Ennie
JF-Expert Member
- Jan 15, 2011
- 7,137
- 4,122
Dah...nimejikuta na mimi machozi yananilengalenga! Kuna watu wanajua kusimulia.
yaani mimi mwili wote vinyweleo vimesimama. Kweli WEMA HAUOZI!
Dah...nimejikuta na mimi machozi yananilengalenga! Kuna watu wanajua kusimulia.
pitisha na michango mtambuzi tutachangia,na litaingia tena kwenye jamii,niliwahi kupata counsceling session moja hivi kutoka kwa Munga,kwa kweli ilibadilisha sana maisha yangu na ya mume wangu.nikisoma post zako huwa nashindwa kujizuia kukumbuka upole na ukarimu wa yule mtu!udongo hula vizuri jamani!R.I.P MUNGA.utaendelea kuishi mawazoni mwetu milele
rest in peace MUNGA TEHENAN!ahsante sana mtambuzi kwa kufanya huyu jamaa aishi ,alikuwa na mtazamo tofauti sana juu ya maisha na nguvu zilizo juu wa uwezo wetu wanadamu!
Ni kweli, hata yeye alilitambua hilo kwamba ipo siku roho yake itaachana na mwili na ndio maana alianzisha madarasa ya kufundisha maarifa hayo ambapo sisi wanafunzi wake tunaendeleza kile alichotuachia.... Madarasa hayo kwa sasa yapo Tabata Kimanga.
Kwa sasa, ninachofanya ni kuendelea kuweka makala mbalimbali za maarifa hayo kupitia hapa JF kwa wale ambao hawana muda wa kuhudhuria madarasa yetu kule Tabata.
Nakumbuka katika makala zake za mwisho mwisho kabla hajafariki Hayati Munga Tehenan aliwahi kuandika hivi:
"Inaonyesha wazi kwamba, binadamu bado ni mjinga sana juu ya maisha yake. Mwili, mwili ni nini, na hadi wapi? Kama mwili ungekuwa na maana sana, baada ya mtu kufariki asingekimbizwa mochuari, usingepakwa asali au usingechomwa sindano ili usiharibike na kuleta usumbufu wa harufu na maradhi. Mwili siyo mimi wala wewe.
Mwili haujawahi kuwa mwenye mwili na hautakuja kuwa. Mwili ni kama tochi tu, ambayo umeiazima ili uweze kukusaidia kufika kijiji cha pili, kutokana na giza na njia ya uchochoro ambayo unatakiwa kuipita ili kufika kijiji hicho cha pili Mwili ni kifaa na siyo wewe, bali wewe unakitumia kifaa hicho. Binadamu anajibainisha kwenye maisha haya ya hapa duniani kupitia mwili wake, lakini yeye siyo mwili. Mwili ni ubainisho, ni chombo cha kutumika kwa kusudi la kidunia tu.
Baada ya muda mwili hukoma kuwepo, hujimaliza wenyewe au kumalizwa, ili binadamu amudu kuingia hatua nyingine ya maisha ambayo haitumii au haihitaji mwili. Tangu ulipozaliwa umeoneshwa na kufundishwa kwamba, wewe ni mwili kwa njia zote. Akili yako imeshika kutu kwa kuamini kwamba, mwili ni wewe na wewe ni mwili. Huna uwezo tena wa kuuona ukweli, kwa sababu vipimo vyako vyote kuhusu maisha vinaishia kwenye akili, ambayo nayo pia haikuhusu, siyo yako umepachikwa tu. Kwa ujinga huu wa kutojua mwili ni nini na sisi ni nani, ndipo ambapo tunaingia kwenye ujinga wa kuendeshwa na miili yetu, hisia zetu na akili. Kila mmoja anaamini kwamba, mwili wake ukipotea, ukishindwa kutumika, yaani akifa, basi huo ndio mwisho wake.
Kama hiyo ni kweli, ina maana binadamu hana maana kabisa, ni upuuzi usiofaa kuelezewa! Yaani binadamu amekuwepo ili awepo kwa mwezi mmoja, miaka kumi, hamsini, sabini, tisini au mia tu. Halafu baada ya hapo basi. Huu ni uongo mkubwa sana, unaoweza kukubaliwa na akili makapi ya kulishwa tu! Anayetafakari zaidi kidogo, atabaini kwamba, mwili ni mwili tu, ni kasha tu. Ni kasha ambalo muda wake wa kutumika ukiisha mtumiaji au (wewe) analiacha kwa sababu haliwezi kukidhi kile kinachohitajika hapa duniani. Mtumiaji anachukua kingine ambacho kinakidhi wakati huo (baada ya kifo).
Kwa hiyo, binadamu hafi bali mwili ndiyo unaofikia ukomo wa muda wake wa matumizi kwa sababu mbalimbali. Anapokufa John au Hamisi, haina tofauti. Anapokufa mkulima hohehahe au tajiri kuliko wote duniani, pia haina tofauti. Wote wanapita kwenye hatua ya mabadiliko, ambapo wanaacha matumizi ya kifaa kilichokuwa ndicho pekee kinachoweza kuwabainisha na wengine hapa duniani na kuchukuwa kingine ambacho hakiwezi kuwabainisha tena na wale wenye miili bado. Anapokufa John au Hamisi, haijalishi kama amezikwa kwa jeneza la dhahabu na mizinga 100 au kwa masululu butu na kaniki."
Was that his name?[/QUOTE
ndio MUNGA TEHENAN,ndio lilikuwa jina la mmiliki wa gazeti la JITAMBUE

dah, imenigusa sana. naomba nikiri kuwa me ni mvivu wa kusoma story ndefu hapa jf kwan natumia simu. ila inapofika kwenye story za Mtambuzi huwa sina budi kusoma. na huwa najifunza mengi sana kupitia story zake!