Nilichojifunza kuhusu ajira za mitandaoni

Joel360

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
981
631
Mimi ni miongoni mwa watu ambao wamehangaika sana kutafuta ajira. Nimekaa miaka 2 mtaani mpaka nilipokuja kupata ajira mwaka huu.

Kuna websites huwa zina matangazo ya ajira. Sitaki kuzitolea mfano maana sitaki kuchafua website yoyote. Na lengo la hii post sio kuchafua website yoyote ila kushare tu kile ambacho mimi nimejifunza katika kutafuta ajira. Katika post hii sizungumzii ajiraportal. Binafsi niseme nina imani sana na ajira portal. Japo mimi sijawahi pata ajira kupitia ajira portal ila nawafahamu watu waliopata ajira kupitia ajira portal. Sizungumzii ajira za serikali zinazotangazwa ajira portal.

Nazungumzia website nyingine za ajira (ambazo zinatangaza ajira kutoka private sector). Website hizi huwa zina matangazo ya ajira kutoka kampuni kubwa za hapa nchini na katika matangazo hayo huwa inaelekezwa mpaka jinsi ya kutuma maombi, lakini nilichokiona (kwa upande wangu) matangazo haya huwa yanawekwa kutimiza wajibu tu.

Inasemekana kwamba, taratibu zinawataka waajiri watangaze ajira mtandaoni (kwenye websites) kwa hiyo baadhi ya waajiri (sio wote, ila asilimia kubwa) hutangaza kwa lengo la kutimiza wajibu tu, lakini nafasi inakuwa imeshazibwa tayari. Kwahiyo tunatuma maombi tukijua maombi yetu yatasomwa lakini hilo suala halitokei kutokana na kwamba nafasi imeshapata mtu tayari.

kwahiyo nilichojifunza baada ya kutuma sana maombi kwenye ajira zinazotangazwa kwenye websites za ajira na kutoitwa hata interview moja ni kwamba: ni ngumu sana kupata ajira kwa njia ile.

Niia gani nimeitumia kupata ajira mwaka huu?
Nimetoka mkoa niliopo nikaja Arusha kwa rafiki yangu ambae nilisoma nae chuo. Nikiwa hapa nikashauriwa nijiunge na Instagram na kufollow Page za ajira za Instagram, nikajiunga na magoup yao ya whatsApp. Basi baadhi ya watu wakawa wanashare ajira mbali mbali. Baadhi ya ajira ukipiga simu unakuta haipokelewi, nyingine haipatikani ila nyingine anapokea anakwambia kwamba mtu kashapatikana. Nikiwa kwenye group ikatumwa ajira ya ualimu kutoka Steps Academy. Nikapiga nikaambiwa nipeleke vyeti nikapeleka nikasubiri kuitwa kwa ajili ya interview. Niseme tu wala sikuamini kama ntaitwa, ila niliitwa. nikafata utaratibu wao wa interview, mwishowe nikapata. (mimi nimesoma ualimu)

Ajira nyingi zinatangazwa ila hazitufikii kwa sababu hatutaki kutoka vijijini tulimozaliwa na kusoma. Si lazima utoke huko uliko. Unaweza kuchukua simu yako, ukaja hapa Jamiiforums ukatafuta watu wanaotafuta ajira kama yako mkawa mnapeana habari na mwishowe mkaunda group mkawa mnashea taarifa za nafasi za ajira, ukajikuta umeshapata ajira kwa njia hiyo.

Kama unaona kazi kufanya hivyo nenda Instagram tafuta page za matangazo ya ajira. Zipo nyingi tu, kuna 'ajirachap', 'ajira na biashara', 'ajiraleo', 'ajiraonline' , 'ajirazone', 'ajira michezo biashara' na nyingine nyingi.

Kwa kutafuta urahisi, tafuta: @ajirazone. Hii mimi ndio ninayoipenda kuliko zote. Kwanza wanapost matangazo ya ajira karibia kila siku halafu kujiunga kwenye group lao la whatsApp ni bure (wengine wanatoza buku 2). Lakini pia link ya kujiunga na group lao la whatsApp iko pale pale kwenye page yao (bio) ya Instagram. Nisuala la kubonyeza link tu tayari umeshajiunga. Nenda kwenye Instagram search, andika "ajirazone", itakuja page yenye hilo jina.

Hata kama bado hujakata tamaa na ajira za website sio mbaya pia kujaribu kutafuta ajira kupitia ma group ya whatsApp. niwatakie siku njema.
 
Mtu anaweza kujiunga na group lolote lile, magroup yapo mengi sana. Kuna ajirachap, ajira na biashara, uwanja wa ajira. Ila mimi nimejiunga kwenye ajirazone maana wao hawakusema kwamba kuna kutoa hela kujiunga kwenye group lao.
Hivi jamani mnambie, kumbe kuna magroup mtu anatakiwa atue hela ajiunge ?
 
Ni kweli mkuu ulicho kisema, kuna chuo fulani hivi huwa kinatangaza ajira kila mwaka, kuna siku nilituma maombi baada ya siku kadha nikapigiwa simu kwenda kwenye interview, bahati zuri tulivyo toka tukapeana namba za simu, ili kupeana taarifa mbali mbali za kazi, Lakin ile interview hakuna aliye pita,

Mpaka leo hii miaka miwili sasa inatimia hiyo nafasi bado ipo, na juzi juzi nimeona wametangaza tena hiyo nafasi ili watu watume maombi..

Sasa hapa huwa najiuliza, huwa wanatangaza ajira ili kupromote biashara zao ama wana maana gani,
 
Ni kweli mkuu ulicho kisema, kuna chuo fulani hivi huwa kinatangaza ajira kila mwaka, kuna siku nilituma maombi baada ya siku kadha nikapigiwa simu kwenda kwenye interview, bahati zuri tulivyo toka tukapeana namba za simu, ili kupeana taarifa mbali mbali za kazi, Lakin ile interview hakuna aliye pita,

Mpaka leo hii miaka miwili sasa inatimia hiyo nafasi bado ipo, na juzi juzi nimeona wametangaza tena hiyo nafasi ili watu watume maombi..

Sasa hapa huwa najiuliza, huwa wanatangaza ajira ili kupromote biashara zao ama wana maana gani,
Huwa wana fanya kwa sababu mbili.

1. Huwa wanafanya ku-promote biashara yao. Wanajua wakisema wanahitaji wafanya kazi basi watatengeneza awareness flani katika jamii kuwahusu.

2. Wanafanya ili kutimiza sheria na taratibu. Naskia (sijafanya utafiti) wanatakiwa na sheria na taratibu kutangaza nafasi za ajira za wafanyakazi wao ili kukidhi leseni zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom