Hali zenu wana JF...
Naomba ushauri wenu tafadhali maana niko njia panda.
kuna huyu m-baba, sitamuita kaka maana ni mtu mzima. tulifahamiana miaka kama 7 iliyopita. Alinipenda sana, mpaka sasa naamini ananipenda kupita maelezo. Mimi binafsi hajawahi kuniingia moyoni. anajua simdondokei, lakini anaamini kuna siku nitabadili mawazo. Wakati huo naanza kufahamiana nae alikua na mke. ana bidii kwa kweli ya kuniweka sawa, lakini mimi wapi. kuna wakati anachoka na kukata mawasiliano, lakini vile mimi sina time nae, wala hainikeri. Mwaka unakatika anarudi tena, lakini mambo ni yale yale kwa upande wangu. Ana matatizo yake huyo kaka, sitapenda kuyaeleza ila kwa kifupi we are not compatible, nionavyo mimi we cant be togather.
Miezi kama mitatu iliyopita, karudi tena kwa nguvu mpya, na this time ni divorcee. nimeamua kua mpole fulani, japo still roho inakataa. ana kazi nzuri, ana watoto wake anaishi nao, anataka ndoa, anadai nafsi yake imeelekezwa kwangu, pamoja na kuwa namuudhi siku zote, lakini bado he thinks we can have a good life togather. Huyu nitamuita John.
Kuna mwingine, huyu namuita Peter. Peter yeye, tuliwahi kua na mahusiano miaka kama mitano iliyopita ambayo yalidumu kama miaka miwili na kiasi fulani. Tulipendana sana mpaka tulipewa majina mji huu. tukatofautiana kidogo sana na kitu cha kijinga mno, sababu ya kila mmoja kua na hasira na mwenzie, tuka break-up. niliumia na yeye naamini aliumia sana. Peter hana ajira inayoeleweka zaidi ya mission town niseme japo ana elimu. ni wale watu ambao they think hawawezi kuajiriwa.
From nowhere Peter nae anataka kurudisha majeshi, kwa nguvu zote. kibaya ni kwamba kaja wakati mmoja na John.
Peter nafsi yangu inampenda sana, na yeye naamini ananipenda, tuna match kwenye kila kitu, very compatible, interests na hobby zetu ni moja. maongezi yanalandana, namzidi kidogo umri, lakini kwangu sio issue.
Niko njia panda. John ananipenda sana na anataka ndoa, maisha yake mazuri, nikiolewa nae najua sitabahitisha kuishi, nina uhakika wa maisha bora, pesa yangu najua nitaotoa kwa kusaidia tu, lakini si lazima. Tatizo bado hayuko moyoni mwangu.
Peter, tunapendana sana, naamini hivyo, lakini hana ajira, maisha ni mishe mishe mjini mradi kunakwenda. aliwahi kuoa nae akaachana na mkewe. kwa sasa nae ni single. nikiwa nae ina maana maisha ni ku share au mimi niwajibike zaidi pale mission zinapokataa.
Mimi mwenyewe nina maisha yangu, I cant complain, najiweza, hata nisipopata msaada wa mtu maisha yangu yanakwenda vizuri bila kukuna kichwa.
Wana JF, ushauri na nasaha zenu ni muhimu. Kina dada, kama ni wewe utaenda kwa Peter au John...
Inakuwaje mtu ambaye humpi nafasi katika nafsi yako akuweke njia panda?(John) Na issue za relationship kwangu binafsi kushauri ni kazi maana inakuwa kama vile kumchagulia mtu partner wa kuishi nae for the rest of his/her life. Kama unampenda Peter na ni mwenye kipato duni endelea nae na huyu John kinachokuweka njia panda ni pesa yake and not true love kitu ambacho huenda kikaathiri maisha yako vile vile. For JUST FOLLOW YOUR HEART only thing I can say.
Yaani mpaka sasa John anaongoza kwa kura nyingi.
Afu tayari ana kura turufu ya kwako na ya kwangu. Imebaki moja tu ya Babu mwenzangu Dark City.
Vote For John... (Nimekumbuka mshiko wangu Superman kanirusha, au adhawaiz fellow tablet klorokwini atakuwa katuuzia kibudu kwenye kiroba.... Do something Kongosho asali ya ODM)
kweli konnienarudi badae kidogo
Nilisema ntarudi sababu nilikuwa nakumbuka hii story hapo chini, nadhani huyu ni Peter.
Si kila mwanamme anaweza ndoa, Peter ulishampa nafasi na akashindwa kuitumia, je unadhani sasa kaenda okota wapi akili ya kuwa mume?
Endelea na John, mapenzi yatajiset huko huko mkiwa ndani, wakati mwingine tunajifunza kupenda.
narudi badae kidogo
Nilisema ntarudi sababu nilikuwa nakumbuka hii story hapo chini, nadhani huyu ni Peter.
Si kila mwanamme anaweza ndoa, Peter ulishampa nafasi na akashindwa kuitumia, je unadhani sasa kaenda okota wapi akili ya kuwa mume?
Endelea na John, mapenzi yatajiset huko huko mkiwa ndani, wakati mwingine tunajifunza kupenda.
kwani wanaume ni hao tu?
ila kama ulimwengu wako wa wanaume ni hao...mimi naprefer john ..
maelezo zaidi nitakupm maana hapa wanga wengiiiiiiiiii
We Da Asia, sikiliza ushauri wangu mie kikongwe babu ODM.
Ni hivi... :
Maisha ni mafupi sana.... ukipata nafasi ya kuinjoi usiipoteze.
Peter mlishawahi kuwa pamoja na ikashindikana mkaachana. Nani alikudanganya jasiri anaacha asili? Hakuna kitu kibaya kama kuumizwa mapenzini mara mbili na mtu mmoja. Usisahau alishakuwa na mwanamke mwingine na ujue kuwa mahawara hawaachani. Pia huyu Peter huyu kama we umemshindwa, na huyu mwingine pia kamshindwa... huyu ni kunguru huyu, hafugiki huyu. (SAmahani najua unampenda lakini ndo hivyo, kunguru ni kunguru tu)
John anakupenda sana... hakuna kitu kizuri mapenzini kama kupendwa. Ana mahela, ni mtu mzima..... (Kama necha itachukua mkondo wake atakufa kabla yako, unaukwaa utajiri lol) Jifunze kumpenda bana ule maisha. maisha mafupi haya.
Kama hujanielewa namaanisha hivi... Go For John Bana.:clap2::clap2:
Hivi leo jumangapi vile? Damn!
Kumbe mimi mshamba sana...........sikujua mapenzi yana tafsiri tofauti kabisa nyakati hizi....Nimejifunza