YESU NI MWEMA..
Nimetafakari habari zako nami
nashindwa kuelewa kabisa
Binadamu angenipa neema kesho
angechoka kunipa zaidi
Lakini wewe hauna kikomo, wala mvua
yako haina majira
Bwana, wanyesha mvua, Bwana, kwa
walio jangwani
Bwana, wawasha jua, Bwana, mpaka
baharini
Kweli Bwana wewe ni mwema sana
Nitasimulia miji, Yesu ni mwema, Yesu
ni mwema
Nitahubiri vijijini, Yesu ni mwema Yesu
ni mwema
Nitayafafanua haya –
Watu wote wapate kuyajua-
Nitasimulia nchi –
1. Niliwaza kwa ubinadamu mpaka
mwisho wa kufikiri
Ukataka nijipe moyo, nisihofu
kitu
Kwa kuwa humtupi
anayekutumainia
Ukataka nijipe moyo, nisihofu
kitu, kamwe
2. Uzoefu wa mapito haya
ukaninyima usingizi . . .
Kanuni za dunia zikavunja
matumaini . . .
3. Giza lilipotanda mchana
likanifunika usoni . . .
Nikapiga kelele hofu kuu
ikanisonga . . .
< h i t i m i s h o >
[t|b] Naimba he he, naimba leo
Naimba he he, naimba mimi
Ulijua wazi kwamba mimi
sikuwa nastahili,
Kwa sababu mimi mdhaifu mwili
na roho
Ukaruhusu nifanikiwe juhudi
zangu
Makusudi ili nione ukuu wako
Ndugu wanipende, jamaa
waniheshimu
Marafiki wanijali, wanisaidie
Ndiyo maana leo, mimi
nakurudishia;
[w] Utukufu ni wako milele
Sifa heshima ni vyako daima
Wewe peke yako unastahili
Usifiwe na uhimidiwe!
Nakushukuru Bwana, kwa kuwa
umeniona asante
Nakushukuru Bwana . . .
Nakupa utukufu . . .
Milele na milele . . .
Nakushukuru Bwana . . .
by B.MUKASA
Cc
charminglady Kongosho Asprin