Nilichojifunza kwenye ajali na matukio makubwa

Negligence ndiyo kikwazo hasa kwa sisi waafrika; tupo tofauti sana na watu weupe
Daladala linajaa mara 2 hakuna anayejali akiwemo abilia mwenyewe
Mwendo kasi unajaa mara 2 hakuna anayejali akiwemo abilia mwenyewe
Train linajaa mara 3 zaidi hakuna anayejali akiwemo abilia mwenyewe
Pantoni na vivuko huko sitaki hata kusema!!
Malori ya kwenda na kurudi minadani huko nako sitaki kusema!!

Kitu ambacho hakijai kujaa hapa Africa ni usafiri wa Ndege tu na huo ni sababu za kiusalama za kimataifa, tungekuwa na mamlaka na huko watu wangesimama au kulala chini ya viti.

Nafirkiri tutahitaji karne nyingi sana kubalidilika; si leo wala kesho na haya majanga yataendelea kutumaliza.
 
Kila binadamu ana umuhimu wake hapa duniani,na kila binadamu anayo haki ya kuheshimiwa nakuthaminiwa,

Meneja wa kampuni hawezi kua meneja bora bila kupata sapoti toka kwa wafanyakazi wa chini,

Ukitaka kua meneja bora hakikisha unajenga mahusiano mazuri kati yako na wafanyakazi wa level zote.
Siku watu wote wakilitambua hili na kuliishi, hakika dunia kutakuwa mahali salama pa kuishi
 
Hakika
Ila hii ipo katika nyamja nyingi si ajali na majanga.
Kwa mfano jeshi la polisi linapotekeleza ops fulan kwa usahihi kama kupambana na wahalifu, credit zote wanapewa hawa wa ofisini kina Sir_0 na kina Mur_t0 na sio wale maaskari wenye vyeo vya chini wanaopishana na risasi field.
Ila wanapofanya vibaya ni kinyume chake
 
Hakika
Ila hii ipo katika nyamja nyingi si ajali na majanga.
Kwa mfano jeshi la polisi linapotekeleza ops fulan kwa usahihi kama kupambana na wahalifu, credit zote wanapewa hawa wa ofisini kina Sir_0 na kina Mur_t0 na sio wale maaskari wenye vyeo vya chini wanaopishana na risasi field.
Ila wanapofanya vibaya ni kinyume chake
wakifanya vibaya wanafukuzwa wao, wakifanya vizuri pongezi anapewa aliyeko juu
 
kuna kisa kimoja jamaa alikuwa na Duka lake, lakini kila siku asubuhi alipokuja kufungua alimkuta mtu masikini kichaa kalala mlangoni akamtimua na mateke, lakini yule kichaa hakukoma kuja kulala pale, yule mmiliki Wa Duka alikasilika na kumpiga teke la tumbo lililopelekea yule kichaa kuugua hadi kufa, lakini baada ya kufa yule kichaa, lile Duka liliibiwa vitu vyote vya ndani, yule mwenye Duka katika kuangalia CCTV camera aligundua kwamba wale wezi walianza siku nyingi kuja kuvunja kufuri lakini yule kichaa ndiye alikuwa akiwatimua! na pindi alipokufa ndipo wakafanikiwa kuiba!
INAUMA SANA
Nakumbuka sana hii video, mwenye duka alipata maumivu sana baada yaya kuona hiyo video
 
Back
Top Bottom