Baba Mtakatifu Francisco wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana??????????? kwenye Maadhimisho ya Siku kuu ya Watakatifu Petro na Paulo, miamba wa imani anasema, hii pia ni Siku kuu ya Jimbo kuu la Roma ambalo limejengekwa katika ushuhuda wa kifo dini cha Mitume hawa wawili???????
Ndugu zangu kauli hii ya baba mtakatifu haiwezi kukubalika bila kufanyiwa kazi na utafiti wa hali ya juu,anazungumzia Petro tunayemjua aliyekuwa Mwanafunzi wa Yesu au Petro mwingine?na huyu mtume Paulo anayezungumziwa ni huyu tunayemjua au mwingine?
Hivi kanisa la Roma lilianzishwa lini?na nani hasa mwanzilishi?huo uzushi wa kusema ni mtume Petro na Paulo haukubaliki hata kidogo
Mama Maria ameingizwaje hapo?katika kusoma kwangu Biblia sijawahi kuona mahali Yesu ameongea kuhusu Mama Maria ambaye alikuwa Mama yake Yesu,wala Biblia haijaelezea kwa kina historia ya huyu Mama zaidi ya kumshukuru kwa kutuzalia Mwokozi
Eti Kanisa limejengwa kwenye Mathayo 16:18,nami nakuambia wewe ndiye Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu wala milango ya kuzima haitalishinda???????
Yesu aliongea kwa mafumbo kamwe kanisa hai la Mungu haliwezi kujengwa juu ya Binadamu,aliongea parable,
Sijasoma popote pale Yesu aliposema mkitaka maombi yenu yafike Mbinguni mwombeni Mama yangu ayalete???huo ni ujinga ambao hauvumiliki,nataka mjue kwamba ujinga ni dhambi,
Mkitaka kusali semeni hivi,Baba yetu uliye Mbinguni,jina lako litukuzwe,Ufalme wako uje,mapenzi yako yatimizwe hapa Duniani kama huko Mbinguni,utupe leo riziki yetu,utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyosamehe waliotukosea,usitutie majaribuni bali utuoke na Yule mwovu,kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu hata milele Amin!!!!
Je kuna Mama Maria hapo?ndivyo Petro alivyofundishwa ,je mnataka kusema Petro alipotoka na kufundisha mambo tofauti na aliyofundishwa?petro asingeweza kugeuza aliyofundishwa na Yesu na kuchomeka majina na taratibu ambazo hakupokea kutoka kwa master wake
Mtume Paulo tunajua background yake alipokuwa njiani kuelekea Damasks kuwakamata Wakristo walioamini akatokewa na Yesu njiani na kupigwa upofu,kisha akapewa majukumu ya kufanya,katika majukumu sijaona jina la Mama Maria hapo
Ni nini hasa kipo nyuma ya kanisa la Roma?na kwa nini wamebadili Biblia inayosomwa na makanisa yote na kubadili baadhi ya vifungu,
Someni kitabu cha Matendo ya Mitume,soma chote na rudia mara kadhaa utajua jinsi Kanisa lilivyoanzishwa,wakati wa kufata mkumbo umepita ndugu zangu,kaa chini tafakari kama kweli imani unayofata na njia unayofata ya kumwabudu Mungu ni sahihi,hata kama umezaliwa ndani ya kanisa la Roma una haki ya kujiuliza kama kweli upo mahali panapostahili au la!!!!!