Niko Njia Panda... Msaada Please | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niko Njia Panda... Msaada Please

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Da Asia, Jun 7, 2012.

 1. Da Asia

  Da Asia JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 725
  Likes Received: 369
  Trophy Points: 80
  Hali zenu wana JF...
  Naomba ushauri wenu tafadhali maana niko njia panda.

  kuna huyu m-baba, sitamuita kaka maana ni mtu mzima. tulifahamiana miaka kama 7 iliyopita. Alinipenda sana, mpaka sasa naamini ananipenda kupita maelezo. Mimi binafsi hajawahi kuniingia moyoni. anajua simdondokei, lakini anaamini kuna siku nitabadili mawazo. Wakati huo naanza kufahamiana nae alikua na mke. ana bidii kwa kweli ya kuniweka sawa, lakini mimi wapi. kuna wakati anachoka na kukata mawasiliano, lakini vile mimi sina time nae, wala hainikeri. Mwaka unakatika anarudi tena, lakini mambo ni yale yale kwa upande wangu. Ana matatizo yake huyo kaka, sitapenda kuyaeleza ila kwa kifupi we are not compatible, nionavyo mimi we cant be togather.
  Miezi kama mitatu iliyopita, karudi tena kwa nguvu mpya, na this time ni divorcee. nimeamua kua mpole fulani, japo still roho inakataa. ana kazi nzuri, ana watoto wake anaishi nao, anataka ndoa, anadai nafsi yake imeelekezwa kwangu, pamoja na kuwa namuudhi siku zote, lakini bado he thinks we can have a good life togather. Huyu nitamuita John.

  Kuna mwingine, huyu namuita Peter. Peter yeye, tuliwahi kua na mahusiano miaka kama mitano iliyopita ambayo yalidumu kama miaka miwili na kiasi fulani. Tulipendana sana mpaka tulipewa majina mji huu. tukatofautiana kidogo sana na kitu cha kijinga mno, sababu ya kila mmoja kua na hasira na mwenzie, tuka break-up. niliumia na yeye naamini aliumia sana. Peter hana ajira inayoeleweka zaidi ya mission town niseme japo ana elimu. ni wale watu ambao they think hawawezi kuajiriwa.
  From nowhere Peter nae anataka kurudisha majeshi, kwa nguvu zote. kibaya ni kwamba kaja wakati mmoja na John.
  Peter nafsi yangu inampenda sana, na yeye naamini ananipenda, tuna match kwenye kila kitu, very compatible, interests na hobby zetu ni moja. maongezi yanalandana, namzidi kidogo umri, lakini kwangu sio issue.

  Niko njia panda. John ananipenda sana na anataka ndoa, maisha yake mazuri, nikiolewa nae najua sitabahitisha kuishi, nina uhakika wa maisha bora, pesa yangu najua nitaotoa kwa kusaidia tu, lakini si lazima. Tatizo bado hayuko moyoni mwangu.

  Peter, tunapendana sana, naamini hivyo, lakini hana ajira, maisha ni mishe mishe mjini mradi kunakwenda. aliwahi kuoa nae akaachana na mkewe. kwa sasa nae ni single. nikiwa nae ina maana maisha ni ku share au mimi niwajibike zaidi pale mission zinapokataa.

  Mimi mwenyewe nina maisha yangu, I cant complain, najiweza, hata nisipopata msaada wa mtu maisha yangu yanakwenda vizuri bila kukuna kichwa.

  Wana JF, ushauri na nasaha zenu ni muhimu. Kina dada, kama ni wewe utaenda kwa Peter au John...
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  narudi badae kidogo

  Nilisema ntarudi sababu nilikuwa nakumbuka hii story hapo chini, nadhani huyu ni Peter.

  Si kila mwanamme anaweza ndoa, Peter ulishampa nafasi na akashindwa kuitumia, je unadhani sasa kaenda okota wapi akili ya kuwa mume?

  Endelea na John, mapenzi yatajiset huko huko mkiwa ndani, wakati mwingine tunajifunza kupenda.


   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Commonsense is knowing the rules of the game, Wisdom is knowing ur opponent(s) before engaging in the game.
   
 4. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jaribu kumpa nafasi JOHN uone moyo wako utakuwa vipi halafu hayo matatizo ya JOHN unafikiri yanaweza kukuletea matatizo?jaribu kufuatilia sababu za wenyewe kuachana na wake zake kwanza.
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,958
  Likes Received: 23,634
  Trophy Points: 280
  Kwa navyokujua, mida hii ungeshakuwa kwenye mlango wa bangaluu la John ukiambatana na dada zako, mabinamu na mama yako mkubwa. Ofkozi virago vyako vyote ungekuwa ushahamishia kwa mama yako.:confused2:
   
 6. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Love is not finding someone to live with; it's finding someone you can't live without...Da Asia hebu tulizana, kama huyo m-baba ameweza kumpenda mkewe na kumuoa na kuzaa naye watoto kabla yako atashindwa vipi kufanya na kwako pia kipindi hicho ikiwa umechoka na yeye akiwa ameona vibinti vibichi vingine??? mpende akupendaye, jaribu kumsaidia huyo Peter awe vile utakavyo wewe...muwezeshe na kumuelimisha ili ajiajiri, awe na maisha mazuri muishi pamoja. Kwa nijuavyo mimi...mwanamke au mwanaume mwenye mpenzi zaidi ya mmoja ni MALAYA... vunja mtandao..tulizana.
   
 7. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Peter....
  u seem to still love him so forgive and forget and get back together, don't worry about money since you can help each other (that's what couples do). u only want John bcoz he is established in life but u dont really love him, so let him go..

