...Nikamwambia nenda kwa Polepole akukopeshe

...Nikamwambia nenda kwa Polepole akukopeshe

Huyu ni rafiki yangu wa kitambo. Alikuwa mwanachadema mzuri na mpigania haki kweli kweli. Basi likaja lile wimbi la wapinzani kununuliwa na ccm akasepea ccm kuunga juhudi. Nikawa namcheki tu

Uchaguzi umekuja akawa mstari wa mbele kuikandia chadema na kuipaka matope wakati ndiyo iliyomtoa jalalani. Akawa mwanaccm machachari kuliko hata wenye chama chao. Nikawa namcheki tu

Basi uchaguzi umeisha anakuja kwangu analialia alivyofulia, maisha yalivyomuwia magumu maana wajumbe walimkatilia mbali, eti anataka nimkopeshe pesa walau akawanunulie watoto ugali

Sikumchelewesha nikampa makavu laivu, nikamwambia umeshiriki kuwadhurumu watanzania na kuikana kweli kisa vipande vya fedha

Umetema big g kwa karanga za kuonjeshwa sasa nenda kwa hao kina Magu na Polepole wakukopeshe. Hata mwezi baada ya uchaguzi bado ushaanza kulia njaa? Akapikie watoto fly over na bombardier...pumbav

Nikamwambia sikukopeshi hata mia shubaamit na urafiki ufe

Dawa ya hawa wasaliti wa haki ni kuwafungia vioo. Walidhani watakuwa na bei zao special za cement, sukari nk, kumbe tunakuja kusota nao hukuhuku mtaani
Akili zako ni robo kilo
 
Kushindwa kumsaidia mwenzio kwa itikadi za kisiasa,ni ujinga usiopimika
 
Safi sana mkuu hata mimi kuna kenge mmoja namsubiri aingie kwenye kumi na nane nimmalize
Angalia usije ukaingia wwe kwenye kumi na nane zake!! Maisha ni Kama Kende za Mbuzi zinapishana kadri Mbuzi anavyo zidi kutembea!!
 
Wewe jamaa inaonekana hata kama ni mshabiki wa simba basi huli sahani moja na yanga. Mambo ya siasa za uchaguzi unaleta mpaka kwnye maisha halisi? Umefeli sana
 
Kwa ushauri wangu,naomba turidhiane,,hakuna sababu ya kuchukiana,uchaguzi ushaisha,sasa tuchape kazi
 
Wewe ni lofa tu nashawishika kuamini hata hela huna maana mawazo yako ni ya kimasikini tu
 
Tusifike Huko,Zanzibar Haya Mambo Wakati Fulani Yaliwapa Tabu Sana Ikafikia Hatua Mbaya Mno
Mwanachama Wa CUF Alikuwa Hawezi Kumzika Wa CCM
Pia Ilikuwa Kuoa/Kuolea Na Mtu Wa Chama Tofauti Haiwezekani.

Mpaka Wakatafuta Maridhiano
Siyo zanzibar tu, hata Mtama jimbo la nape ukawa na CCM wametengana kabisa, lile jimbo ni gumu mnao ndio maana nape anamsumbua sana jamaa wa Chadema
 
Kuna kenge mwingine alikuwa kila siku anapost madudu ya ccm nilimpa onyo hakunielewa, sasa ikawa kuna kazi ya muda mfupi kama masaa 20 tupate 3m ila mimi ndio naiunganisha, kwa hasira nikaipiga chini tukose wote, jamaa mpaka sasa haamini na hana kitu
Wwe una Akili Kama za Lissu,yeye kukosa kwake Uraisi anataka na Tanzania yote ipotee ili tukose wote, kumbe yeye anakula zake Bata huko Ubelgiji!!
 
Kuna mjumbe mmoja aliniomba kama nina viatu vilivyoisha nikapita kama simuoni vile. Mungu anisamehe hivi sasa hata maskini siwapi kitu nahisi ni ccm.
 
Kitu pekee kinachoumiza wa tanzania ni unafiki na hofu na woga wa maisha halafu kuna muda wanajikuta na hekima
 
Akili zako ni robo kilo
Hivi nyie akili mnatumia nini kuzipima haya itoshe kusema wote mnao support Ccm mna akili sana halafu mtu hafundishwi jinsi ya kumfunza mtu acha wafunzane ili wakati mwingine ajifunze kuchakata mambo .
 
Huyu ni rafiki yangu wa kitambo. Alikuwa Mwana-CHADEMAmzuri na mpigania haki kweli kweli. Basi likaja lile wimbi la wapinzani kununuliwa na CCM akasepea ccm kuunga juhudi. Nikawa namcheki tu

Uchaguzi umekuja akawa mstari wa mbele kuikandia chadema na kuipaka matope wakati ndiyo iliyomtoa jalalani. Akawa MwanaCCM machachari kuliko hata wenye chama chao. Nikawa namcheki tu

Basi uchaguzi umeisha anakuja kwangu analialia alivyofulia, maisha yalivyomuwia magumu maana wajumbe walimkatilia mbali, eti anataka nimkopeshe pesa walau akawanunulie Watoto Ugali

Sikumchelewesha nikampa makavu laivu, nikamwambia umeshiriki kuwadhurumu watanzania na kuikana kweli kisa vipande vya fedha

Umetema Big G kwa karanga za kuonjeshwa sasa nenda kwa hao kina Magu na Polepole wakukopeshe. Hata mwezi baada ya uchaguzi bado ushaanza kulia njaa? Akapikie Watoto Fly Over na Bombardier.

Nikamwambia sikukopeshi hata mia shubaamit na urafiki ufe

Dawa ya hawa wasaliti wa haki ni kuwafungia vioo. Walidhani watakuwa na bei zao special za cement, sukari nk, kumbe tunakuja kusota nao hukuhuku mtaani
Mwambie auze nchi kama Lissu labda na yeye atapelekwa kupakatwa Ubelgiji?
 
Back
Top Bottom