Nikaona maiti zao..!

Hata mimi nishawahi kukutana live na 'wema wa jana' siku nyingine kabisa
wema huwa hauozi
 
Yes. Niliisoma hii kwenye gazeti la JITAMBUE. Ni ajabu umeitunza vizuri. Hongera na asante kwa stori hii muhimu.
 
Tengeneza kitabu na ukipe jina la "Uchawi wa maisha" kisheheni stori zako zenye visa vifupi yenye mafunzo makali sana.Kwa kweli Mtambuzi unafanya uinjilishaji wenyewe achana na hule wa kumtaja Yesu na kidondosha watu madhabahuni kumbe mchungaji ni Freemason.
 
Imekugusa eh..............!
Hongera Mtambuzi yaani ni juzi tu Mke wangu kipenzi kaenda kwao kusalimia ni nje ya Mkoa katika kubeba mkoba wake na mwanangu akasahau pochi iliyokuwa na Pesa yote na ya nauli pamoja na Simu
kwa vile magari ni mengi akapanda mini-Bus kufika ndani akakutana na Mzee wa miaka zaidi ya 65 aliyempisha kiti kwa ajili ya Heshima ya kufahamiana na mimi na akamlipia nauli. Baada ya nusu-saa mke wangu akafika na kuagana nae.
Mara akagundua kuwa huenda kaibiwa akaipiga simu yake na mm nikamjibu kuwa kaiacha nyumbani ana mawazo gani?
wakati wa kurudi alipewa nauli na shangazi yake kuja kunihadithia nilitamani kulia kwani huyo Mzee akili zake haziko sawa na kila siku nilikuwa namsaidia.
Leo nimelia zaidi kunifananishia stori hii na ya huyu Mzee niliyekuwa namsaidia kila siku, Mke wangu makonda wasingeamini km hana Nauli wangemshusha popote na mwanangu, huyu Mzee nikimuona sijui nitamshukuruje kwa kitendo alichokifanya bila kuelewa kuwa Wife hana hata senti
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka nilikuwa mpenzi sana wa gazeti la Jitambue japo nilikuwa bado sijakomaa vyema, nilipokuwa nasoma wakati ule nilisoma kwa kuvutiwa na habari na simulizi za kusisimua wakati huo huo nilikuwa nahangaika kweli kujitambua na kutafuta nafasi yangu duniani.
Niseme unconsciously Jitambue limehusika sana kunijenga katika mtu niliye sasa....
Asante Mtambuzi na wengine hapa JF kwa kuendelea kufanya tuzidi kujitambua kupitia mabandiko yenu

Elizabeth Dominic, bora wewe unajitambua...mimi jana nimegundua bado sijitambui.
 
Last edited by a moderator:
hii story imenifanya hadi niingie humu ndani leo, Hakika wema hauozi, asante sana Mtambuzi endelea kutuelimisha na kuinjilisha mkuu, Mwenyezi Mungu azidi kukupa hekima na maarifa
 
Dah mkuu Mtambuzi hiz story aise zina simanzi sana mkuu
Ni mambo ambayo sometime unaamini kuna nguvu za ziada au kuna Mungu ambae huwa anaongoza kitu fulani kutokea
Kweli inasikitisha ila ule msemo wa tenda wema uende zako usingojee shukrani huwa unatimilika sana
Shukrani au matokeo ya wema wako utayaona tuu bila hata kuambiwa asante na yule aliyefanyiwa wema huo
Asante sana Mkuu Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Thanks mtambuzi, kweli unatukumbushia gazeti la Jitambue na tutafurahi zaidi kama unavyosema utaliibua upya, yaani utafanya jambo la maana sana.
Story is very touching kwakweli japo jamaa alitaka kumtimua yule kijana bt lililopangwa na Mungu katu binadamu hawezi likwepa
 
Mmmh...kumbe nilikuwa nakosa uhondo wa story ya kuhuzunisha mana kila cku nilikuwa naipita post nikidhani itakuwa haina mashiko,thanks mtambuzi umenitiririsha chozi mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom