Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,210
Mwenzenu mie nina maswali kwa Kikwete. Natamani nimuone Kikwete popote, iwe ni Ikulu au safarini katika kampeni ili nimuulize maswali haya:
- Kabla ya kuanguka siku ya tar 21/08/2010 wakati akifungua kampeni alionyesha kushituka sana, akasema "AISEE!!" akatulia kama sekunde arobaini hivi bila kusema neno, akauma meno halafu akaendelea kusema tumefanya mambo mengi huku akielekea chini kama mtu aliyesukumwa kwa nguvu na kitu. Swali ni je Kikwete aliposema Aisee, alikuwa ameona nini? Kama alijua kuna nguvu ambayo ilimzidi,kwanini hakufanya haraka kukimbilia kiti kabla hajaanguka kwa kishindo? Je jambo hili ni la kiafya au lina nguvu za giza?
- Jana tar 21 ilikuwa ni mara ya tatu kwa rais kuanguka mbele ya hadhra. Je anajua tatizo linalomkabili? Ikiwa anajitambua kwamba uwezo wake wa kustahimili mikiki mikiki ya kuongoza nchi ni mdogo, haoni kwamba kuna umhimu wa yeye kuridhika na miaka mitano aliyoongoza nchi na hiyo mingine akamwachia mwingine?