mmmh mpaka nimelia jamani, story imenisisimua sana, lakini nimeshukuru mwisho wake umenifariji na ubarikiwe sana zaidi na zaidi (ukimsaidia yatima unamkopesha Mungu, malipo yapo tu hata kwa kizazi chako). Ki ukweli nakuunga mkono kuwa wema hauozi fanya wema kadri uwezavyo na hata kama hutalipwa wewe, inakua ni hazina kwa kizazi chako.. Pia kwa kuongezea hapo,mara nyingi kadri unavyoendelea kufanya mema kwa kadri ya uwezo wako, Mungu anakuepusha na mabaya mengi ,mengine unayaona kabisa mengine huyaoni.. mimi binafsi nimekua shahidi wa haya ninayo yazungumza. Vivyo hivyo hata ubaya.. tena ubaya huwa unarudi faster hata unaweza ukashangaa hata mwaka haujaisha.. limekupata jambo ukashangaa why??? ukijaribu ku recall back utaweza kuona pengine kunajambo fulani baya ulimfanyia mtu .. afu yule mtu hakusema na wewe.. analia na Mungu tu.. Haya yapo sana kwenye maofisi yetu na mimi pia ni mshahidi wa hayo. So ndugu zangu, kama unaona huwezi kumtendea mtu jema bora umwache tu kuliko kumtendea baya.. litakurudia tu hata kama ni ten years to come.
Ardhi ni tajiri sana kwani inameza kila kitu,bonge la story,unaweza kuwapa wataalam wakatengeneza kitabu au movie moja ya ukweli sana.Fundisho hapa ni kuwa wema hauozi na binadamu tunajua tulikotoka ila tuendako hatujui.
Mtambuzi, hapa nilipo hata mimi machozi yananitoka, secretary wangu ananishangaa na ananiletea maji huku nikiandika, niko naye live ananiuliza kama ningependa kikombe cha kahawa,,,simjibu kitu " babangu kuna shida? Tina ananiuliza kwa sauti ya upole....mke wangu anapiga simu sasa ngoja nipokee, Ila ningependa kuwa na namba zako MCHAMBUZI, nikupigie sasa hivi? Mke wangu anapiga tena, sasa napokea!!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.