Niko sahihi au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niko sahihi au?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by salma juma, Apr 13, 2011.

 1. s

  salma juma Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  H abari wapendwa,si mgeni sana humu ila huwa nasoma zaidi kuliko kuchangia mada mbalimbali za jf na naridhika na michango ya wachangiaji karibia wote wa forum hii.Leo nna tatizo langu si kubwa wala dogo kivile,mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 14 sasa na nna ndoa ya kanisani usitishike na jina tafadhali,tuliishi kwa maelewano sana na mme wangu japo kulikuwa na vimatatizo vya hapa na pale ila tulivimaliza na maisha yaliendelea kama kawaida,tatizo lilianza pale ambapo mwenzangu aliposhindwa kuelewa familia ni nini na inahitaji nini,mume wangu hana muda na familia wala kiajana wetu,anachojua nikutoa pesa tu,nimejitahidi kuongea nae sana juu ya hili kwa muda mrefu sana mwisho nami nimechoka nikajikuta natengeneza chuki za ajabu dhidi yake mpaka heshima yangu kwake imekwisha kabisa,hata nikijaribu kumuheshimu najikuta siwezi sio kwa kuwa najifanyisha imetokea tu mpaka chumba nimehama nadhani huu ni mwaka wa nne sasa,tunaishi kwa ajioli ya mtoto tu si yeye wala mimi aliewahi kumueleza mtu yoyote juu ya hili watu wakituona kwa nje wanaona ni mke na mume kumbe ndani hamna kitu,sina wivu nae hata kidogo,tunasalimia kama watu tusojuana na hata kama tuko pamoja kama kuna jambo tunatumia message kuelezana ila kuongea naona kichefuchefu maana akijaribu kuongea nnaona kama ananipotezea muda sielewi nini kimenikuta naomba msaada wenu jamani....wale waropokaji naona si mahala pake hapa huwezi changia soma kimyakimya.
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  pole ndg yng! Huyo ni shetani kaingia ndani ya nyumba na nyie mkampa nafasi awatawale! Kwa nini mmeacha tatizo mpaka miaka 4?? Je bado unampenda mumeo kwa dhati ya moyo wako? Mmeshindwa kukaa chini na kuelezana kwa upendo? Sio vizuri, mbona tatizo sio kubwa hivyo?
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jaribu kufanya mawasiliano na ndugu wa pande mbili yaani upande wa kwako wewe na upande wa mumeo ili muweze kujadili ili swala vile vile kama ulifunga ndoa kanisani ni vizuri kama kuna uwezekano hilo swala pia likaenda kuzungumziwa huko kanisani kuona tatizo liko wapi, kama ulivyosema huu ni mwaka wa nne hamkai chumba kimoja ila mko ndani ya ndoa naweza kusema both wewe na mumeo mna matatizo tatioz lako wewe ni KUMDHARUA MUMEO TENA HADI KUONA KICHEFUCHEFU anapoongea hiyo dharau tayari imekufanya uone kuwa mumeo si lolote wala si chochote akiwa anaongea mbele yako.

  Pia wewe na mumeo bado mna nafasi ya kuzungumzia hili tatizo lilipo

  Nitarudi kutoa ushauri mwingine
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Duh Da salma pole sana................. hebu kaa ujitafakari ni nini HASA kinachokukera kwa mumeo?? Ni hilo la kutokuijali familia tu au kuna JINGINE??
   
 5. s

  salma juma Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahsante sana mpendwa,kiukweli nimejaribu kumuweka chini mara nyingi zaidi ya nnavyoweza kueleza lakini hakuna kinachofanyika baada ya hapo,tatizo ni kubwa sana mpendwa sijaeleza mambno mengi sana hapa.
   
 6. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Pole sana dada kwa yaliyokusibu cha kufanya hapa kwa kuwa matatizo yameshindikana ndani ya nyumba inabidi utafute wazee wa familia yako na yake muyaongee naamini utapata ufumbuzi, Ila hapo kwenye Red yale mambo yetu sijui ndo inakuwaje !!!!!
   
 7. s

  salma juma Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru mpendwa sina tatizo lolote zaidi ya hili la kutoijali familia kinachoniuma zaidi ni yeye kushindwa kuwa karibu na mtoto wetuambae anazidi kukua bila ukaribu baina yake na mzazi wake wa kiume,anahitaji muda mwingi sana babake kinyume chake amekuwa ni mtoto wa mama zaidi,hii ndio sababu inayonifanya nimchukie kadri siku zinavyokwenda mbele.
   
 8. s

  salma juma Member

  #8
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kiukweli hapo kwenye Red nafikiri tushapasahau kabisa sina kumbukumbu yoyote,na suala la kuwashirikisha wazazi wa pande mbili inakuwa ngumu kidogo maana wazazi wangu wote wawili walishafariki,nna ndugu wa baba mmoja ila sipendi waelewe maisha yangu kiundani zaidi na kwa upande wake nadhani ni jukumu lake kuwaeleza wazazi wake kama anakaa kimya sina namna.
   
 9. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  daaah, pole again! Mlishawahi kushirikisha ndugu wa pande zote? Umemchunguza labda ana nyumba ndogo mahal, coz daaah miaka mi4 ni mingi ndgu yangu. Mwulize anataka mwisho wenu uweje? Manake bdo mpo kwnye ndoa.
   
