Niliahidi na natekeleza

Niliahidi na natekeleza

Ghaysh

Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
33
Reaction score
58
NILIAHIDI NATEKELEZA.

Tunaanzia mbali kidogo kujenga msingi....

Katikati ya umri wa kuhitaji malezi bora yanayohusisha wazazi wote wawili, baba na mama yake wanafarakana kiasi cha kufikia kutengana... Hali hii inamuweka kwenye wakati mgumu wa wapi aelekee... Mchungaji Philemon Ndelemu anabeba jukumu la kumchukua na kumfanya sehemu ya familia yake kwa kumpatia malezi anayostahili mtoto...

Miaka inasogea... umri unachochea kuni... ujana (Maji ya moto) unafikia fukuto la nyuzi joto (⁰C) 100... Maswali 39 ya ujana yanaanza kufanya ziara kwenye kichwa chake na kujikuta anaanza safari ya kutafuta majibu ili afikie jawabu...

Kijeba cha mtu kinaingia mtaani kujitafuta... kinakula nondo (kunyanyua vyuma) mitaa ya mchikichini kujenga na kuimarisha mwili.... anakula dili za ubaunsa kwenye milango ya nyumba za starehe... anajiongeza kucheza michezo ya kutumia nguvu za mwili kuonesha uwezo mkubwa alionao... anakuwa kama Power Mabula, ananyanyua na kuvuta vitu vizito kwa meno...

Anaona haitoshi anaamua kuwa Mandonga wa enzi hizo... Mwili na utundu unamruhusu kurusha apakati panchi za maana... anazoea ringi anakuwa mwanamasumbwi... anapigana ndondi mapambano kadhaa mpaka anatolewa meno... Anaona cha kufia ilingoni nini? Anaamua kubadili harakati za kutafuta hela kwani anazitaka tena nyingi...

Katika yale maswali 39 ya ujana anapata jibu la swali moja... "BORA KUISHI PAKA PARIS UFARANSA KULIKO MTU TANZANIA". Harakati za kuiacha Tanzania bila hati ya kusafiria zinaanza... Njia pekee ni zile za panya kwenye mipaka isiyo na ulinzi...

Inatafutwa kwanza SA (Afrika Kusini) [emoji1221] kupitia Malawi [emoji1156], nashindikana... Inajaribiwa njia ya Zambia [emoji1268] kupitia Tunduma, inashindikana...

Inawekwa kambi Chunya na shughuli za kuchimba madini zinashika hatamu... inatafutwa dhahabu kwa jasho, mzuka wa madini unakolea kambi inahamia Congo [emoji1078], mambo yanakuwa si mambo shughuli zinahamia Arusha kuyasaka madini adhimu zaidi Duniani, Yes... Tanzanite.

Wakati shughuli za migodi zinaendelea huku akijiona kama nataka anafulia zaidi, mwamba anajitafuta zaidi... anakumbuka anacho kipaji kingine kinachoweza kumuongezea kipato, naam kipaji cha Kuchora na kuchonga Vinyago... anaanza kujitendea haki kwa kuchonga Vinyago na kuvitega kwenye mahoteli makubwa ikiwemo Kilimanjaro Hotel [emoji545] Arusha...

Richard Hananja ndilo jina lake maarufu kwa sasa, Mchungaji fulani mtukutu sana wa maneno.... wakati huo anakijulikana kwa jina la Richie na sasa unaweza kumuita Richie Bilionea...

Hakuna maisha ya kijanja na utukutu wakati huo Richie hajapitia... Ofisi za vyombo vya dola ilikuwa sehemu ya maisha yake kwa kukamatwa mara kadhaa kwenye mampambano ya maisha... Moja ya matukio asiyo yasahau ni pamoja na wakati Nchi ya Tanzania inapitia msoto mkali yeye alikuwa miongoni mwa watu wanaokula bata kiana... Wakati huo kuvaa jeans [emoji158] tu unaweza kupewa mke bure. Alishawahi kukamatwa na kushitakiwa kwa kukutwa na Sabuni, Dawa ya mswaki na mafuta ya kupakaa...

Na kuonesha siyo bahati mbaya mahakamani alitinga akiwa amevalia kinachofuata sana Shati kali, Jeans ya maana na Raba mamtoni imesimama hiviii... Anasema hakimu mwenyewe alipomuona tu akamuelewa na akampa dhamana kibabe sana...

