Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 770
- 2,408
Kuna mambo yanafanyika ila athari zake huja huonekana baada ya muda mrefu sana..Ukifatilia asilimia kubwa watoto wanakuwa na migogoro na baba zao kuliko mama zao. Yaani ukisikia mtoto ana bifu na mzazi mmoja au amemtelekeza, basi asilimia 99% ya mzazi aliyetelekezwa anakuwa ni Baba. Moja kwa moja hisia za wengi huwa tunawaza kuwa mtoto amelishwa sumu na mama yake, au baba alikataa ujauzito na majukumu. Huenda huwa tupo sahihi kwa hypothesis zetu lakini sio mara zote huwa tunakuwa sahihi. Leo nimegundua sababu nyingine.
Nina rafiki yangu ambae tumekua wote na tulisoma wote hadi kidato cha nne. Baada ya hapo tukapotezana hadi tulipokutana wikendi iliyopita. Tukaanza kupiga story na kukumbushana matukio ya nyuma hasa hasa pale shuleni kwa wajeda...waliosoma hizi shule watanielewa.
Ilikuwa moment nzuri kukutana na rafiki yangu na tulifurahi sana kukumbuka past zetu..Tulivyoanza serious talk, nikagundua jamaa hana time kabisa na baba yake mzazi. Yeah, mshikaji yuko well off kimaisha na yupo kitengo kizuri sana. Sikutarajia kukuta jamaa anamchukia baba yake kwa jinsi ambavyo naijua familia yao kumbe kuna vitu vingi sana sivijui..Nikamdadisi jamaa kwa hiari yake kama hatojali anaweza share na mimi then niweze kumpa ushauri..Aliamua kufunguka na kuniambia sababu kuu ya kumchukia Baba yake.
Kipindi anakua, ameshuhudia mara kibao Baba yake akimpiga mama yao..Yaani Mzee alikuwa anampiga mama mbele ya watoto..Ile hali imemtesa sana jamaa kisaikolojia kiasi kwamba hadi leo amekua bado anamchukia Baba yake na hana time nae..Amejitahidi kusahau na kusamehe ila zile taswira za kilio cha mama huwa zinamrudia na kumuumiza sana nafsi..Amejiapiza hatakuja kumpiga mkewe mbele ya watoto maana impacts zake ni kubwa sana..Ameniahidi kusamehe, kusahau na kujitahidi kumpa heshima mzee wake.
Nakuja sasa kwenu wakuu. Hivi unaanzaje kumpiga mkeo mbele ya watoto wenu. Unadhani watoto wanajisikiaje? Aisee, chuki na visasi vyao huwa zinadumu muda mrefu sana. Hata kama ni hasira basi kuna namna mnaweza tafuta solution ila sio mbele ya watoto. Basi stress zikiziwazidi sana Hamieni Yanga.
Mimi nashukuru sijawahi kushuhudia haya matukio.
Nawasilisha.
Mzee Mpili na Rais watakuwepo Kigoma tarehe 25.