Nilichojifunza katika msiba wa mama yake Sugu

Tee Bag

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
7,220
Reaction score
5,627
NILICHOJIFUNZA KATIKA MSIBA WA MAMA YAKE SUGU

MOSI ni uhusiano wa kijamii. Pili ni mahakama na athari za uamuzi wake.

UHUSIANO

Katika ibada ya kumwombea mama yake Sugu, Desderia Mbilinyi, Muhimbili, hakuwepo mbunge hata mmoja wa CCM. Hakukuwa na 'kampani' yoyote ya kibunge. Hakuna ofisa wa Bunge aliyekuwepo kuonesha Bunge lilikuwa bega kwa bega.

Sugu ni mbunge. Amefiwa na mama yake mzazi. Tofauti za kisiasa ni tunda tamu la demokrasia. Siasa hazipaswi kuathiri uhusiano wa kijamii. Siasa kufanya watu wasizikane huo ni ushamba na uzezeta.

Unaweza kuniambia wabunge wa CCM walikuwa na majukumu mengi ya kamati za Bunge. Nitakuuliza; wote? Hata mmoja akosekane kutoa kampani?

Nakumbuka wabunge CCM waliokwenda kumwona Lema gerezani, waliitwa wasaliti. Eti mbunge CCM kumtembelea mbunge wa Chadema mahabusu ni usaliti! Nakumbuka Lissu alilazwa Nairobi baada ya kupigwa risasi, hakuna mbunge CCM aliyekwenda. Nyalandu aliyekwenda aliishia kuhama chama na kujiuzulu ubunge.

Siasa za kishamba. Siasa za Mashikolo Mageni.

MAHAKAMA

Sugu aliposoma wasifu wa marehemu (eulogy), alisema chanzo cha mama yake kuumwa hadi kifo ni mshtuko baada ya Sugu kuhukumiwa kifungo jela, Februari 26, mwaka huu. Sugu alisema, mama yake aliamini alionewa, hivyo alianza kuumwa presha na kusababisha figo zifeli.

Sugu alitoka gerezani Mei 10, mwaka huu. Katika wasifu wa marehemu, Sugu alisema Julai mwaka huu, mama yake alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka mauti yalipomfika.

Kwa alichokisoma Sugu kinajenga imani kuwa Sugu asingefungwa, mama yake asingezidiwa kwa presha. Bila presha kuwa juu sana figo zisingefeli. Mpangaji wa mauti ni Mungu, ila chanzo cha kifo cha mama Sugu kinaonekana ni hukumu ya kifungo jela aliyohukumiwa Sugu.

Hapa kuna ushauri kwa mahakimu na majaji; kazi yao ni nyeti na ngumu. Watu wanaosimama mbele yao na kuwahukumu ni dunia ya wengine. Unamhukumu baba au mama ambaye ni dunia ya mtoto au watoto wake. Unamtia hatiani mtoto ambaye mama yake haoni thamani ya dunia bila mwanaye. Vilevile mke au mume kwa mwenzi wake. Mwisho ni kuzaa maafa!

Ni vizuri uwe umesababisha maafa kwa kutenda haki. Kwamba umemhukumu mtu alichostahili, hata yakitokea maafa itakugusa lakini haisuti nafsi. Ukimhukumu mtu ndivyo sivyo, maafa yakitokea, nafsi itakusuta na laana itakushukia. Maana Mungu hasinzii wala halali!

Kisa cha Andha Kanoon, mke alimuua mtoto akajiua na yeye baada ya Amitabh Bachchan kufungwa jela. Mke aliona dunia yao ni Amita. Hakuna maisha mengine bila yeye. Nilimfahamu kidogo mama Sugu, alimpenda sana mtoto wake. Sugu pia alimpenda sana mama yake. Alimtaja mara nyingi kwenye nyimbo zake, hata hoteli yake, Hotel Desderia, Mbeya ni jina la mama yake.

Haki ndio uhuru wa kweli. Tenda haki na utaishi kwa uhuru duniani mpaka ahera. Mahakimu na majaji wasifanyie biashara haki za watu wala wasizilie njama haki za watu. Ni hatari sana.

