vanmedy
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 2,698
- 1,395
Kila akipata kibunda aende mwenyewe sokoni anunue mahitaji yote kwa jumla..Swali toka kwa mdau mmoja hapa ofisini leo asubuhi, anasema anautaratibu nyumbani kwake wa kutoa matumizi ya kawaida kwa mwezi kati ya laki nne hadi sita kutokana na mwezi umeenda vizuri vipi, wakati mwingine sikukuu mambo yakiwa sawa huenda hadi laki nane, lakini mambo yakiwa magumu hasa nyakati za ada, basi hupungua na kuwa laki tatu.
Swali ni hili, anafahamu mke wake anakuwa na mahitaji yake, hana tabia ya kuuliza listi, lakini wakati mwingine mahitaji huisha ndani ndani ya wiki mbili ama tatu na imekuwa akiuliza tu, basi ni ugomvi, na anaambiwa anafikiri watu wezi. February hali ilikuwa ngumu na aka afford kutoa laki mbili sabini. Jana amepewa taarifa na msichana wa kazi kuwa vitu kadhaa vimeisha, asubuhi amemuuliza mwenzake ugomvi umeanza na mwanamke anasema anataka kuondoka.
Familia ni ya watu tano, watoto wawili, mdada wa kazi , mke na mume. Mkewe kwa sasa ni mama wa nyumbani
Hebu toeni ushauri
Unga nusu kiroba
Mchele nusu kiroba
Harage nusu kiroba
Dagaa robo kiroba
Ngano nusu kiroba
Chumvi za kutosha.
Mafuta ndoo ndogo
.. halafu awe anaacha pesa za matumizi ya ziada kwa siku za kupiga nyama,ndizi, samaki na kuku...
Unampigaje na kibunda chote at once.. laki 4 hadi 6 ni mshahara wa mtu mjini hapa na ana familia na kodi analipa.
Kwakuwa ameshamzoesha ajiandae na mabifu yasiyoisha... sasa bibie anatishia kuondoka anamzuia akitest tu unamchapa na talaka moja kabisa.. baki na watoto na msaidizi wao.. halafu uone ataeleza nini kwao sababu ya kurudi..
Sent using Jamii Forums mobile app