Niko njia panda,naombeni ushauri

Niko njia panda,naombeni ushauri

Kuna haja ya kuuliza kabla ya yeye ushawahi kuwa na mpenzi mwingine?
Duuuu haya mapenzi kweli shida na matapeli wamekuwa wengi.
 
Kuna mwamba anakuja kuishi nae kwa miezi 5...ili usimsumbue au kumwaribia ndo imekua hivyo.. Shtuka........
 
Kazi ipo hapo..cha kufanya ujimuvuzishe tu kwa mwingine. Mwenzio analiwa..ameshachange mind ya kuolewa na wewe.
 
Wapendwa Wana JF,

Nimekuwa katika uhusiano na dada mmoja mzuri sana, na kulingana na nilivyo mtathimini anaonekana ni wife material, I admit to say that from my heart. Tatizo lililopo ni kuwa tunaishi mikoa mbali mbali. Mimi naishi mkoani kagera, na yeye anaishi mkoa wa Katavi.

Toka tufahamiane tumekuwa na mawasiliano active muda wote, though mikwaruzo ya mara chache chache sana hutokea na immediately we resolve it and become one thing again.

USHAURI:
Kwa kuwa tumeadhimia kuweka mambo yetu hadharani kwa wanafamilia mwishoni mwaka huu (december, 2016), huyu mpenzi wangu ameniomba na kushauri kuwa ni vema tusiwe na mawasiliano kwa muda wa miezi mitano toka sasa hadi mwezi september, 2016 ili ibaki miezi mitatu...then ndio tuanze mawasiliano motomoto kuelekea december kukamiliasha mambo muhimu ya kutuunganisha rasmi.

Kasisitiza kuwa ili kufanikisha hilo kila mmoja am-block mwenzake kwenye simu na kusiwe na mawasiliano hadi tarehe 1 semptember, 2016. Mimi nilishangazwa na kauli ile, kwa haraka ili kupima upepo nione itakuaje. Nilipomkubalia tu, basi akani-block kweli hadi muda huu naandika huu uzi.

1. Wadada kweli mnaweza fanya hivyo kwa mtu unayempenda kwa dhati - kutowasiliana nae for 5 months?
2. Inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia huko katavi na mimi nisijue kinachoendelea?

Nipo njia panda...nishaurini....nielekeee upande wa kulia kumfuata atakavyo yeye au mimi niamue kufuata njia nyingine upande wa kushoto?

NB: Naombeni ushauri sahihi hasa kwa watalaam wa mambo ya mahusiano yenye muelekeo wa ndoa.

KARIBUNI.

Huyo dada atakuwa Mhaya, tena ana mapepo.

Tumia namba nyingine kumtafuta, au tumia marafiki zake kuwasiliana nay, ili upate kujua kama ana ugomvi au ana lengo gani na wewe.

Plan C:
Weka namba yake hapa tukusaidie kumwaga ugali....
 
Mmh! Huyo ana lake jambo

Unaempenda humchoki,muda wote unatamani muwasiliane,mchat vya muhimu na utani wa hapa na pale mradi burudani tu
 
Ebwana daah! So sorry mkuu, mwenyew yashankut kam hayo but hayo yamezidi kina, GF wangu mm alitaka tupotezeane nkamlilia sana mwisho wa siku nkaona what ever happens ngoj nijikaze nkamwambia pow akawa hapokei for almost one week nkaaona pow, mara akantafuta mwenyewe till now npo nae sawa.
But for you daah fanya kuangalia the other side mkuu japo maumivu nayaelew yalvo but pole mwana.
 
huyo mchuchu wako anafanya kazi gani huko katavi?
 
Hata mimi nashangaa sana ''yaani kutamka tu ameshakublock''
 
Kwa mwanaume kamili anaejitambua huwezi omba ushauri ktk hili.
 
Polee mkuu, simama hapo hapo njia panda atapita na mkaka mmoja utamuona
 
Huna chako hapo kaka kuna mtu anakusaidia majukum na huyu anapima upepo nacho kiona hapo ww sio chaguo la kwanza ww ni chaguo la pili angalia kua makin atakupotezea muda huyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom