Nilichogundua kwenye maisha kuzaliwa tumbo moja sio tiketi ya kusaidiana

Naja naja

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
747
1,452
Unaweza mtu ukawa unaishi maisha ya kidhalili kabisa yasiyo na mbele wala nyuma hali ya kuwa ndugu yako ana mafanikio ya kimaisha.

Inauma sana kuona mtu unaishi maisha ya dhiki hali ya kuwa kuna ndugu yako wa damu tumbo anaweza akakusaidia kukushika mkono kukuvusha kwenye magumu unayopitia.

Inauma zaidi kuona ndugu yako anajali sana marafiki kuliko wewe nduguye.

Inauma zaidi pale wewe kama kaka uone dada yako hakuthamini na kukujali wakati wewe ndiye baadaye utakaye tolewa macho na watoto wa dada yako uwasomeshe kama itatokea dada yako amepata matatizo ya kiuchumi halafu wewe umefanikiwa kimaisha.

Ukikumbuka ya nyuma ulivyosoma kwa tabu na kuishi kwa tabu na ukakataa kuwasomesha watoto wa dada yako utaonekana una roho mbaya.

Kikubwa uhai.
 
Maisha yanabadili watu, wakati wewe ukiona kama hausaidiwi, hujui huyo nduguyo alipita wapi mpaka kua hapo alipo ,

Labda nikufungue macho

Hapo uliposema siku akiyumba kiuchumi wanae watakutolea macho (kwa nilivyo elewa hutowasaidia/utafikiria sana kabla ya kusaidia), nae alikua hapo siku/miaka ya nyuma, pengine akajiapia kabisa siku akifanikiwa hatugeuka nyuma kukumbuka ndugu, pengine sasa ndio anatimiza ahadi yake hiyo, nawe uko kwenye situation hiyo hiyo..utakuja kua hivyo hivyo

Pambana , hakuna ulazima wa nduguyo kukusaidia, n hiar yake
 
Unasemaje mzigo wa watoto ni wako wewe unajua mipango ya kimaisha ya familia yake? Acha kuwa na roho za kichawi wewe kwani nilazima uje kuwasaidia watoto wake? Wamekuomba? Halafu kaa ukijua kutoa ni moyo siyo lazima utangaze au unayemsaidia akulipe.
Mimi na fight kivyangu mkuu.

Simtegemei yeye kwa sababu hakuna anachonisaidia.

Napambana na maisha yangu, ila kinachoniuma ni kwamba najua tu kivyovyote mzigo wa watoto wake ni wa kwangu tu iwe isiwe maana mimi ndo nafuata baada ya yeye ,maana nipo tu na bi mkubwa hakuna mtu mwingine wa kumsaidia

Na mzee alishatutelekeza kitambo tu.
 
Ndugu wengine hataa wakishikwa mkono hawashikiki, unalipa kazi linaishia kula bata ambazo hata wewe hujawahi kula, yaan anagalagaza pesa zako na kuhonga as if aliambiwa wewe hujui kuhonga, by the way pambana na maisha yako, acha excuse na kutegea akili, acha kuwabebesha watu mizigo yako wakati nao wana yao
 
Back
Top Bottom