Bemendazole
JF-Expert Member
- Nov 14, 2020
- 2,716
- 6,823
Niko hapa napata kinywaji ili kumalizia wikiend, ghafla namkumbuka Dr Manguruwe!
Hawa ni moja ya madogo niliowalea kiroho kipindi tunasoma sekondari kule Mbeya.
Simon alikuwa ni mmoja ya watoto wazuri, mtiifu na mnyenyekevu aliyefuata maadili ya kiroho.
Kifupi, alikuwa ni moja ya vijana niliokuwa najivunia.
Baada ya kupotezana naye kwa miaka mingi, nilikutana naye Chanika kwenye mwaka 2017 akasimamisha gari yake aina ya Prado, akanielezea mishe zake za kuwawezesha wakulima katika kilimo cha papai.
Baada ya miaka michache mbele, nikaanza kumuona kwenye Tv na mitandaoni.
Kwa kweli mwenendo wake ulikuwa umebadilika na alikuwa siyo yule tena niliyemfahamu.
Nikajisemea moyoni kuwa kwa mwenendo huu, kijana hatofika mbali.
Na kweli. Hivi sasa Simon yuko sehemu mbaya.
Nasikitika kumuona mdogo wangu anapata shida, anasota gerzani nikiwa sina namna nzuri ya kumsaidia.
Hivyo nakuomba mh Raisi, ikikupendeza, umuelekeze DPP, aweze kumalizana na huyu dogo nje ya mfumo wa mahakama ili dogo aweze kurudi uraiani, kwani ana majukumu na familia iko inateseka.
Wasalaam.