Nikiuliza matumizi mbona anakuwa mkali

aisee hata mimi mume wangu akinileteaga hizo za eti hela umefanyia nini lazma huwa panachimbika, kuna kipindi hadi nilisusa kupokea hizo hela zake za matumizi mwenyewe amejirekebisha ameacha kabisa biashara ya kuniuliza eti hela umefanyia nini mbona imeisha haraka, inakera bwana

Na nyie mnapenda sana hela za bure mjue kuzitafuta, me ukikasirika wala sijal, wanawake wanapendaga kujinunisha bila sababu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mawasiliano ni muhimu kwenye ndoa , nilijua anajenga kiwanja si tulinunua wote,ila mimi nilikuwa nasafiri ndani na nje ya nchi. Naweza kaa nje ya nchi mwezi mzima kila kitu kiko poa.

Hivyo sio kila siku unaulizia jengo limefika wapi,

Ninachosema hela zikibaki alikuwa ananiambia zile za mwezi uliopita zilizobaki tuzifanyie nini ?

Unaona wenzako Mungu alivyowapa hekima. Huyu wife wangu angejua ID yangu asingeamini nampenda hivi.

Tulishajenga Tabata, zilizobaki ni story.

Badilisha huo msimamo haukusaidii kitu labda kama na wewe una kipato chakutosha kuchangia bajeti. Vinginevyo mikwara yako haina busara kabisa. Mmeo atashangaa kwanza hawezi amini, utakapoacha hiyo mikwara ya kipuuzi.
Siku moja mwambie Baby mbona laki 2 zimebaki za mwezi january fanya kucheki tu utarudi hapa kuniambia.

Hata hivyo sijui matatizo ya wengine lakini mi nilipata mtoto wa kihehe mbichiiiii bikra. Nimetusua mwenyewe. Na amelelewa vizuri na wazazi, sijawahi kujuta.
Namshukuru Mungu sana
huna lolote kwa uandishi wako tu unaonekana hata ndoa huijui, ingia kwanza ndo uje uongee for now let the grown up talk
 
Hauwezi kuwa unatumia kwenye mambo yenye manufaa kwa familia halafu ugeuke mbogo unapoulizwa jinsi ulivyotumia.Soma pia comment za watu juu ya mchango wako,jifunze ubadilike au ficha upumbavu wako kwa kukàa kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
wewe ndo ukae kimya mana naona una panic kwa yasiyokuhusu, pambana na mkeo mimi sikuhusu
 
Kwa huu mtazamo kweli lazma pachimbike, ni mtazamo wa kiboya sana kwa dunia ya leo, kwahyo usipopewa hela na mumeo suluhu ni kuchepuka, jiulize mchango wako kwenye familia ni upi? Je ni kutoa papuchi na kuzaa watoto tu? Ww huna mikono na akili, hamna unachoweza fanya ili kikupe hela, maisha kusaidiana mama. Labda kama kwako ni tofauti, ila kama na we ni mama wa nyumbani, una house girl, watoto wachache, utakuwa mzembe sana kusubiri utunzwe kama mzigo
kazi ya mume ni kutunza mke, ila kwa panic yako inaonesha wewe ni wale wanaume marioo waliozoea kutunzwa na wanawake
 
Si wote wabinafsi kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiacha kufugwa ukaanza kujitegemea ndio utajua kama ni ubinafsi au akili.
Laki nane kwa mwezi familia ya watu wa tano mtu anamaliza yote?Anashindwa hata kufikiria kusave na kufungua mradi utakao support familia siku mambo ya kienda mrama?
Kuna familia hiyo laki nane ndio mshahara wa baba alipe ada,aangalie afya ya familia, chakula, mavazi etc na bado mke anakua na akili ya kufanay side hustle.
Sasa wewe kwa akili yako ya kimandazi unaona kusave laki 8 ili afanye kitu ni ubinafsi??? Nakuambia hiviii kua kaka/dada ukiacha kufugwa utayaelewa maisha kwa upana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anafugwa aliyekuzaa na kukunyonyesha

Kuna mdada hapo juu sijui kadhamiria au limemtoka tu bahati mbaya! Yaani pesa ninayokupa ya matumizi iwe kwa wiki, siku au mwezi inipe tabu tena kuiulizia iwapo nitaona vinavyotumika havilingani na uhalisia?

Sijaoa bado, siku nikioa yakawa ya namna hii na mtu anatishia kuondoka ni bora akwende tu.
 
Mpenzi, haya mambo huwa mnatuzoesha ninyi wenyewe tangu mwanzo kabisa wa mahusiano. Unapompa pesa mtu unatakiwa useme wazi kabisa kuwa ndio bajeti ya mwezi mzima. In fact, inatakiwa ijulikane kabisa inaenda kununua nini na nini kama ni pesa ya matumizi binafsi ujulikane ni kiasi gani. Sasa wewe mwanzoni unanipa laki sita, baada ya wiki mbili nikisema mahitaji yameisha unanunua bila hata kuhoji halafu naachaje kujiachia na kununua kila nguo mpya inayotoka? Halafu from nowhere uanze kuniuliza unadhani nitakuelewa? Nitahisi umenichoka. Ila mambo yote inategemea makubaliano yenu tangu mwanzo kabisa wa ndoa yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui mimi ndiye Mpumbavu nisiyeelewa haya mambo!?

Hivi dada, nimetoa laki nane au tano ya matumizi nyumbani kwa mke wangu. Yeye mke atashindwa kujiongeza kwenda duka la jumla au sokoni akanunua vitu vinavyoweza kudumu ndani hata kwa mwezi mzima!? Kwamba kufanya budget unataka ukafundishwe kwa mume wakati nimekuoa kutoka kwenu na rundo la Mahari!!?
 
Familia yangu ni ya watu watatu. Huwa nanunua kila kitu mwanzoni mwa mwezi. Halafu wife nampa 250,000/=, hapo mpaka mwezi uishe ndiyo natoa tena 250,000/=. Na mambo yanakwennda vizuri tu
 
Sijui mimi ndiye Mpumbavu nisiyeelewa haya mambo!?

Hivi dada, nimetoa laki nane au tano ya matumizi nyumbani kwa mke wangu. Yeye mke atashindwa kujiongeza kwenda duka la jumla au sokoni akanunua vitu vinavyoweza kudumu ndani hata kwa mwezi mzima!? Kwamba kufanya budget unataka ukafundishwe kwa mume wakati nimekuoa kutoka kwenu na rundo la Mahari!!?
Siku zote unatakiwa ujue udhaifu wa mwenza wako, kuna watu wamekulia kwenye mazingira ambayo mama na hg ndio kila kitu yeye anakuwa hajui lolote kuhusu budgeting. Ukiona hivyo inabidi mwanaume umfundishe mkeo hakuna namna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali toka kwa mdau mmoja hapa ofisini leo asubuhi, anasema anautaratibu nyumbani kwake wa kutoa matumizi ya kawaida kwa mwezi kati ya laki nne hadi sita kutokana na mwezi umeenda vizuri vipi, wakati mwingine sikukuu mambo yakiwa sawa huenda hadi laki nane, lakini mambo yakiwa magumu hasa nyakati za ada, basi hupungua na kuwa laki tatu.

Swali ni hili, anafahamu mke wake anakuwa na mahitaji yake, hana tabia ya kuuliza listi, lakini wakati mwingine mahitaji huisha ndani ndani ya wiki mbili ama tatu na imekuwa akiuliza tu, basi ni ugomvi, na anaambiwa anafikiri watu wezi. February hali ilikuwa ngumu na aka afford kutoa laki mbili sabini. Jana amepewa taarifa na msichana wa kazi kuwa vitu kadhaa vimeisha, asubuhi amemuuliza mwenzake ugomvi umeanza na mwanamke anasema anataka kuondoka.

Familia ni ya watu tano, watoto wawili, mdada wa kazi , mke na mume. Mkewe kwa sasa ni mama wa nyumbani

Hebu toeni ushauri
Mzee mkeo ni mkeo tu.Unachoweza kufanya ni hivi,Nunu mchele na unga kg 50 50 na maharage kilo 25 ulete nyumbani kisha unampa elfu 50 ya mboga kwa mwezi mzima akitaka matumizi mengine akwambie umpe.Kisha uone kama matumizi ni madogo au makubwa.Pia anagalia aina ya menu mnayokula kama kweli kuna value for money.Ukiona vipi basi mfundishe mwenzi kubana matumizi
 
Subiri utakaribishwa kwenye bonge la Nyumba, lenye usajiri wa mama yake utasikia "baby mama kasema tutoke uswahilini tuje kuishi hapa.
 
Mwanamke hovyo hovyo utamjua tuu

Back
Top Bottom