Nikikumbuka huwa naumia sana

Nikikumbuka huwa naumia sana

Inno laka

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Posts
1,616
Reaction score
585
Habari wana JF

Kila ikifika tarehe kama ya leo tarehe 8/7/ huwa nikikumbuka naumia sana. Mwaka 2012 niliachana na mpenzi wangu Suzie Mapesa, nilikaa muda mfupi sana nikaingia tena katika uhusiano mpya na Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ambaye mwanzoni sikumpenda ila siku zilivyozidi kwenda, moyo wangu ulizidi kumpenda.

Nilimpenda sana, ndio kwanza tu alikuwa kaajiriwa binti huyu alikuwa hana kitu, mimi nikawa nikimuhudumia kwa kila kitu, mwaka huo 2013 nilimtafutia chumba nikampangishia, nikamnunulia vitu vya ndani sofa, Tv, kitanda n.k.

Nilimuamini sana nikiamini huyu ndiye mke wangu mtarajiwa kumbe huyu mwanamke utafikiri ana pepo la ngono muda wote yupo busy na ma bwana hakuwa na mmoja, kumbe mimi Inno watu wananiona.

Ni ngumu kufahamu maana watu hushindwa jinsi ya kukueleza siku fahamu mienendo yake. Siku moja nilikuwa katika kijiwe kimoja cha boda boda, kuna boda boda aliniita kufika pale simu ya boda boda ikaita akapokea baada ya kukata yule boda akasema "huyu dada nae kazidi umalaya kila siku nampeleka kwa mabwana tofaut tofauti" wenzie wakamuuliza pale nani huyo, akasema "si yule mwalimu wakataja jina lake, mapigo ya moyo yalienda kasi, roho ikaniuma na furaha ikakata ghafla nikaondoka pale.

Sikuwa na raha kabisa chakula hakiendi mapenzi mabaya, nilipofanya uchunguzi niligundua ni tabia yake na kuna mwalimu mwenzie anatoka nae pale pale shuleni.

Nikamdanganya nasafiri na nitarudi baada ya wiki mbili, usiku wa tarehe 8.7.2013 nilienda kwake bila taarifa nikakuta njemba linakula mzigo nikaona nikigonga mimi hatofungua nikaita katoto ka pale jirani kakagonga takribani dk 20 hivi ndio akaja kufungua mlango.

Nikaingia ndani akashituka, nilipitiliza mpaka chumbani nikakuta njema imekaa kwenye kitanda ina boxer tu roho iliniuma sikufanya fujo nikaondoka zangu.

Nisingekuwa na uvumilivu na subira ningechukua maamuzi magumu pengine leo hii ningekua Jela.
 
Hao walimu sio waku kaa nao kaka...we piga then tembea...mm sinaga habari za kugandana...nikiwa na ugumu naita mmoja napiga maisha yanaendelea ...
 
Hao walimu sio waku kaa nao kaka...we piga then tembea...mm sinaga habari za kugandana...nikiwa na ugumu naita mmoja napiga maisha yanaendelea ...

Ndo tabia zao mkuu...
 
Ndo tabia zao mkuu...

Yas mkuu...ndio tabia zangu...
Ukiwa na demu wa permanent kwanza ni very costful ..hata mambo ya familia atakutegemea ww...unashuka kiuchumi

Pili..ukiwa na demu mmoja wa permanent unakosa chaguo la variouties...so unakosa kugundua utamu wa wengine
Na la mwisho kuepuka hayo wanayoita naumivu...mwanamke ni product kila mtu anataka haitumia nawe unatakiwa uifanye bithaa ukitumia una dest huko unatafuta nyingine maisha yanasonga...
 
Sawa mkuu hii formula yako nzuri..no kuumizwa
 
Back
Top Bottom