Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Wadau, bila shaka mwajua mpango wa serikali kujenga mji wa kisasa Kigamboni. Vikao kadhaa vimefnyika baina ya wakazi wa huko na Serikali lakini hakuna mwafaka ingawa serikali imeahidi fidia kubwa. Serikali pia imepiga marufuku wakazi wa huko kujenga nyumba kwa kuwa ni eneo la mradi. Haijulikani fidia yenyewe itatolewa lini na nina eneo langu nataka kujenga na ikumbukwe kuwa hakuna makubaliano rasmi baina ya wakazi na serikali.
Je, nikijenga itakuwaje? Ikiwa serikali itaamua kunibolea naweza kuishtaki?
Je, nikijenga itakuwaje? Ikiwa serikali itaamua kunibolea naweza kuishtaki?