Nile maharage kwani mi muha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nile maharage kwani mi muha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mfianchi, May 9, 2012.

 1. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  ''Nile maharage kwani mi Muha''hii ni kauli ambayo ilipendwa sana kutumiwa miaka ya nyuma na wakazi wa Kunduchi wakati huo njia ya kwenda Bagamoyo ilipita Kawe hadi nyumba za polisi Kunduchi,kauli hiyo ilitokana na wakazi wengi wa Kunduchi wakati huo wakiwa Wazaramo kupendelea kula samaki ambao walikuwepo kwa wingi,hao Waha wanaosemwa walikuwa wanfanya kazi kwenye shamba la mkonge la giriki liliokuwepo kuanzia Tangibovu hadi pale Mbuyuni , vibarua wengi wa hilo shamba walikuwa watu wa kuja kutoka Kigoma ambao ndio walikuwa wengi,na pia ndio walikuwa vibarua kwenye machimbo ya kokoto Kunduchi menu yao kubwa ilikuwa harage na dona.Kwa vijana wa CCM ya Jakaya naona mtashangaa kuwa kuanzia Tangibovu hadi Mbuyuni palikuwa shamba la mkonge,hivi sasa familia ya huyo giriki imebakiwa na kipande cha ardhi kuanzia kona ya Africana hadi Mbuyuni.Hawa Waha ambao walikuwa wanataniwa enzi hizo kwa kula maharage sasa ndio matajiri wa vitongoji vya Tengeta na Kunduchi na wale ambao walikuwa wanajifanya hawali maharage sasa maharage kwao ndio menu kubwa na ndio malofa,ama kweli dunia imebadilika .
   
 2. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Ye braza wee, naona hao jamaa hakuwahi kula maharage ya luwese ndio maana walisema hivyo. Ugali kwa maharage ya luwese, hapana bwana, nyama nyuma!
   
 3. kimpe

  kimpe JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 745
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 80
  Tengeta ndo nini
   
 4. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ulakoze mutama.!
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  wa zamani wewe?????????? wengine hat dar hatuaijua enzi hizo.
   
 6. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,725
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Thx alot kwa huu uzi, umenifanya nijue kwa nini tegeta kuna waha wengi sana, kuanzia pale skaska mpaka kibaoni ni wamejaa waha tu na wengi wao wanamiliki maduka
   
Loading...