Nilichojifunza kwenye ajali na matukio makubwa

hili tabaka ndilo linaloleta maendeleo kuna kila sababu Mimi nawaheshimu mno hawa watu
yan siku ambayo tutaanza kulieshimu ili tabaka la chini ndo siku afrika(Tanzania) itaanza kusonga mbele maana hawa ndo wanajenga uchumi wetu wa kila siku achana na hao wanaoenda kufanya shopping dubai
 
Mkuu umenikumbusha ya mlinzi getini kufokewa akichelewa kufungua geti na dada wa ndani kula peke yake.

Ilhali hao watu wameshikilia utu wetu kwa asilimia 50%.
 
yan siku ambayo tutaanza kulieshimu ili tabaka la chini ndo siku afrika(Tanzania) itaanza kusonga mbele maana hawa ndo wanajenga uchumi wetu wa kila siku achana na hao wanaoenda kufanya shopping dubai
njia ni rahisi sana ni kitendo cha kuwapunguzia foleni wananchi katika huduma zote mhimu za kijamii kama maji, Umeme ,afya na barabara na vyakula
 
Hakika inasikitisha na kuvunja moyo kuona akishukuriwa aliyeokoa mmoja na kuwaacha waliookoa 40!
 
we jamaa umeandika kitu cha maana sana na ni ukweli mtupu, tatizo pengine nature ya binadamu haiku hivyo,credit huwa haiendi kwa mtu wa kawaida hata siku moja
hapana ndugu sio wote wenzetu walio endelea wanathamin sana raw material ila sisi wa africa tuna thamin final goods ndo maana hata mkulima hathaminiw katika nchi hiz anathaminiwa bakhresa mtengeneza unga
 
njia ni rahisi sana ni kitendo cha kuwapunguzia foleni wananchi katika huduma zote mhimu za kijamii kama maji, Umeme ,afya na barabara na vyakula
ni kwel kabisa lazima tumpunguzie ugumu wa maisha kupitia hizi huduma za muhimu hazipate bila shida ikiwezekana tena ziwe katika bei ya chini
 
hapana ndugu sio wote wenzetu walio endelea wanathamin sana raw material ila sisi wa africa tuna thamin final goods ndo maana hata mkulima hathaminiw katika nchi hiz anathaminiwa bakhresa mtengeneza unga
ni kweli mkulima ndiye anaeanzisha mchakato mzima kupanda mbegu
 
ni kweli mkulima ndiye anaeanzisha mchakato mzima kupanda mbegu
Ila kwa upande mwingine pia huyu tabaka la chini akijua thamani yake itasaidia sana maana ataijua nguvu yake katika maendeleo ya nchi hii leo hii wakulima wakigoma akuna mtu katika nchi hii atapona .ata leo wavuvi wangegoma akuna mtu ambaya angepatika akiwa hai kwenye ajali
 
Kila binadamu ana umuhimu wake hapa duniani,na kila binadamu anayo haki ya kuheshimiwa nakuthaminiwa,

Meneja wa kampuni hawezi kua meneja bora bila kupata sapoti toka kwa wafanyakazi wa chini,

Ukitaka kua meneja bora hakikisha unajenga mahusiano mazuri kati yako na wafanyakazi wa level zote.
 
ni kwel kabisa lazima tumpunguzie ugumu wa maisha kupitia hizi huduma za muhimu hazipate bila shida ikiwezekana tena ziwe katika bei ya chini
inashangaza vile mwananchi analipia huduma bei kubwa na haipati hadi atoe rushwa ie. Umeme na maji
 
Ila kwa upande mwingine pia huyu tabaka la chini akijua thamani yake itasaidia sana maana ataijua nguvu yake katika maendeleo ya nchi hii leo hii wakulima wakigoma akuna mtu katika nchi hii atapona .ata leo wavuvi wangegoma akuna mtu ambaya angepatika akiwa hai kwenye ajali
bahati nzuri hawa watu kawaajalia moyo Wa huruma,
 
Hakika inasikitisha na kuvunja moyo kuona akishukuriwa aliyeokoa mmoja na kuwaacha waliookoa 40!
kule ufaransa yule kijana aliyejitolea kumwokoa mtoto alipothaminiwa, ilichangia sana kutia moyo wananchi kujitolea
 
bahati nzuri hawa watu kawaajalia moyo Wa huruma,
Kuna watu wanaamini kua "Tenda wema uende zako usingoje shukrani" hakuna jambo jema utakalolifanya na likapita bure,Mungu atakulipa tu,kama sio hapa duniani basi utalipwa siku ya hukumu,

Ushauri wangu ni kwamba tuendelee tu kujitolea hasa katika kusaidia wenzetu katika majanga,malipo yapo mbele ya Muumba wetu.
 
Mwenzenu huwa nachukua mda kutafakali kusudio la Mungu kumleta mwanadamu duniani kwa kila tukio linapotokea:
Lakini nimegundua kuna kundi la watu MHimu sana jamii huwa hailipi kiaumbele;
hili kundi ndilo linaloifanya jamii iheshimike, hili kundi ndilo linaoijenga nchi, lakini wachache waliopewa mamlaka ndiyo wanaoonekana peke yao!
Nimesikiliza Viongozi mbalimbali wakianza hotuba kwa kushukuru jitihada za watu mashuhuli tuu kiitifaki kwa wanasiasa, lakini kundi hilo halimo!
Imenitafakarisha sana Maisha ya hapa duniani.

Ebu tafakari haya;
  • Wavuvi wenye mtumbwi ndiyo watu Wa kwanza kabisa kuona,kutoa taarifa na kuokoa lakini sijasikia angalau wakikumbukwa kiitifaki au sijaona wakipewa neno la kutiwa moyo angalau kutambulika kazi zao, pamoja na kwamba media ukiona zinazungumzia wavuvi ujue kwamba wanazungumziwa kwa uvuvi haram,n.k
  • Njoo kwenye mazishi, coverage IPO zaidi kwa wanaoweka mashada lakini walioshika makoleo hawaonekani.

Hii imenifanya niamini kabisa binadamu hushughulika na finishing na si chanzo, Binadamu hushughulika na mwili na si roho, Binadam hushughulika na ajali na sio kinga, Binadamu hughalamikia misiba na sio kuponya,
Haya yote yanasababishwa na kutoijua kesho yetu kama binadamu, Laiti kama tungeijua kesho yetu hata nyimbo za huzuni tusingeimba, laiti kama tungejua kwamba Vipaji hutoka kwa Mungu tusingezarauliana,

Magorofa haya yanajengwa na watu wadogo sana lakini sifa anapewa mwingine hao hawatajwi, barabara zinajengwa na watu Wa kawaida lakini sifa anapewa mwingine, makaburini wanaoshiriki kuzika ni watu Wa kawaida sana ambao hata wakija majumbani mwenu hamuwapi hata viti vya kukaa,
NINACHOKIAMINI HATA KWENYE KITI CHA MAMLAKA YA JUU DUNIANI, BADO TUNAKALIA MATAKO YETU!
kwahiyo tutengeneze utamaduni Wa kutambua makundi ya watu wadogo kwani wao ndio chimbuko la umaarufu & utajili wako .
Ukiona una vyeo tumia cheo chako kuwasaidia hawa watu, Boresha huduma zao, boresha miundombinu, Huduma za kijamii, Usiwafanye watu hao kusononeka wakati tamko lako ni tiba kwao!
Tambua watu hao ndiowatakaokuchimbia kaburi lako wakati hao viongozi wenzako, mabosi wenzako unaowathamini na kuwadhania hakuna hata mmoja atakaebeba jeneza lako.
Tujifunze kuliweka kundi hilo kwenye itifaki. Aksante
Uchambuzi mzuri, ni kweli hata mama nyumbani anasifiwa watoto wana afya nzuri lakini anayehangaika nana bakuli la uji kwa masaa mawili ili mtoto ashibe nina dada wa kazi, lakini wengine hata hawathamini, ofisini mhudumu(msaidizi wa ofisi), ndo anafanya kazi nzuri ofisi ikaonekana, bosi anasifiwa taarifa nzuri lakini ps ndo kaipanga na kurekebisha hadi lugha mana mabosi wengine wanaandika kiswahili cha kilugha chao. Kila mmoja aheshimu wasaidizi wake
 
kuna kisa kimoja jamaa alikuwa na Duka lake, lakini kila siku asubuhi alipokuja kufungua alimkuta mtu masikini kichaa kalala mlangoni akamtimua na mateke, lakini yule kichaa hakukoma kuja kulala pale, yule mmiliki Wa Duka alikasilika na kumpiga teke la tumbo lililopelekea yule kichaa kuugua hadi kufa, lakini baada ya kufa yule kichaa, lile Duka liliibiwa vitu vyote vya ndani, yule mwenye Duka katika kuangalia CCTV camera aligundua kwamba wale wezi walianza siku nyingi kuja kuvunja kufuri lakini yule kichaa ndiye alikuwa akiwatimua! na pindi alipokufa ndipo wakafanikiwa kuiba!
INAUMA SANA
 
Hata wachimba visima huangaika sana namadrill pipe pindi wakiwa site na mda mwingine hushinda na kulala bila kutokana na kipato kidogo wanachopewa na wakubwa wao ,lakin yakipatikana maji sifa zote huenda kwa mkurugenzi ambaye hata tabu ya site haijui anashinda kwenye kiyoyozi
 
Back
Top Bottom