Nikikumbuka Mambo haya yaliyofanyika miaka mitano iliyopita nakua nasikitika Sana,naomba yasijirudie Tena.

Wagombe wa ubunge wa upinzani nchi Zima kushindwa uchaguzi,

Wagombe wa upinzani kutekwa wakirudisha fomu kwa wasimamizi wa uchaguzi,

Wagombe wa upinzani peke yao kukosea kujaza fomu za uchaguzi tu,

Wasimamaizi au maofisa wa uchaguzi kutokuwepo ofisini pale tu wagombe wa upinzani walipokua wakirudisha fomu,

Wakurugenzi kuogopa kuwatangaza washindi wagombe wa upinzani kwa sababu walionywa kuwa wamepewa magari na fedha wakitangaza mpinzani kashinda watakiona Cha moto, Ni kweli wengi walishinda lakini hawakutangazwa,

Mawakala wa wagombea wa wapinzani kufukuzwa ndani ya vyumba vya kupigia na kuhesabia kura,

Wasichana wanafunzi walipigwa mimba kwa kutongozwa na wanaume lakini wanaume hao waliendelea na masomo au kazi zao lakini wasichana hao kutokuruhusiwa kuendeleza na masomo,

Agizo kwamba wabunge wa upinzani wakorofi wafukuzwe bungeni wakija uraiani nako watashughulikiwa,

Kauli Kama "maendeleo hayana vyama,ikipingana na msinichanganyie berti na magunzi,msinichagulie wapinzani sitawaletea maendeleo",

Kauli Kama msiwabomolee watu wa kwetu kwani hawa ndio walionichagua,

Nikikumbuka mashamba ya mboga ya Freeman yalivyovurugwa,

Nikikumbuka club yetu pendwa Bilicanas ilivyosambaratishwa,

Nikikumbuka watu wasiojulikana walivyowapoteza baadhi ya Watanzania wenzetu, walivyoiteka nchi yenye polisi mahili kabisa EA,Jeshi madhubuti kabisa Afrika,Maspy Bora kabisa duniani,

Watu walipoteza,waliteswa na kuuwawa lakini hakuna watekaji ama wauaji waliokamatwa,

Watu waliwekwa mahabusu miezi zaidi ya sita kinyume Cha sheria,

Kuna watu walipigwa faini kubwa ambayo hawangeweza kulipa ilibidi wananchi wenye mapenzi mema wawachangie,


Nikikumbuka Maxence Melo aliambiwa awataje kwa majina wakazi wa Jamiiforums,

Nikikumbuka wafanyakazi wakimaliza miaka mitano bila increment,promotion Wala ongezeko la mishahara,

Wakulima wa korosho walivyokutana na wanunuzi wa korosho ambao hawakuwazoea,maana walikuja na maroli na nguo za mabakamabaka,

Wafanyabiashara walipekuliwa akauti zao na Kodi nyingi walibambikiwa waliokufa na wengine walisepa,

Nawakumbuka wafanyabiashara wa bureau de change,

Wanafunzi wa vyuo vikuu walijikuta wanabaguliwa kupata Loan board tofauti na hapo kabla,

Wanafunzi wa vyuo waliopata ajira walijikuta wanalipa loan board zao kwa riba kubwa kinyime na mikataba ya awali,

Wakazi wa Kagera hawata sahau tetemeko la ardhi lilivyowatesa na baadae masimango yakafuata badala ya kufarijiwa,

Nikikumbuka Profesa mahili kabisa Mussa Assad CAG aligundua 1.5 trillion hazijulikani ziko wapi,akaja kuulizwa hadharani kabisa kwenye sherehe Fulani hivi,Tena mbele ya makamera na wahudhuriaji"eti CAG 1.5trillion ZIMEPOTEA?
CAG akajibu hazijapotea!,

Nikikumbuka kauli Kama NYINYI WATU WA KUSINI ATAKAE ANDAMANA KUDAI MAMBO YA KOROSHO NITAWAPIGA HADI SHANGAZI ZENU,

Nikikumbuka siku ile yule mbunge aliepigwa risasi nyingi Hadi mwili ukatoboka matundu mengi Kama chujio la Nazi,halafu hamna hata mmtu mmoja aliekamatwa Hadi leo,

Nikikumbuka wazee waheshimiwa Sana Wastaafu walijaribu kushauri Mambo Fulani kwa njia kukosoa,majibu waliyapata walikua wapole wote watatu kwa pamoja kwa Mara moja"NYNYI WAZEE WASTAAFU ACHENI KUWASHWAWASHWA"

Nikikumbuka kauli ngumu Kama hizi,"WALE WALIOISHI KAMA WAKO PEPONI KWANGU MIMI WATAISHI KAMA MASHETANI"
"MATAJIRI WALIOKUA WANACHEKEWA KWANGU MIMI WATASHUGHULIKIWA"


Aisee Mambo Ni mengi yaliyotokea miaka mitano iliuopita,nikikumbuka ntakuongezea.
Pole sana jamaa yangu. Hope hatakuwa kiongozi wa malaika kweli maana tukirudi kwa Mola atatuzuia mlangoni.
 
nilianzisha mada kama hii last few days Moderator wakafuta. sijui wanaingiwa na uoga gani au wanajaribu kulinda maslahi ya nani?. acheni watu wateme nyongo kuhusu marehemu, tupo wengi ambao tulikuwa hatuvutiwi na sera zake.
Tangu Yesu (Mungu nafsi ya pili) affufuke hakuna kiumbe aliyefufuka.
 
Back
Top Bottom