Ndimi Luqman MALOTO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni watanzania wachache ndio wanaoelewa kwamba kwa sasa Tz swala la uhuru limrpotea...

Kuwa kira sababu za kusema katika msiba huo kuna maamuz yalitoka juu kuwa jamaaa asipewe ushirikiano wowote

Nnashindwaje kuamin jambo kama hilo kama Lisuu tuu walimmiminia risasi za kutosha na kusema akifa hasipelekwe bungen kuagwa kwa heshima kama mbunge!!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuhizi siasa zimeharibu mahusiano ya kijamii, ukiwa chama hichi hupewa ushirikiano, naona tu ni kiasi gani siasa za kistaarabu zinahtaji watu wasio na mihemko, na wenye high level of maturity, kwanza kibongo kutofautiana mawazo huwa ni kosa tunahtaji kukuwa kiakili aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni watanzania wachache ndio wanaoelewa kwamba kwa sasa Tz swala la uhuru limrpotea...

Kuwa kira sababu za kusema katika msiba huo kuna maamuz yalitoka juu kuwa jamaaa asipewe ushirikiano wowote

Nnashindwaje kuamin jambo kama hilo kama Lisuu tuu walimmiminia risasi za kutosha na kusema akifa hasipelekwe bungen kuagwa kwa heshima kama mbunge!!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hali ilivyo sasa jela hajuna mwenyewe na ukiwa mwana CHADEMA you are more prone to that.
 
Tulikuwa na jaka,benja,Mzee alii na mwalimu mpaka kaenda ahera hatukuwahi baguana ,alipoingia yeye sasa.....wacha kabisa
 
Na hilo ni funzo dogo tuu,sasa je tupo tayari kuendelea na siasa zetu za 'mwisho wa lami'?
Au tufunge breki,halafu suka aturudishe tulipotokea?
Mi mwenyewe sijuii[emoji102]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inasikitisha mno huku ndiko tulikofikia sasa watanzania,hatupeani pole,hatuuguzani,na sasa hatuzikani ;kisa ya yote haya ni kutofautiana kiitikadi ila wote sisi ni watanzania na Tanzania ni nchi yetu wote,chuki,hasira,utumiaji wa nguvu kupita kipimo,hizi zote ni DNA ambazo zinasambaa kwa kasi chanzo chake ni mpangaji mkuu wa pale magogoni,na inashangaza sana kuona eti makanisa na misikiti yetu inatumika kuzidi kumwombea atutawale(sio kutuongoza) kwa amani,nimepoteza kabisa imani yangu kwa kanisa langu(likiwa ni moja yaliyombele kwa hili),watu wanaumizwa,familia zinaishi kwa woga ,watu wanapoteza maisha bila ya serikali kutoa tamko lolote au wahusika kufikishwa mbele ya sheria
 
Katika hoja ulizoweka hapa, ya kwanza ni hoja na kuna cha kujiuliza, hoja ya pili inaonesha kuwa na wewe na SUGU ni WASHAMBA, Kifo chochote kina sababu zake, Mama huyu kafa kwa ugonjwa, sababu za ugonjwa unazotaja ni mbinu bunifu za kujinufaisha kisiasa.

WATU WANAHUKUMIWA KUTUMIKIA VIFUNGO KWA MIAKA MINGI NA KWAO HAKUNA KITU LAKINI WAZEE TEGEMEZI WANAENDELEA KUKOMAA NA MAISHA, IWEJE HUYU MWENYE KILA KITU. ACHA USHAMBA
 
NILICHOJIFUNZA KATIKA MSIBA WA MAMA YAKE SUGU

MOSI ni uhusiano wa kijamii. Pili ni mahakama na athari za uamuzi wake.

UHUSIANO

Katika ibada ya kumwombea mama yake Sugu, Desderia Mbilinyi, Muhimbili, hakuwepo mbunge hata mmoja wa CCM. Hakukuwa na 'kampani' yoyote ya kibunge. Hakuna ofisa wa Bunge aliyekuwepo kuonesha Bunge lilikuwa bega kwa bega.

Sugu ni mbunge. Amefiwa na mama yake mzazi. Tofauti za kisiasa ni tunda tamu la demokrasia. Siasa hazipaswi kuathiri uhusiano wa kijamii. Siasa kufanya watu wasizikane huo ni ushamba na uzezeta.

Unaweza kuniambia wabunge wa CCM walikuwa na majukumu mengi ya kamati za Bunge. Nitakuuliza; wote? Hata mmoja akosekane kutoa kampani?

Nakumbuka wabunge CCM waliokwenda kumwona Lema gerezani, waliitwa wasaliti. Eti mbunge CCM kumtembelea mbunge wa Chadema mahabusu ni usaliti! Nakumbuka Lissu alilazwa Nairobi baada ya kupigwa risasi, hakuna mbunge CCM aliyekwenda. Nyalandu aliyekwenda aliishia kuhama chama na kujiuzulu ubunge.

Siasa za kishamba. Siasa za Mashikolo Mageni.

MAHAKAMA

Sugu aliposoma wasifu wa marehemu (eulogy), alisema chanzo cha mama yake kuumwa hadi kifo ni mshtuko baada ya Sugu kuhukumiwa kifungo jela, Februari 26, mwaka huu. Sugu alisema, mama yake aliamini alionewa, hivyo alianza kuumwa presha na kusababisha figo zifeli.

Sugu alitoka gerezani Mei 10, mwaka huu. Katika wasifu wa marehemu, Sugu alisema Julai mwaka huu, mama yake alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka mauti yalipomfika.

Kwa alichokisoma Sugu kinajenga imani kuwa Sugu asingefungwa, mama yake asingezidiwa kwa presha. Bila presha kuwa juu sana figo zisingefeli. Mpangaji wa mauti ni Mungu, ila chanzo cha kifo cha mama Sugu kinaonekana ni hukumu ya kifungo jela aliyohukumiwa Sugu.

Hapa kuna ushauri kwa mahakimu na majaji; kazi yao ni nyeti na ngumu. Watu wanaosimama mbele yao na kuwahukumu ni dunia ya wengine. Unamhukumu baba au mama ambaye ni dunia ya mtoto au watoto wake. Unamtia hatiani mtoto ambaye mama yake haoni thamani ya dunia bila mwanaye. Vilevile mke au mume kwa mwenzi wake. Mwisho ni kuzaa maafa!

Ni vizuri uwe umesababisha maafa kwa kutenda haki. Kwamba umemhukumu mtu alichostahili, hata yakitokea maafa itakugusa lakini haisuti nafsi. Ukimhukumu mtu ndivyo sivyo, maafa yakitokea, nafsi itakusuta na laana itakushukia. Maana Mungu hasinzii wala halali!

Kisa cha Andha Kanoon, mke alimuua mtoto akajiua na yeye baada ya Amitabh Bachchan kufungwa jela. Mke aliona dunia yao ni Amita. Hakuna maisha mengine bila yeye. Nilimfahamu kidogo mama Sugu, alimpenda sana mtoto wake. Sugu pia alimpenda sana mama yake. Alimtaja mara nyingi kwenye nyimbo zake, hata hoteli yake, Hotel Desderia, Mbeya ni jina la mama yake.

Haki ndio uhuru wa kweli. Tenda haki na utaishi kwa uhuru duniani mpaka ahera. Mahakimu na majaji wasifanyie biashara haki za watu wala wasizilie njama haki za watu. Ni hatari sana.

Ndimi Luqman MALOTO

Sent using Jamii Forums mobile app
Malalamiko ya kutoka ufipa haya.
 
Kweli hapo kwa ugonjwa na maelezo sugu aliingiza siasa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.....duh! Unaenda msibani, then unajilazimisha kujifunza negativity tu? Anyway......hakuna mkamilifu duniani, cha msingi kuwaombea wote hata wale waliotukwaza. Tumuombe mamake sugu alale panapostahili.
 
NILICHOJIFUNZA KATIKA MSIBA WA MAMA YAKE SUGU

MOSI ni uhusiano wa kijamii. Pili ni mahakama na athari za uamuzi wake.