  A word of advice: is solve ur problems instead of breaking up. i don't know y u broke up with peter b4 but if that situation arises again, solve it peacefully otherwise u'll come to hate him even more
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kwani wanaume ni hao tu?
  ila kama ulimwengu wako wa wanaume ni hao...mimi naprefer john ..
  maelezo zaidi nitakupm maana hapa wanga wengiiiiiiiiii
   
 9. Da Asia

  Da Asia JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 725
  Likes Received: 369
  Trophy Points: 80
  OGOPASANA, naomba tu niweke wazi kua, mpaka naandika hapaa hakuna hata mmoja kati ya hawa wawili ambaye nimeshampa green light. ingekua hivyo wala nisingetaka nasaha zenu maana tayari ningekua nimeshafanya maamuzi.
  Asante kwa ushauri.

   
 10. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Love is not finding someone to live with; it's finding someone you can't live without

  Ebu mpe Penzi lake huyo asiye na hela maana hata ukienda kwa John najua utakuwa unazini nafsini mwako kila siku na Peter.
   
 11. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Usikilize moyo wako na tumia akili kwani mda unakwenda....
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Asprin, Maisha yenyewe ya kujivunga yako wapi?
  Kesho na keshokutwa niwe na ukavumacho hata maisha yenyewe sikuyala???


  Hapa ni kata mti panda mti, period!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,958
  Likes Received: 23,634
  Trophy Points: 280
  We Da Asia, sikiliza ushauri wangu mie kikongwe babu ODM.

  Ni hivi... :

  Maisha ni mafupi sana.... ukipata nafasi ya kuinjoi usiipoteze.
  Peter mlishawahi kuwa pamoja na ikashindikana mkaachana. Nani alikudanganya jasiri anaacha asili? Hakuna kitu kibaya kama kuumizwa mapenzini mara mbili na mtu mmoja. Usisahau alishakuwa na mwanamke mwingine na ujue kuwa mahawara hawaachani. Pia huyu Peter huyu kama we umemshindwa, na huyu mwingine pia kamshindwa... huyu ni kunguru huyu, hafugiki huyu. (SAmahani najua unampenda lakini ndo hivyo, kunguru ni kunguru tu)

  John anakupenda sana... hakuna kitu kizuri mapenzini kama kupendwa. Ana mahela, ni mtu mzima..... (Kama necha itachukua mkondo wake atakufa kabla yako, unaukwaa utajiri lol) Jifunze kumpenda bana ule maisha. maisha mafupi haya.

  Kama hujanielewa namaanisha hivi... Go For John Bana.:clap2::clap2:
  Hivi leo jumangapi vile? Damn!
   
 14. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,217
  Likes Received: 8,292
  Trophy Points: 280
  monsieur go for Peter.because men of that type are very brave.
   
 15. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  nenda kwa john,john john ...achana na wauza sura...
   
 16. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  dada, unajua unajiweka katika wakati mbaya sana wakati unajihusisha na WAUME ZA WATU? unatakiwa UPATE SABABU za KWA NINI HAO WOTE WALIACHANA NA WAKE ZAO? ili yasije kukukuta kama yaliyowakuta wenzako hao wa kabla. Naamini hakuna mwanamke hata mmoja anayependa kushare mumewe na mwanamke mwingine, na HATA WEWE usingependa hilo likutokee, na hakuna mwanamke atakayekuwa na urafiki na mwanamke aliyemchukua mume wake...JIANGALIE usije kuwa unadanganywa kuwa kuna divorce kumbe hakuna ukajitafutia dhambi za bure...
   
 17. LD

  LD JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ugonjwa wangu mimi ni KUPENDA!!! Ingekuwa mimi nitakwenda ninapopapenda zaidi...ambapo nafsi yangu inapata furaha na amani. Manake wakati mwingine Mapenzi ni utumishi kwa huyo mpenzi. Na hivi mwanamke tena, kumtumikia mtu ambaye hayuko kwenye nafsi yangu SIWEZI.

  Fedha zinatafutwa na kupatikana lakini FURAHA na Shangwe ya nafsi avinunuliwi....utajitahidi lakini wapi. Hivyo kwa kweli nitazingatia kwa yule Nimpendaye zaidi. Tatizo ni kujua tu kama yeye anakupenda kweli au anaigiza? Manake bwana maigizo nayo yamezidi siku hizi.
   
 18. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inakuwaje mtu ambaye humpi nafasi katika nafsi yako akuweke njia panda?(John) Na issue za relationship kwangu binafsi kushauri ni kazi maana inakuwa kama vile kumchagulia mtu partner wa kuishi nae for the rest of his/her life. Kama unampenda Peter na ni mwenye kipato duni endelea nae na huyu John kinachokuweka njia panda ni pesa yake and not true love kitu ambacho huenda kikaathiri maisha yako vile vile. For JUST FOLLOW YOUR HEART only thing I can say.
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,958
  Likes Received: 23,634
  Trophy Points: 280
  Khaaa! Leo ndo nimejua definisheni ya jina Kongosho.... Kumbe kongosho inamaanisha Mchimvi!.......... hahahaha umeenda kupekua makabrasha... unamfaa sana Shigongo wewe.

  Tatizo Peter wa kule ni mwajiriwa na bibie kamzidi mshahara, huyu wa sredi hii ni mishen town. Labda Da Asia atuambie kumbe kuna njemba jingine la tatu liko kwenye list yake..... khaa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha ha, chezeiya Konnie akiingia kwenye fani.

  Huyu Peter labda aliachishwa kazi, ndo atuambie.

  Nilitaka kumuonesha kuwa bora aendelee na John, Peter hana akili ya kuoa.

   
Loading...