 10. s

  salma juma Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kichefuchefu kimekuja baada ya kuona hakuna nntakachoweza kuokoa kutokana na tabia yake,sikuwa namdharau kabisa ila kama miaka 2 na nusu ndo hizi dharau zimeanza
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  ..............Labda ungeelezea kidogo kwa urefu huko kutoijali familia ni kwa namna gani? Anatumia muda mwingi na friends kuliko familia yake? Yuko buzy na mambo gani haswa au ni mmoja wa maprofesa ambao ni yeye na matheory na matheory na yeye?? Sijakupata vizuri
   
 12. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mnaishi kwa ajili ya mtoto.
  Ukiongea nae unasikia kichefuchefu
  Mmetengana miaka minne
  mnafanya usanii nje muonekane bado mpo kwenye ndoa!


  Ngoja kwanza nikajipange kwanza..........
   
 13. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Salma, bado unampenda mumeo? Na ungependa muendelee kuishi pa1, maisha ya mke na mume? Hebu jitoe muhanga kwenye hili, nenda wafwate hao wakwe zako, waeleze hali halisi bila kuwaficha chochote then uone watakujib nini. Hayo maisha mnayoishi sio mazuri kabisa. Jishushe mpe nafasi mumeo kama mwanaume.
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa kuangalia maelezo yako kwa haraka haraka nisingependa ku-conclude kitu ambacho sina uhakika nacho ila ningependa kukuuliza maswali yafuatayo

  1. Je unahisi mumeo anatoka nje ya ndoa yenu?
  2. Mwaka wa nne sasa hamkai chumba kimoja kila mtu yuko kivyake inamaana hata kwenye kukutana kwenye tendo la ndoa suala
  hilo halipo? kama ndivyo basi swali la kwanza litakuwa limepata jibu
  3. Mumeo anafanya kazi gani kiasi kwamba asiwe na muda na familia?
  4. Bado unampenda mumeo?
   
 15. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja. Hebu 2fafanulie kdogo kwenye huo ubsy wa mumeo!
   
 16. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Salma unajua nini??! mawasiliano ni kitu muhimu kabisa katika dunia ya mapenzi/ndoa, hata kama mtu anakukera vipi pata moyo wa kuongea nae..Kwa jinsi mnavyoishi haipendezi kabisa, sasa unaelewa mtoto anapata picha gani? ukikaa na mambo moyoni yanazidi kujaa na kukukera mpaka kuyapunguza inakuwa too late.
  Halafu unasema haijali familia yani kutumia muda na nyie au?anafanya kazi gani?pole lakini ukiongea nae huwezi jua labda yote yanaweza kubadilika..
   
 17. s

  salma juma Member

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru mpendwa,yeye ni mtu amabye sijui hata nimuweke kundi gani,anajifanya yuko busy sana lakini nashawishika ni moja ya sababu zake za kukwepa majukumu yake kama mzazi,tangu kijana wetu ana miaka 4 hajawahi ona hata siku moja familia imekaa mezani ikapata mlo wa pamoja,kutoka kwenda sehemu yoyote ile ila yuko radhi atoe kiasi chichiote cha pesa nisafiri kokote nnakotaka na mwanangu pale tunapohitaji,mtoto anahitaji ukaribu fulani na mzazi wake yeye hana muda huo,kila siku yuko kazini haijalishi jumamosi wa jumapili,simjui rafiki yake yoyotye maana si mtu wa marafiki hata kidogo ana jamaa tu anaofahamiana nao kiubinaadam lakini kusema huyu rafiki yake hana hata mmoja...ntaendelea kuelezea kadri mnavyoniuliza maana ni mengi mpaka nashindwa nianze wapi niishie wapi
   
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Tangu miaka 4?!! buzy kikazi tu??!! mh angekuwa ni mtu wa marafiki saaana ningesema marafiki but mh!! huko kazini kwao hawachukuagi likizo? miaka 14 hajawahiona umuhimu wa kukaa na familia? au ana familia nyingine anayospend nayo muda zaidi??? Si kawaida aisee.........................................
   
 19. s

  salma juma Member

  #19
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kiukweli siwezi kumsemea kama anatoka ama hatoki,ila kwa miaka minne yote yanawezekana ,kumpenda sidhani maana sina hisia zozote juu yake kiukweli..na ndo maana nikaja omba ushauri wenu hapa nakosea ama niko sahihi kwa upande huu..
   
 20. s

  salma juma Member

  #20
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo ndipo nilipochoka kiwmili mpaka kiakili na mwisho wa siku kumhama na kumtoa kabisa katika akili yangu,akichukua likizo anakuja nyumbani kupumzika mwezi mzima na hata siku anayorudi huwa sijui nakuta tu kuwa amefika,na ni wa kwanza kutembelea familia yangu mpaka kijijini ndani kabisa anafika kwa mababu zangu na kama kuna tatizo anatatua na wala akurudi hanielezi chochote nafanya kusikia tu kwa ndugu zangu...babu yangu yuko hai na ananguvu na akili timamu kabisa ila hajawahi hata mueleza chochjote kinachoendelea kwenye nyumba yetu hapa ndipo nnaposhindwa kumuelewa kiumbe huyu
   
Loading...