UHUSIANO

Katika ibada ya kumwombea mama yake Sugu, Desderia Mbilinyi, Muhimbili, hakuwepo mbunge hata mmoja wa CCM. Hakukuwa na 'kampani' yoyote ya kibunge. Hakuna ofisa wa Bunge aliyekuwepo kuonesha Bunge lilikuwa bega kwa bega.

Sugu ni mbunge. Amefiwa na mama yake mzazi. Tofauti za kisiasa ni tunda tamu la demokrasia. Siasa hazipaswi kuathiri uhusiano wa kijamii. Siasa kufanya watu wasizikane huo ni ushamba na uzezeta.

Unaweza kuniambia wabunge wa CCM walikuwa na majukumu mengi ya kamati za Bunge. Nitakuuliza; wote? Hata mmoja akosekane kutoa kampani?

Nakumbuka wabunge CCM waliokwenda kumwona Lema gerezani, waliitwa wasaliti. Eti mbunge CCM kumtembelea mbunge wa Chadema mahabusu ni usaliti! Nakumbuka Lissu alilazwa Nairobi baada ya kupigwa risasi, hakuna mbunge CCM aliyekwenda. Nyalandu aliyekwenda aliishia kuhama chama na kujiuzulu ubunge.

Siasa za kishamba. Siasa za Mashikolo Mageni.

MAHAKAMA

Sugu aliposoma wasifu wa marehemu (eulogy), alisema chanzo cha mama yake kuumwa hadi kifo ni mshtuko baada ya Sugu kuhukumiwa kifungo jela, Februari 26, mwaka huu. Sugu alisema, mama yake aliamini alionewa, hivyo alianza kuumwa presha na kusababisha figo zifeli.

Sugu alitoka gerezani Mei 10, mwaka huu. Katika wasifu wa marehemu, Sugu alisema Julai mwaka huu, mama yake alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka mauti yalipomfika.

Kwa alichokisoma Sugu kinajenga imani kuwa Sugu asingefungwa, mama yake asingezidiwa kwa presha. Bila presha kuwa juu sana figo zisingefeli. Mpangaji wa mauti ni Mungu, ila chanzo cha kifo cha mama Sugu kinaonekana ni hukumu ya kifungo jela aliyohukumiwa Sugu.

Hapa kuna ushauri kwa mahakimu na majaji; kazi yao ni nyeti na ngumu. Watu wanaosimama mbele yao na kuwahukumu ni dunia ya wengine. Unamhukumu baba au mama ambaye ni dunia ya mtoto au watoto wake. Unamtia hatiani mtoto ambaye mama yake haoni thamani ya dunia bila mwanaye. Vilevile mke au mume kwa mwenzi wake. Mwisho ni kuzaa maafa!

Ni vizuri uwe umesababisha maafa kwa kutenda haki. Kwamba umemhukumu mtu alichostahili, hata yakitokea maafa itakugusa lakini haisuti nafsi. Ukimhukumu mtu ndivyo sivyo, maafa yakitokea, nafsi itakusuta na laana itakushukia. Maana Mungu hasinzii wala halali!

Kisa cha Andha Kanoon, mke alimuua mtoto akajiua na yeye baada ya Amitabh Bachchan kufungwa jela. Mke aliona dunia yao ni Amita. Hakuna maisha mengine bila yeye. Nilimfahamu kidogo mama Sugu, alimpenda sana mtoto wake. Sugu pia alimpenda sana mama yake. Alimtaja mara nyingi kwenye nyimbo zake, hata hoteli yake, Hotel Desderia, Mbeya ni jina la mama yake.

Haki ndio uhuru wa kweli. Tenda haki na utaishi kwa uhuru duniani mpaka ahera. Mahakimu na majaji wasifanyie biashara haki za watu wala wasizilie njama haki za watu. Ni hatari sana.

Ndimi Luqman MALOTO

Sent using Jamii Forums mobile app
yani sikuizi ndugu wa mwanasiasa akifa tu tayari lawama zinatupiwa kwa Serikali
mambo mengine mnakufuru
 
Back
Top Bottom