Nikiuliza matumizi mbona anakuwa mkali

vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,572
2,000
Swali toka kwa mdau mmoja hapa ofisini leo asubuhi, anasema anautaratibu nyumbani kwake wa kutoa matumizi ya kawaida kwa mwezi kati ya laki nne hadi sita kutokana na mwezi umeenda vizuri vipi, wakati mwingine sikukuu mambo yakiwa sawa huenda hadi laki nane, lakini mambo yakiwa magumu hasa nyakati za ada, basi hupungua na kuwa laki tatu.

Swali ni hili, anafahamu mke wake anakuwa na mahitaji yake, hana tabia ya kuuliza listi, lakini wakati mwingine mahitaji huisha ndani ndani ya wiki mbili ama tatu na imekuwa akiuliza tu, basi ni ugomvi, na anaambiwa anafikiri watu wezi. February hali ilikuwa ngumu na aka afford kutoa laki mbili sabini. Jana amepewa taarifa na msichana wa kazi kuwa vitu kadhaa vimeisha, asubuhi amemuuliza mwenzake ugomvi umeanza na mwanamke anasema anataka kuondoka.

Familia ni ya watu tano, watoto wawili, mdada wa kazi , mke na mume. Mkewe kwa sasa ni mama wa nyumbani

Hebu toeni ushauri
Kila akipata kibunda aende mwenyewe sokoni anunue mahitaji yote kwa jumla..
Unga nusu kiroba
Mchele nusu kiroba
Harage nusu kiroba
Dagaa robo kiroba
Ngano nusu kiroba
Chumvi za kutosha.
Mafuta ndoo ndogo

.. halafu awe anaacha pesa za matumizi ya ziada kwa siku za kupiga nyama,ndizi, samaki na kuku...
Unampigaje na kibunda chote at once.. laki 4 hadi 6 ni mshahara wa mtu mjini hapa na ana familia na kodi analipa.
Kwakuwa ameshamzoesha ajiandae na mabifu yasiyoisha... sasa bibie anatishia kuondoka anamzuia akitest tu unamchapa na talaka moja kabisa.. baki na watoto na msaidizi wao.. halafu uone ataeleza nini kwao sababu ya kurudi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tumbayz

Member
Oct 11, 2018
79
125
Matumizi ya ndani yawe na kiasi kila mwezi though mwezi huu yanaweza kua chini na mwngne yakawa juu ila hizo tofauti ni ndogo sana
Ila pia mume unaweza kwenda sokoni kwa week au 2 weeks ukaweka kila kitu ndani then uone km kutakua na tofauti ktk bajeti,
Huku usisahau kumpatia wife pocket money ya kwake binafsi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RicMbowe

Member
Nov 21, 2018
78
125
Kazi ya mume ni kutunza familia, Kazi ya mke ni kumsaidia mume (kwenye kila kitu ikiwemo masuala ya uchumi wa familia), sasa wewe endelea kusubiri kutunzwa huku unashinda ndani siku nzima ukiangalia tamthilia,
kazi ya mume ni kutunza mke, ila kwa panic yako inaonesha wewe ni wale wanaume marioo waliozoea kutunzwa na wanawake
, na
 
RicMbowe

Member
Nov 21, 2018
78
125
kazi ya mume ni kutunza mke, ila kwa panic yako inaonesha wewe ni wale wanaume marioo waliozoea kutunzwa na wanawake
Af ww unaonesha ni zile type za wanawake wa uswazi waliokulia kwenye familia zenye maisha magumu, mama hajishughulishi kwa chochote, ndomana hujajifunza kuwajibika, jamani kwa wazazi tunapolea watoto tujue mambo muhim kama uwajibikaji watoto hujifunza nyumbani, sio unamsomesha mtt wa kike af kichwani kwake anategemea ataolewa atatunzwa badala ya kufkiria akiolewa ataenda kujenga familia na mumewe, mwanamke wajibika lakin nafasi ya mumeo kama kuongozi wa familia ipo palepale.
 
Jan 19, 2020
61
150
Maisha banaa.. Kweli kuna watu wanaishi sisi wengine ilimradi siku zimesogea! Laki8 hekoo

Hapo anaposema anataka kuondoka anaenda kwenye nyumba yake aliyojenga kwa hela za matumizi.

Jamaa afanye manunuzi mwenyewe either kwa week au mwezi! Yeye ampatie hata kalaki tu kanatosha, hiyo nyingine afanye saving kwa ajili ya kesho yao..maisha yanabadilika mambo yanaeza kwenda mrama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siempre Hechos

JF-Expert Member
Dec 9, 2016
1,062
2,000
Yes nilisusa, hakuna kitu kibaya kama kutoaminiwa kwenye ndoa, mimi nilimwambia kuanzia leo sitaki hela yako kanunue kila kitu mwenyewe, ikabidi tu awe mpole tukayaongea yakaisha sikuhizi haulizi tena
Unamsaidia mumeo matumizi ya nyumbani? nimeulza kwa nia njema tu mkuu!
 
The Initiator huru

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,316
2,000
Swali toka kwa mdau mmoja hapa ofisini leo asubuhi, anasema anautaratibu nyumbani kwake wa kutoa matumizi ya kawaida kwa mwezi kati ya laki nne hadi sita kutokana na mwezi umeenda vizuri vipi, wakati mwingine sikukuu mambo yakiwa sawa huenda hadi laki nane, lakini mambo yakiwa magumu hasa nyakati za ada, basi hupungua na kuwa laki tatu.

Swali ni hili, anafahamu mke wake anakuwa na mahitaji yake, hana tabia ya kuuliza listi, lakini wakati mwingine mahitaji huisha ndani ndani ya wiki mbili ama tatu na imekuwa akiuliza tu, basi ni ugomvi, na anaambiwa anafikiri watu wezi. February hali ilikuwa ngumu na aka afford kutoa laki mbili sabini. Jana amepewa taarifa na msichana wa kazi kuwa vitu kadhaa vimeisha, asubuhi amemuuliza mwenzake ugomvi umeanza na mwanamke anasema anataka kuondoka.

Familia ni ya watu tano, watoto wawili, mdada wa kazi , mke na mume. Mkewe kwa sasa ni mama wa nyumbani

Hebu toeni ushauri
haloooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,948
2,000
Andaa daftari la bajeti, Andika bajeti ya kila mwezi mkishirikiana, bajeti ya sikukuu iwe tofauti na bajeti ya ada pia.

Kuna pesa unaweza muachia nyingine unakaa nayo kulingana na bajeti.

Kwa idadi ya watu wa 5, kwa uzoefu wangu mwezi hakizidi laki 4.5 hayo tena ni maisha ya juu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mocrana

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
536
250
Swali toka kwa mdau mmoja hapa ofisini leo asubuhi, anasema anautaratibu nyumbani kwake wa kutoa matumizi ya kawaida kwa mwezi kati ya laki nne hadi sita kutokana na mwezi umeenda vizuri vipi, wakati mwingine sikukuu mambo yakiwa sawa huenda hadi laki nane, lakini mambo yakiwa magumu hasa nyakati za ada, basi hupungua na kuwa laki tatu.

Swali ni hili, anafahamu mke wake anakuwa na mahitaji yake, hana tabia ya kuuliza listi, lakini wakati mwingine mahitaji huisha ndani ndani ya wiki mbili ama tatu na imekuwa akiuliza tu, basi ni ugomvi, na anaambiwa anafikiri watu wezi. February hali ilikuwa ngumu na aka afford kutoa laki mbili sabini. Jana amepewa taarifa na msichana wa kazi kuwa vitu kadhaa vimeisha, asubuhi amemuuliza mwenzake ugomvi umeanza na mwanamke anasema anataka kuondoka.

Familia ni ya watu tano, watoto wawili, mdada wa kazi , mke na mume. Mkewe kwa sasa ni mama wa nyumbani

Hebu toeni ushauri

MREJESHO....MREJESHO

Baada ya kusoma comments ambazo zina mwelekeo chanya. Nilirejea nyumbani na kumtaarifu bibiye nikiwa na mshenga kuwa nahitaji asepe akapumzike nyumbani sababu sijapendezewa na hiyo tabia yake ( mkwara tu). Aliangua kilio kikuuuuuubwa sana na kuomba msamaha. To cut the story short. Sitakuwa natoa hela lumpsum. Ntanunua vitu mwenyewe na kumwachia matumizi. Sababu nimepita maduka na masoko kadhaa kama wale majamaa zangu wa procurement nikafanya price analysis na nimegundua mengi.

Asanteni kwa michango yenu
Aiseee,
 
Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
17,935
2,000
aisee hata mimi mume wangu akinileteaga hizo za eti hela umefanyia nini lazma huwa panachimbika, kuna kipindi hadi nilisusa kupokea hizo hela zake za matumizi mwenyewe amejirekebisha ameacha kabisa biashara ya kuniuliza eti hela umefanyia nini mbona imeisha haraka, inakera bwana
naona wewe ndo umeoa!au umeolewa na boya!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom