Nikiwa nyumbani nitashindwa kufanya michongo kiufasaha

Ankoh Mazukuh

Member
Jan 16, 2023
27
29
Wanangu wa JF mimi bwana nina jambo langu em naombeni ushauri kidogo.

Mimi bwana nimemaliza chuo mwaka jana mwaka huu mwishoni natimiza miaka 23 naishi na mama yangu peke yake mzee alishafariki miaka mitatu sasa ma bro zangu walishaoa masister nao vile vile.

Sasa bwana changamoto yangu ni moja nikiwa nyumbani nakuwa mvivu sana pia akili haichangamki kama nilivyokuwa chuo. Maana nilovyokuwa chuo nilikuwa napambana maana. Niliamini kwenye kipaji changu sana pia nilikuwa na dhana ya kujiajili so nilivyo kuwa chuo nilipambana mpaka nikafanikiwa kufungua ofisi yangu.

Lakini sasa tangu nimemaliza chuo uchumi uliniyumbia lakini pia nilitamani biashara yangu niihamishie mjini Dodoma ambapo ndio kuna soko kubwa na ndo nyumbani sasa tangu nimerudi naona uchawi uchawi tu sielewi kila siku nina mipango mipya.

Leo nawaza kitu baadae nabadilika. Kitu kibaya mwanzoni sikutaka kufikiria kama nyumbani watanipa mtaji lakini nilivyorudi wakaonyesha kunisaidia alafu baadae wamebadilika so kama vile nimeachwa kwenye mataa.

Sasa ushauri ninao uomba ni huu mimi nilitamani nitoke nyumbani nikapange angalau akili ichangamke kuliko kuamka sehem moja chakula uwakika sijui nini yaani sasa shida mama yangu hataki kusikia kabisa hizo habari tena nilipo jaribu kumwambia kulizuka mambo mengi kiasi kwamba akataka kunitoa kwa laana sasa nikaogopa sana.. Bimkubwa anadai kuwa mimi ni mdogo pia anasema nataka nipange kwa sababu ya wanawake so nikae nyumbani mpaka nitakapo oa.

Pia hawezi kulipa kodi mara mbili yaani imekuwa changamoto nikimwambia najilipia kodi ndo ugomvi zaidi anasema kumbe nina hela ndio zinanipa kiburi ugomvi mwingine anataka awe anajua bank nina kiasi gani na vitu vingine vingi kama hivyo sasa mimi kwangu hii ni changamoto mno.. Kuendelea kukaa nyumbani tu naona kama sikui kiakili.

Yaani tofauti na nilivyokuwa chuo kingine anadai kuwa napenda sana hela. Kwa sababu mze aliniachia nyumba ambayo kwa sasa hivi inaingiza hela na bimdashi aliahidi kunikabidhi nikimailiza chuo sasa nilichokosea ni kugusia iyo mada. Lakini binafsi sijitaji mali za urithi natamani na mimi kuwa na mali zangu kwa amani sasa hapa ni changamoto kwakweli naombeni ushauri wadau.
 
Kazia hapo hapo mzee step out of your comfort zone

Bi mkubwa wako anakupenda sawa lakini you're a grown up guy who has to be independent..... at some point in life kukaa nyumbani napo ni kama utumwa

Kama unauhakika unaweza ku survive nje ya home nenda...Bimkubwa wako anakutishia laana hamna chochote hapo anakutisha tu

Wangapi wanatamkiwa maneno ya baraka na mafanikio na wazazi wao lakini bado maisha yanawachapa

All the best bro...see you at the top
 
If you know you know kama kweli wewe Ni mpambanaji basi unaweza pambana popote

Kwani ukiwa unatoka unaenda kwenye mishe zako jioni unarudi Kuna shida gani

Anyway good luck
 
Wanangu wa JF mimi bwana nina jambo langu em naombeni ushauri kidogo..

Mimi bwana nimemaliza chuo mwaka jana mwaka huu mwishoni natimiza miaka 23 naishi na mama yangu peke yake mzee alishafariki miaka mitatu sasa ma bro zangu walishaoa masister nao vile vile. Sasa bwana changamoto yangu ni
Tumiaka 23 tu unahama nyumbani ili iweje. wenzio tuna 40 na hatujawa na hayo mawazo
tulia dogo
 
Kazia hapo hapo mzee step out of your comfort zone

Bi mkubwa wako anakupenda sawa lakini you're a grown up guy who has to be independent..... at some point in life kukaa nyumbani napo ni kama utumwa...
Thank you but me nilikuwa nimewaza labda niende nikasome chuo sehem ambayo najua my business will grow fast tofauti na kule mwanzo nilipokuwepo nilikuwa nasoma Mbeya biashara ya photography hapana but napenda sana photography unawez pia nifwatilia kazi zangu instagram @munixpic
 
Uzuri ushajua mapungufu yako. Basi ushashinda.

1. Tafuta hela kidogo utafute chumba ukodi ata cha 50k. Ukae tu uko. Tena kaa mbali na maskani isje kua jioni unarudi kula home afu ghetto unarudi kulala tu.

2. Anza tu na godoro. Akili itaamka tu usijali. Mdogo mdogo watu tulianza na kulala chini sahivi tuna hadi subwoofer.

3. Work hard bro.
 
If you know you know kama kweli wewe Ni mpambanaji basi unaweza pambana popote

Kwani ukiwa unatoka unaenda kwenye mishe zako jioni unarudi Kuna shida gani

Anyway good luck
Kuna namna n ngumu sometimes narudi usiku sana... Unakuta nimeenda ukumbini so changamoto n nying alaf mzazi anakuwa aelewi agomba sana asa me hicho kitu ndio sipend naona kama kinanikosesha amani
 
Endelea kukaa hapo nyumban, na mbadilishie wanawake kila siku mwenyewe atakuruhusu ukapange

Pia usijionyeshe kuwa una hela anza kumuomba hela za matumizi madogo madogo mwenyewe atakuchoka
 
Nakazia.

Bimkubwa anakuchelewesha, kumbuka una dada na kaka zako kubak kama mrithi wa nyumba mojawapo itakuletea ugomvi na hao nduguzo, komaa kaza nje na home na unajua kuishi chini ya maamuzi yako akili itatatanuka na ni kipimo tosha kuwa umekuwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom