Mwenzenu huwa nachukua mda kutafakali kusudio la Mungu kumleta mwanadamu duniani kwa kila tukio linapotokea:
Lakini nimegundua kuna kundi la watu MHimu sana jamii huwa hailipi kiaumbele;
hili kundi ndilo linaloifanya jamii iheshimike, hili kundi ndilo linaoijenga nchi, lakini wachache waliopewa mamlaka ndiyo wanaoonekana peke yao!
Nimesikiliza Viongozi mbalimbali wakianza hotuba kwa kushukuru jitihada za watu mashuhuli tuu kiitifaki kwa wanasiasa, lakini kundi hilo halimo!
Imenitafakarisha sana Maisha ya hapa duniani.
Ebu tafakari haya;
Hii imenifanya niamini kabisa binadamu hushughulika na finishing na si chanzo, Binadamu hushughulika na mwili na si roho, Binadam hushughulika na ajali na sio kinga, Binadamu hughalamikia misiba na sio kuponya,
Haya yote yanasababishwa na kutoijua kesho yetu kama binadamu, Laiti kama tungeijua kesho yetu hata nyimbo za huzuni tusingeimba, laiti kama tungejua kwamba Vipaji hutoka kwa Mungu tusingezarauliana,
Magorofa haya yanajengwa na watu wadogo sana lakini sifa anapewa mwingine hao hawatajwi, barabara zinajengwa na watu Wa kawaida lakini sifa anapewa mwingine, makaburini wanaoshiriki kuzika ni watu Wa kawaida sana ambao hata wakija majumbani mwenu hamuwapi hata viti vya kukaa,
NINACHOKIAMINI HATA KWENYE KITI CHA MAMLAKA YA JUU DUNIANI, BADO TUNAKALIA MATAKO YETU!
kwahiyo tutengeneze utamaduni Wa kutambua makundi ya watu wadogo kwani wao ndio chimbuko la umaarufu & utajili wako .
Ukiona una vyeo tumia cheo chako kuwasaidia hawa watu, Boresha huduma zao, boresha miundombinu, Huduma za kijamii, Usiwafanye watu hao kusononeka wakati tamko lako ni tiba kwao!
Tambua watu hao ndiowatakaokuchimbia kaburi lako wakati hao viongozi wenzako, mabosi wenzako unaowathamini na kuwadhania hakuna hata mmoja atakaebeba jeneza lako.
Tujifunze kuliweka kundi hilo kwenye itifaki. Aksante

- Wavuvi wenye mtumbwi ndiyo watu Wa kwanza kabisa kuona,kutoa taarifa na kuokoa lakini sijasikia angalau wakikumbukwa kiitifaki au sijaona wakipewa neno la kutiwa moyo angalau kutambulika kazi zao, pamoja na kwamba media ukiona zinazungumzia wavuvi ujue kwamba wanazungumziwa kwa uvuvi haram,n.k
- Njoo kwenye mazishi, coverage IPO zaidi kwa wanaoweka mashada lakini walioshika makoleo hawaonekani.