Pamoja na utukutu wake wote Richie hakuwa mtumiaji wa kilevi chochote na kwa mujibu wake ni kwamba akiwa kawaida tu anajiona basi limewaka sasa akiongeza kilevi itakuwaje? Hivyo busara kwake ikawa kutojiingiza kwenye matumizi ya vileo ili ndoto yake ya kuwa bilionea itimie kwa nidhamu... Hii ilimsaidia kuweza kumiliki viwanja maeneo ya Pugu Kajiungeni karibu na Kanisa. Alifanikiwa kujenga nyumba na kwa kuwa alililelewa katika misingi ya Kikristo basi akiwa Pugu kwake alikuwa anapenda kuhudhuria zaidi Kanisani. Na safari ya Uchungaji ikaanzia hapa kwa ushawishi mkubwa wa nje huku msukumo wa ndani nao ukiitikia....

Itaendelea...

Timothy Levy
1674846644772.jpg
 
Inaendelea....

Jamuhuri ndogo ya watu wa Pugu Kajiungeni inamtazama Richie kwa jicho la tatu kupitia mazungumzo yake mengi yanayoonesha kuwa ni vitamini na madini muhimu kwenye akili za watu... Unaanza kufanyika mpango wa kumshawishi aanze kuhudumia watu kiroho... lakini mara kadhaa Richie anakataa, akili na mawazo yake vipo Vinyago kumpatia pesa na kutimiza ndoto zake nyingi.

Msongo wa ushawishi wa kuhudumia watu kwa mafundisho unakuwa mkubwa zaidi na nafsi yake inaitikia... Richie anakubali na rasmi anaanza kutumika madhabahuni.... Muda unasogea anaanza kupata nafasi kwenye madhabahu zingine nje ya Pugu Kajiungeni.

2001 anapata nafasi kwenye madhabau ya moja ya Sharika Heavy za K.K.K.T... yes, Usharika wa Msasani. Richie anashusha nondo heavy za hadhi ya Usharika wenyewe... watu wanaguswa kwa namna ya tofauti na mioyo yao inasema MWAMBA HUYU HAPA... Madon wa Usharika wakati huo wakiongozwa na Charles Kimei, Joel Mabiba (mwenye mabasi ya JM) na wengineo wanamfuata Richie na kumwambia atafute chuo POPOTE DUNIANI wao watatoa mpunga akasome ili awe mchungaji Rasmi. Bila kupoteza muda tena vhuo kinatafutwa na Richie anaenda kusoma kwa mujibu wa taratibu za K.K.K.T.

Richie anahitimu masomo ya Thiolojia na anatambulika rasmi kama MCHUNGAJI RICHARD HANANJA.... Naam mume wa Rose [emoji257] (Daktari wa binadamu), mwanamke aliyepatwa kitukutu sana... Ndiyo, Kitukutu mno...

Akiwa kwenye umri unaokaribia Miongo minne (Miaka 40) bado akilini mwake anawaza utajiri tu... hata wazo la kuoa halipo kabisaaa... Siku moja afya yake inateteleka, mwili unapata msukosuko usio wa kawaida kiasi cha kulazimika kwenda Hospitali [emoji541]. Kufika hospitali anakutakana daktari ambaye baada ya kumuona tu msukosuko wa mwili unaondoka na kuhamia moyoni... Mwamba halazi damu tena anamtolea uvivu daktari na kumwambia "UGONJWA ULIONILETA HAPA UMEPONA, UGONJWA WANGU KWA SASA NI WEWE"... Daktari Rose anampa makavu na kumfukuza... Mwamba hakukata tamaa japo hatujui swaga gani ziliendelea ila tunachojua ni kuwa baada ya Miaka 4 Richie na Rose walisimama madhabahuni na kula kiapo cha ndoa takatifu.

Usharika wa kwanza kwa ajili ya mazoezi Mchungaji Hananja anapangiwa Kunduchi... baada ya kumaliza muda wa mazoezi anaingia rasmi kwenye ajira ya Uchungaji na kuanza kupangiwa sharika.

Kutokana na maisha aliyopitia, uzoefu wake wa muda mrefu kwenye maisha ya mtaa vilitosha kujua jamii inataka nini kutoka kwa watumishi wa Mungu (Viongozi wa Dini zote). Unaweza kusema kuwa aliisoma jamii katika kiwango ambacho kila anayemsikiliza leo atakubali kuwa sasa jamii inaanza kumsoma yeye. Mchungaji Hananja aliamua kukaa kwenye falsafa ya kuihudumia jamii kwa kuipa furaha badala ya vitisho.

Anaamini kuwa watu wanakuja makanisani kutafuta majibu ya maswali yao mbalimbali... hawatamani kuongezewa maswali na msongo wa mawazo... Ndiyo maana falsafa ya mahubiri ya Mchungaji Hananja ni ujumbe kutolewa kwa njia yenye vituko na utukutu wa maneno ambayo kila anayesikiliza lazima atacheka, atafurahi na kutamani kuendelea kusikiliza. Anaamini jamii yenye furaha na inayofundishwa na kuelekezwa kwa lugha rafiki inayowavuta iliyojaa upole ni rahisi kuachia uovu wao mezani na kufuata njia mpya kwa kuoneshwa na kuwezeshwa.

Wakati Sharika nyingi za K.K.K.T zikipambana kwa nguvu kubwa kujiimarisha kiuchumi kwa kuanzisha miradi mbalimbali yakiwemo majengo ya gharama kubwa kama vitega uchumi, yeye Mchungaji Hananja amekuwa kinyume na amekuwa akiongea kwa uwazi kabisa kuwa "KANISA LINATAKIWA KUWA NA VITEGA HUDUMA SIYO VITEGA UCHUMI". Na katika ufafanuzi wake amekuwa akisisitiza kuwa suala la Vitega Uchumi Kanisa linatakiwa kuwafundisha washirika wake hususani vijana na kuwawezesha wao kuwa na vitega uchumi ambao mwisho wa siku wao ndiyo wataleta sadaka ya kutosha kanisani itakayoliwezesha Kanisa kujenga VITEGA HUDUMA vinavyoweza kuhudumia jamii kama Hospitali (washirika watatibiwa kwa gharama ndogo kama siyo bure kabisa), Shule (watoto wa washirika watasoma kwa gharama ndogo sana), Vituo vya wahitaji, miundombinu ya maji nk

Muziki unaanzia hapa taratiibu....

Itaendelea baadaye....
1674895363304.jpg
 
Kutowahukumu, kuwapenda na kuwakumbatia watu ambao jamii inawatenga kwa matendo yao huo ndiyo msimamo wa Mchungaji Hananja. Anaamini watu wanajiingiza kwenye matendo maovu kutafuta majawabu ya maswali yao mbalimbali ya maisha, hivyo ili kuwaondoa huko ni lazima wapatiwe majawabu sahihi. Ndiyo maana pamoja na hadhi yake ya Uchungaji muda wake mwingi anautumia kuwa na wala ngada (unga), wavuta ndumu (bangi), madada poa na vijana wengine waliokata tamaa.

Akiwa anahudumia Usharika wa Kigogo alianzisha kwaya ya Watumiaji wa Madawa ya Kulevya (Unga na Bangi). Halikuwa jambo rahisi na ndiyo maana kila anayesimuliwa anastaajabu, lakini alichokifanya ni kuwaonesha upendo na kuwajali, kisha wakawa huru kusimulia madhira yao kila mmoja. Haikuchukua muda mateja na watoto wa mtaani kuaniz Kigogo, Mabibo, kuja mpaka Ubungo wakambatiza cheo cha Rais wao. Kila kona aliyokatiza walimshangilia na wakaandika jina lake kwenye kingo za madaraja na barabara.

Hakuna kituo cha polisi kanda ya Dar es Salaam kisichomfahamu Rev. Hananja... Yes, kwani mateja na watoto wa mtaani wengi wanaposhikiliwa vituo vya polisi wanatoa namba yake na huenda kuwafanyia utaratibu wa kisheria hususani kuwawekea dhamana. Kuna wakati hata Mateja wenyewe wanamstaajabu Rais wao huyu, kwani Licha ya kuwasaidia kuna wakati wanampiga matukio lakini anawapongeza na kuongea nao kirafiki badala ya kuwashitaki. Baadhi ya matukio kumbukwa ni haya...

1. Akiwa Mchungaji K.K.K.T Usharika wa Kigogo, licha ya ofisi yake kuwa ghorofani walipiga jeki nondo za dirisha wakaingia ndani na kuchukua wastani wa 600,000 kwenye droo... aliporejea na kugundua aliwaita wote waliokuwepo akawapongeza kwa akili waliyotumia kumuibia na akawapa 5,000 kila mmoja.

2. Miongoni mwa mateja aliokuwa wanazunguka walikuwa na vipaji na fani zao... hivyo wengine alikuwa anawawezesha kulingana na fani na vipaji. Waliokuwa na leseni za udereva na wanaonesha utulivu wa akili aliwapa gari aina ya DCM TOYOTA wafanye biashara... Siku moja basi liliwaka vichwani mwao wakaona kama Traffic anawazingua... kwa nini walimpelekee gari mazima... ikawa kesi, mwisho wa siku ikabidi gari ipaki kwanza...

Hapo hapo gari ilipopaki wana wakarudi wakaanza kuondoa kitu kimoja kimoja na kwenda kuuza...

3. Katika harakati zao za fukunyua pekenyua nyumbani kwa mchungaji waliotea kiasi cha Milioni 2 n kusepa nazo. Mchungaji Hananja aliposhtukia kama kawaida aliwakusanya na kuwaambia "HAYA KWENYE ILE MILIONI 2 LETENI CHENJI ILIYOBAKI..." walipokabidhi ndiyo kesi ikawa imeisha...

Juhudi zake, msimamo wake na zaidi MFUMO WAKE wa kuisaidia jamii hii ya waarhirika wa Madawa ya Kulevya, Madada poa na watoto wa mtaani vinapokewa na kuzungumzw kwa hisia tofauti baina ya wachungaji wenzake sambamba na viongozi wake. Ukosoaji wake wa kitukutu wake na maoni yake kwenye mikutano ya ndani navyo vinapokewa kwa hisia tofauti.

Itaendelea...
1674925668059.jpg
 
Nimechimbwa biti ila tumalizie kipole [emoji28][emoji28][emoji28]

Wakati wengine wakitazama kitendo cha kuwakumbatia mateja na watoto wa mtaani ni kukaribisha wezi na vibaka kanisani, lakini yeye alikuwa anamtazamo chanya wa kuwa kitendo hicho ndiyo njia sahihi ya kuwaidia kwani nao ni watu wa maana sana ndiyo maana shetani alipeleka vita kwao. Mara kadhaa anapokea maonyo juu ya tabia hiyo na maelekezo ya kufuata toka juu lakini Rev. Hananja anabaki kwenye msimamo wake wa kile anachokiamini.

Hata kila alipokuwa anahamishwa kituo cha kazi haikuwa rahisi kuhamisha mission yake juu ya Vijana hawa walioathirika na uraibu wa madawa ya kulevya. Kutokana msimamo huo changanya na utukutu wake wa naneno inatafsiriwa ni ukaidi. Kuna wakati watu waliaminishwa kuwa Rev. Hananja ni Drug Dealer (Muuza Madawa ya Kulevya) ndiyo maana hawezi kuacha kukumbatia kundi hilo. Jambo hilo liliwafanya viranja wake wazidishe maonyo kwake na ilipoonekana bado ana msimamo mkali wakamlima barua ya likizo ya mwaka mzima. Licha ya kutokuwa na hofu lakini alipita kwenye msoto fulani hivi amazing.

Baada ya Miaka kadhaa na kuona anazongwa sana juu ya maoni na misimamo yake, Rev. Hananja anaamu kwa hiyari yake kuandika barua ya kustaafu ili apate wasaa mzuri wa kusimamia maono na kutimiza ndoto yake ya kuwasaidia vijana hususani waliogeuziwa kisogo na jamii kwa kuamini hawafai. Inakuwa ni wakati mwingine K.K.K.T inapoteza mapema kwenye mfumo moja ya wachungaji wenye ushawishi mkubwa kwa vijana na mwenye mafundisho au madini muhimu.

Hata hivyo kustaafu kwake kunainufaisha jamii kwa mapana yake kwani ndipo anaanza kuonekana zaidi kwenye mitandao ya kijamii na wale ambao hawapati fursa ya kwenda makanisani wanaanza kufaidi madini yake kupitia mahojiano mbalimbali ambayo anayafanya mara kwa mara.

Lipo deni moja muhimu ambalo jamii ya vijana tunamdai Rev. Hananja... Yes, ni somo muhimu la maswali 39 ambayo vijana tunajiuliza. Tunahitaji madini haya.
1675011775240.jpg
 
Back
Top Bottom