Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 10,884
- 18,824
Wakuu mi sitaki vyeo vikubwa kama ndugu Dennis Robert Shughuru , ukuu wa mkoa tu unanitosha.
Pombe/wine ya asali ni pombe moja ghali sababu ya ughali wa asali. Tanzania ni ya pili Afrika baada ya Ethiopia kwa uzalishaji wa asali. Mkoa wa Tabora ni mkoa unaoongoza kwa kuzalisha zao hilo nchini. Na asali yake ni moja ya asali inapendwa zaidi duniani sababu ni asali ya msituni.
Nikiwa mkuu wa mkoa wa Tabora, katika kuliongezea zao hilo thamani na kukuza uchumi wa watu wa mkoa wangu nitahakikisha naenda huku na huko kutafuta wawekezaji wa kujenga viwanda vya pombe ya asali. Nitawapa incentives kwa kuwapatia maneno ya kujenga viwanda vyao bure, kuwapelekea huduma za maji na umeme.
Mead tofauti na wine inachukua muda mfupi sana kulipa. Ulitaka kutengeneza wine itakuchukua miaka si chini ya mitatu kuvuna zabibu. Na pengine zaidi ya mwaka ili tena kusubiri wine iive kiwandani. So inaanza kukulipa labda mwaka wa Tano.
Mead yenyewe unaweza kununua asali leo, baada ya miezi sita, au hata chini ya hapo unaanza kuuza.
Hesabu za kwenye makaratasi: Pombe ya asali kwa wastani huko majuu wa Tsh 30,000 kwa chupa ya 750mls. Kwa wastani klo moja ya asali hutoa lita nne mead. Hiyo ni chupa tano za 750mls. Ni kama laki na nusu. Hii ni bei ya retail. Labda viwanda vitauza nusu yake.
Bei ya asali kwa kilo inacheza 5,000 hadi 10,000. So kwa meadery iliyojengwa na gharama zake ikawa asali, umeme, maji, yeast, wafanyakazi, packaging na vikolombwezo vingine vya kila siku hii ni biashara kubwa sana inayoweza kufanya mkoa wa Tabora kuinuka kiuchumi. Nchi yetu inazalisha kama tani 30,000(Kilo milioni tatu) za asali kwa mwaka. Sehemu kubwa ikitoka Tabora. Kwa kuvutia wawekezaji kadhaa wa viwanda vya pombe ya asali mkoa Tabora nitainua sana uchumi wa mkoa, na kuufanya uwe kitovu cha pombe ya asali Afrika na pengine duniani.