Nilichogundua kwenye kelele zinazoendelea hapa nchini

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,882
NILICHOGUNDUA KWENYE KELELE ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI

Na, Robert Heriel.
Taikon wa Fasihi

Mayowe kila upande,
Kusini hakuna umeme!
Mashariki hakuna maji,
Kaskazini Tozo
Magharibi vifurushi
Chini Mafuta
Juu mlipuko wa bei!

Kelele siku zote zinamzunguko na mhimili wake. Hata hivyo kuna namna ya kudhibiti kelele hizo.

Chanzo cha kelele wengi watasema SERIKALI imeshindwa kutoa Huduma Kwa wananchi wake, Kwa upande mmoja ni sahihi lakini Kwa upande mwingine si sahihi.

Panaweza kukawa na shida ya umeme na pasiwe za kelele.
Panaweza pakawa na shida ya maji, chakula, gharama za maisha kuwa juu na matatizo mengine lakini pasiwe na kelele.

Kelele na malalamiko Kama nilivyosema yanamhimili na mzunguko wake.

Katika ngazi ya Familia, Baba anaweza asiwe muwajibikaji lakini pasiwe na kelele na malalamiko kutoka Kwa mkewe na Watoto.

Kuna namna kadhaa za kudhibiti kelele/malalamiko. Namna kuu ni hizi zifuatazo kulingana na Akili zangu;

1. Kumbebesha mtu mwingine msalaba
2. Kumpa mchawi mtoto ambebe

Mbinu hizi mbili ndizo mbinu za kidunia zitimikazo kuzima kelele za malalamiko ya watu.

1. Kumbebesha mtu mwingine Msalaba
Mbinu hii imemsibu mhusika dhahania maarufu Duniani aitwaye Shetani.
Kila ubaya wowote uujuayo amepewa Shetani. Yaani Taikon nikikutwa nimechepuka na mwenzi wangu kuepusha kelele na lawama zote namrushia zigo la misumari Shwetani. Nitasema Shetani ndio kanipitia.

Moja ya sababu za kuumbwa Kwa Lusifa ni kuficha udhaifu wa MUNGU, hili najua wengi watanipinga, so Shetani kawekwa kimkakati kuzima kelele za viumbe kuhusiana na udhaifu wowote ambao utajitokeza katika mfumo WA maisha. Yaani lolote Baya likitokea apewe Shetani hata Kama hajafanya yeye. Sijui kama naeleweka.

Kwa upeo wangu mdogo naweza kuona moja ya Role kuu ya Shetani ni kuficha udhaifu wa MUNGU. Iwe Kwa kujua ama laa. Hata hivyo udhaifu wa kimungu Kwa binadamu ni ubora kabisa wa Hali ya juu ndio maana wanadamu wanaamini Mungu sio dhaifu. Na wanaamini Mungu sio dhaifu Kwa sababu ya uwepo wa Shetani yaani aliyebebeshwa zigo la misumari.

Embu imagine Shetani asingekuwepo alafu Yatokee mapungufu Kama Ajali, njaa, matetemeko, tamaa zilizopitiliza, ubinafsi, unafikiri lawama angezibeba Nani?

Ili lawama zifike kwa Mungu ndio maana Shetani akaumbwa Kwa lengo la kubebeshwa lawama na kelele zote za mabaya.

Najua wapo watakaoniona naongea Kama mjinga au Mpumbavu, sitawalaumu Kwa sababu ndivyo walivyofunzwa na kuaminishwa.

Wanasiasa na watawala pia hutumiaga mbinu hii ya kuamisha lawama na wao kujitoa katika kelele hizo.

Hayyati Nyerere na Magufuli walitumia mbinu hii ya kuhamisha kelele za lawama Kwa wengine na wao kujitoa kana kwamba wao hawahusiki.

Kumbuka kanuni kubwa ya kumbebesha mtu msalaba ni kumtengeneza adui iwe halisi au bandia kisha kumpa ubaya wote na kuwafanya watu wamchukie.

Ndio maana mpaka hivi leo shetani anachukiwa licha ya kuwa hajawahi kuonekana na wala kuhusika moja Kwa moja Kwa shutuma apewazo.

Mwalimu Nyerere na Magufuli waliwachagua maadui zao ambao wakaona nchi za kibepari wazitwishe msalaba WA lawama na kelele ili wao wajinasue madhaifu Yao endapo yangetokea.

Marais Kama kina RObert Gabriel Mugabe, Gadafi, Sadamu Hussein, na wengineo wanaangukia katika kundi hili.

Yaani wao wanachagua adui Mwanzoni kabisa hata kabla hawajaingia madarakani, watasema nchi hii inamaadui hawa, nchi hii haisongi mbele Kwa sababu ya hawa mabeberu, nchi hii wapo vibaraka vya maadui zetu mabeberu, yaani wao maneno hayo yatasemwa hivyo hivyo kila wakati watakapopata nafasi.

Lengo ni wananchi waweke chuki na waungane naye. Wakishafanikiwa hivi, basi kazi yake imekuwa rahisi.

Hata Kama hakuna maji, umeme, dawa Hospitalini, au chochote kile wananchi watapeleka lawama zote Kwa Mabeberu (adui aliyetengenezwa)

Na yeyote atakayempinga Kiongozi wa namna hii, ataitwa kibaraka wa maadui. Hivyo wafuasi WA kiongozi na wananchi watamchukia.

Mbinu hii hutumika pia katika makanisa yasiku hizi. Adui atatengenezwa na ku-promotiwa kuwa ananguvu na ndiye chanzo cha maisha ya waumini kuwa magumu. Mchungaji akishafanikiwa katika hili huweza kufanya lolote alitakalo.

Kanuni hii wanaitumia hata Vyama vya upinzani kuwaaminisha watu kuwa ugumu wa maisha unasababishwa na chama tawala

2. MPE MCHAWI MTOTO AMBEBE
Mbinu hii pia ni moja ya mbinu ya kimedani ya kuzima kelele za malalamiko ya watu.

Yaani ni vile unaona unalaumiwa Sana unaamua kujivua Gamba, au kujiudhulu kisha kumuachia huyo anayekulaumu afanye yeye.

Yaani Kama Shetani angekuwa mjanja hizi lawama anazoshushiwa, angeomba ajivue au ajiue aondoke Duniani ili viumbe tuone watapata Nani wa kumlaumu.

Mbinu hii Kisiasa ni ngumu kufanya kazi Kwa sababu itabana maslahi ya mlaumiwa.
Yaani CCM ati imsusie CHADEMA Madaraka ili tuu Ione Kama itaweza kuyafanya na kuleta maendeleo wanayoyasema mdomoni upinzani, Jambo hili haliwezekaniki.

Lawama zinazoendelea Kwa Rais aliyepo ni matokeo ya mbinu ya Kwanza iliyotumiwa na Mtangulizi wake.

Na bahati mbaya ni kuwa, Rais aliyepo madarakani hajaamua kutumia mbinu yoyote kuzima kelele zinazoendelea ndani ya nchi.

Rais aliyepo madarakani bado hatujamsikia alitengeneza adui isipokuwa Adui mmoja ambaye alitajwa kuwa wanaanza kuleta chokochoko.

Mimi sisemi mengi, Acha nikale ugali bamia Hapa, niendelee kusikia makelele ya Watanzania.

Ni Yule Mtibeli,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kariakoo, Dar es salaam
 
Mwambie huyo aliyetuia sisi wananchi makaidi mkaidi mwenyewe itakuwaga vibaya 😥

Kutatua changamoto za wananchi kashindwa yeye ajabu lawama kwangu Mwananchi 😔
 
Tusipende uwongo, kwani maji yapo au hayapo dar?

Kule Kihonda Morogoro mjini tangu na tangu hakuna Maji na umeme ulikuwa unakatika katika.

Ni kweli yanayosemwa lakini hizi kelele zikiamuwa kuzimwa mbona rahisi Sana.

Hapo mbinu ya kumsingizia Adui kisha kumtumbua waziri WA nishati Bwana Makamba, alafu unaweka umeme siku Saba au kisha tabu inaanza upya.

Unatengeneza zengwe la uongo na kweli Unaunguza transformer au sehemu ya mitambo ya tanesco unafanya uchunguzi unakamata watu ambao wala sio wahalifu, bali ni michezo ya Siasa, unawapakazia uchafu wote na kusema wametumwa na maadui.

Hivyo hivyo unakuwa mtu wa propaganda mpaka unamaliza awamu zako unaitwa Mstaafu
 
Mbona tayari watu washaumia


Sio Sana Boss,

Huoni mtaani, Redioni, bungeni, mitandaoni, kwenye vyombo vya usafiri watu wanapiga kelele.

Unafikiri hizi kelele zinatokana nashida au nafasi ya waliyoachiwa wapige kelele.

Kuna wakati wananchi wanakuwa wamebanwa na bado wanaambiwa wasipige kelele.

Hata hivyo sikatai shida iliyopo, Ila natiwa moyo na Uhuru wa watu kujieleza.
 
Sio Sana Boss,

Huoni mtaani, Redioni, bungeni, mitandaoni, kwenye vyombo vya usafiri watu wanapiga kelele...
Uhuru haupo kihivyo, bado watu wanakamatwa kwa kukosoa.

Humu watu wanatumia I'd fake hivyo wakua safe na hata kipindi Cha mwendazake walikuwa safe.

Ila twitter na Facebook huko kila Leo wanakamatwa.

Pili hata magazeti bado yanafungiwa, rejea kilichotokea kwa raia mwema.

Umejivisha upofu.
 
Uhuru haupo kihivyo, bado watu wanakamatwa kwa kukosoa.
Humu watu wanatumia I'd fake hivyo wakua safe na hata kipindi Cha mwendazake walikuwa safe...
Uhuru upo Kwa Asilimia kubwa Mkuu, Facebook mbona kila siku naona watu wakitukana yaani matusi ya nguoni kabisa lakini hakuna hatua yoyote.

Nenda vijiweni, nenda kwenye vyombo vya usafiri.

Niliwahi leta Mada hapa Kueleza Jambo hili.

Sisemi kuna Uhuru 100% lakini walau upo tofauti na Mwanzoni.

Nakubali yapo madhaifu katika SERIKALI hii lakini ni serikali gani isiyokuwa na madhaifu? Hiyo hatuwezi ipata hapa Duniani.

Udhaifu haupaswi kuzidi hilo ndilo la Msingi.
 
Umenikumbuaha kubambikizia kesi watu pia


Unapewa zigo uhangaike nalo.

Ni mbinu ya kizamani inayofanya kazi hasa katika nchi zisizostaarabika.

Ukipewa Kesi lazima uachane na mambo mengine upambane na kesi Kwanza. Hivyo automatically utakuwa umewapa ushindi mwororro
 
Back
Top Bottom