Niko njia panda,naombeni ushauri

Niko njia panda,naombeni ushauri

Binafsi mapenzi ya kuwa mbali hivyo I cant. Raha ya kupendana muwe karibu karibu, yaani ukiwashwa tuu fasta unakimbia
 
Mimi sio mwanaume wa Dar; mimi nipo huku mkoani Kagera.
wanasemaga ukiona manyoya ujue ameliwa ........we achana nae songa mbele ila usisahau kufanya kazi na kujibuludisha ili umsahau inaonekana umefall in love .......mie yaliwah nitokea eeeeeh nikikumbuka duuuuh lakin maisha yapo yanakwenda love ilipotea
 
kunatawi moja la klabu ya yanga linaitwa ukiona manyoya ujue kaliwa
 
Kuna jamaa alileta uzi unaomuhusu rafiki yake wa ki love story, nikamuuliza rafiki yako anasoma akasema ndio! na wewe nakuuliza huyo msichana anasoma?
Mkuu hapo hapo kwenye hao wanaosoma hebu funguka kidogo ktk experiance ulyonayo.
 
Dah!,hii tabia ya kupenda kushauriwa kila kitu ...mwanaume!!!, sijui mnaitoa wapi..…..........?,au kizazi?
 
Sijawahi kuona mwanaume anapewa masharti...

Wewe ndio wa kwanza...ka bwege fulani
 
Nyie vijana wa dot. Com balaa sasa anakwambia ivo nawe unasema yes dia, kweli dunia ina mambo huo ni mwanzo wa kushikwa masikio ukijamweka ndani atakwambia dear tusigegedane mwaka mmoja utasema yes dia afu utakuja kuomba ushauri apa
 
Endelea na maisha yako mdogo mdogo,
AMEPATA MWINGINE
 
Wapendwa Wana JF,

Nimekuwa katika uhusiano na dada mmoja mzuri sana, na kulingana na nilivyo mtathimini anaonekana ni wife material, I admit to say that from my heart. Tatizo lililopo ni kuwa tunaishi mikoa mbali mbali. Mimi naishi mkoani kagera, na yeye anaishi mkoa wa Katavi.

Toka tufahamiane tumekuwa na mawasiliano active muda wote, though mikwaruzo ya mara chache chache sana hutokea na immediately we resolve it and become one thing again.

USHAURI:
Kwa kuwa tumeadhimia kuweka mambo yetu hadharani kwa wanafamilia mwishoni mwaka huu (december, 2016), huyu mpenzi wangu ameniomba na kushauri kuwa ni vema tusiwe na mawasiliano kwa muda wa miezi mitano toka sasa hadi mwezi september, 2016 ili ibaki miezi mitatu...then ndio tuanze mawasiliano motomoto kuelekea december kukamiliasha mambo muhimu ya kutuunganisha rasmi.

Kasisitiza kuwa ili kufanikisha hilo kila mmoja am-block mwenzake kwenye simu na kusiwe na mawasiliano hadi tarehe 1 semptember, 2016. Mimi nilishangazwa na kauli ile, kwa haraka ili kupima upepo nione itakuaje. Nilipomkubalia tu, basi akani-block kweli hadi muda huu naandika huu uzi.

1. Wadada kweli mnaweza fanya hivyo kwa mtu unayempenda kwa dhati - kutowasiliana nae for 5 months?
2. Inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia huko katavi na mimi nisijue kinachoendelea?

Nipo njia panda...nishaurini....nielekeee upande wa kulia kumfuata atakavyo yeye au mimi niamue kufuata njia nyingine upande wa kushoto?

NB: Naombeni ushauri sahihi hasa kwa watalaam wa mambo ya mahusiano yenye muelekeo wa ndoa.

KARIBUNI.


Watoto wa mjini wanasema "Chapa Lapa" aka "Sepa" aka Kimbia.
 
Huna haja ya kujiweka njia panda, endelea kubaki Kagera.
Ni ngumu ILA naungana na wengine " there is a big shadow of doubt.."
 
Katavi-Kagera bila mawasiliano kwa miezi 5? Hakika msubiri tu kiongozi maana utakuta tayari alishaolewa muda mrefu. Na mwenyewe umesema ni "wife material"...
 
Kuwa mvumilivu, mbona zamani hakukuwa na mawasiliano ya simu lakini still watu walivumiliana? msikilizie
 
Hapa ni kama vile una mtihani wa kuhitimu masomo yako kisha unashauriwa kuwa usishike kitabu mpaka week ya mtihani ikifika halafu na wewe ukaamini utafaulu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom