa zaidi ya mara moja. Tena kwa kumtaja wazi.

Leo katika Ibada moja kati ya maombi yaliyotajwa ilikuwa kuwaombea waumini wote wa madhehebu mengine ya kikristu.

Nikawaza, Moja kati ya kanisa linaloongoza kwa kushambuliwa na madhehebu mengine ni hili la RC likishutumiwa kwa mambo mbalimbali kama vile kubadili Sabato, kuitwa mpinga Kristu n.k Lakini pamoja na yote bado Kanisa linawaombea na kuwakumbuka waumini wote wakristu na madhehebu yao popote walipo.

Jambo hili limenifunza unyenyekevu wa hali ya juu kama muumini wa Kristu ni jambo la muhimu na la pekee sana.Hata pale unapodhulumiwa na kushitakiwa kwa uongo ukiwa kama Mkristu unapaswa kuwa mnyenyekevu kama jinsi Kristu alivyokuwa mnyenyekevu hata pale aliposhtakiwa kwa uongo, Kanisa linatufundisha kuwa wanyenyekevu daima.

Nawatakia Ijumaa Kuu Njema na Maandalizi Mema Ya Pasaka
Hivi Kristu ndo kitu gani
 
SAUT watu wanasoma bure? Au hizo sehemu ulizoorodhesha wanatowa huduma bure?

Umelewa divai eheee?
Umeshawahi kuwa na hela na hakuna cha kununua? Haya niambie chuo gani watu wanasoma bure? Hiyo mikopo inayodaiwa kwa watanzania na serikali unataka kusema nini?
 
Hi
Mwalimu wako anapokuagiza ukashike jembe ukalime kisha ukakataa na kumtukana unadhani utakuwa umetenda dhambi au la? Kuna amri ya Mungu inasema Usitukane? Vipi wenye majivuno,dharau,jeuri,kiburi n.k wanaenda kinyume na amri zipi? Mungu amemuagiza na kumruhusu mwanadamu kuwa na kiburi?
Hivyo vyoote ulivotaja vinaangukia kwenye upendo maana kama unampenda mwenzako huwezi kumtukana, kumdharau nk
Nakuuliza nikila nyama ijumaa kuu ni dhambi inayoangukia wapi? Ni uasi dhidi ya Mungu?
 
Basi hata kufunga kula nyama siku ya Ijumaa kuu inaangukia katika amri hiyo hiyo ya Upendo.Ukimpenda Kristu na kukumbuka jinsi alivyoteswa kwa ajili ya dhambi zetu hauwezi kula Nyama.Pia ukipenda na kutii taratibu na sheria za Kanisa lake takatifu ambalo ndilo mwili wa Kristu, Basi hauwezi kwenda kinyume na amri zake zilizowekwa kwa upendo.
 
Amina.
 
Back
Top Bottom