Nikajifanya kutaka ujiko, demu akaniletea noma……….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikajifanya kutaka ujiko, demu akaniletea noma……….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 27, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Katika watu ambao wamepambana na misukosuko hapa jijini, naweza kusema mimi ni mmoja wao. Na labda niseme tu kwamba tabia yangu ya kiherehere na kupenda ujiko, iliniletea kasheshe nyingi sana kiasi kwamba mpaka leo hii nikikumbuka mapito niliyopitia, wakati mwingine huwa nacheka mwenyewe. Nisiwapotezee muda, ngojeni niwasimulie hili kasheshe nililolipata miaka ya tisini.

  Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nakaa kwa dada yangu maeneo ya Mwananyamala, ambaye alinichukua kwa mjomba wangu niliyekuwa nikiishi naye maeneo ya Tandale. Lengo lilikuwa ni kunitafutia kozi yoyote ili niweze kujimudu, kwani matokeo yangu ya kidato cha nne niliangukia pua.

  Siku nilipokutana na dhahama hiyo ilikuwa ni kipindi cha sikukuu ya Pasaka. Siku hiyo nilitoka nyumbani kwa dada yangu Mwananyamala kwenda kwa rafiki yangu aishiye maeneo ya Kinondoni. Huyu jamaa alikuwa ni rafiki yangu ambaye nilikutana naye maeneo ya club moja maarufu maeneo ya Mwanayamala iliyokuwa ikijulikana kama Mwanayamala Club Villa. Nilikutana naye hapo wakati wa mashindano ya disco, kipindi hicho ule mtindo wa break dance ndio ulikuwa umeshika kasi, na mimi na yeye tulikuwa ni miongoni mwa vijana tulioingia fainali, wakati huo nilikuwa naweza kujinyonga hasa kwa mtindo huo wa break dance na ndio chanzo cha kujuana na huyo kijana.

  Na yeye kama mimi alikuwa ameangukia pua kidato cha nne, lakini mwenzangu alikuwa ametafutiwa shule ya kulipia huko Moshi ili aendelee na kidato cha tano. Huyu mwenzangu wazazi wake walikuwa wanajimudu kidogo, kwa hiyo mara nyingi tukienda kujirusha jamaa ndiye alikuwa mfadhili wangu.

  Siku hiyo, tuliamua kwenda beach ambapo jamaa yangu alikuwa ametafuta wasichana wawili wa kujirusha nao. Ile jioni tulipokutana jamaa yangu alinambia kwamba itabidi nichukue msichana mmoja lakini akaninong'oneza , ‘inabidi ujifanye mtoto wa mtu mkubwa, maana demu mwenyewe ni mtoto wa kigogo.'

  Mimi bila kumuuliza ni mtoto wa nani nilichangamkia ‘tenda.' Jamaa hakuniangusha, alinipatia shilingi 6,000 na mimi nilikuwa na kama 1,200. Kwa kipindi kile hizo zilikuwa ni hela nyingi za kutangazia ujiko.

  Basi jamaa akamchukua demu wake na mimi nikamchukua demu wangu, tukaenda kila mtu njia yake. Tulifika kwenye kona moja tukakaa na kuagiza vinywaji, kisha tukaanza kupiga stori. Yule msichana akaniuliza jina langu na ninaishi wapi, yaani akitaka kunijua vema.

  Na mimi kwa kiherehere changu na kupenda ujiko, nikatafuta jibu la haraka haraka, Nilimtaja kigogo mmoja ambaye wakati ule alikuwa ni waziri kwamba ndiye baba yangu. Yule msichana aliniambia, ‘nakuuliza kweli, siyo mzaha.' Lakini mimi kwa akili yangu ya kifisi maji niliendelea kusisitiza kwamba yule kigogo ndiye baba yangu. ' Am very serious na wala sitanii yule ndiye baba yangu kabisaa' niliweka msisitizo wa madai yangu kwa kukoleza na kiingereza changu cha kuombea maji.

  Yule msichana alionekana kukereka na alisema, ‘sasa mbona sikufahamu, wakati huyo mzee ni baba yangu mdogo na ninaishi kwake.' Kwanza nilidhani ni mzaha, lakini aliponikazia macho na kuzidi kuniuliza, nilibabaika kidogo na kujikuta nikianza kuchanganyikiwa. Lakini akili yangu ikafanya kazi harakaharaka na kupata jibu la kuua soo……………… Si mnajua wanaume hawakubali kushindwa kirahisi, hasa na mwanamke!

  Nikamwambia kwamba, huyo mzee ni mlezi wangu, ndiye anayenilea, ingawa ninaishi na mama yangu. Yule binti ambaye alionekana kunitazama usoni kwa makini kama anasoma mawazo yangu, alinitupia swali la kushtukiza. ‘je unawajua watoto wake?'

  Nilijikuta naropoka, ‘ndiyo nawafahamu watoto wote wa yule mzee.' Yule binti ambaye nadhani amesomea saikolojia ya kuwabaini watu waongo, aliniuliza kuhusu mtoto wa yule mzee aliyefariki miezi miwili iliyopita. Kwa kweli sikuwa najua chochote, nikabaki nimeduwaa nisijue nijibu nini.

  Yule msichana alianza kunituhumu kwa kujikweza. ‘kama umetoka familia masikini si useme tu, kwani mapenzi unadhani ni lazima mtu awe na fedha au umaarufu!' Alianza kunisomea, na kwa sababu alikuwa ameshapata moja moto moja baridi, aliongea kwa kelele kubwa bila staha kama mwanamke. Ilibidi jamaa yangu ambaye hakuwa mbali na tulipo waje na mpenzi wake ili kujua kulikoni.

  Yule binti alimwambia jamaa yangu. ‘Nini bwana unanipa mshamba huyu, sijui katokea Mbwinde huko, anajifanya kujikweeza na kunibania pua. Anataka ukubwa wa kulazimisha, mwambie aache hizo.'

  Jamaa yangu alinivuta kando na kuniuliza kulikoni. Nilipomsimulia, alihamaki na kushika mdomo. ‘Ah umeharibu, huyu binti, huyo ni baba yake mdogo na amemlea tangu akiwa mdogo.'

  Kama mjuavyo watu wa Dar hawataki kupitwa na jambo, walijisogeza karibu ili kujua sababu ya ile tafrani, na yule binti ambaye alikuwa anaongea kama cherehani, aliendelea kunipaka kishenzi, na kila kitu kikawa hadharani…………….

  Watu walikuwa wakiniangalia kwa huruma na wengine wakinicheka kwa ushamba wangu. Uso wangu ulisawajika kwa tahayari nikawa kama vile nimeachwa uchi……………

  Najua mnataka kujua kilichojiri baada ya pale. Kwa bahati mbaya nimepoteza kumbukumbu. Kwani nyie mnadhani ni kitu gani kiliendelea………………tafuteni jibu………………………LOL
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaa vituko vya ujana hivyo!
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ujana maji ya moto kaka..................
  Hujambo lakini, Ni muda sasa hatuonani................Kulikoni kaka..................LOL
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndefu hiyo inachosha kusoma nitairudia baadae
   
 5. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Dooh bonge la sooo, kumbe alikujua mshambaaaeeee
   
 6. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hahahahaha!aiseee,ashukuriwe mama kwa kukubali ukamuoa maana cjui ungeendelea kuutafuta huo utukufu kwa style zako za magumaishi ungeishiaga jela cku moja lol!hahahaha ckupatii picha kiherehere na micfa yote ilivokushuka!kumbe baba 4m foo ulipata mwanaasha!
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu na wewe umerithi kiherehere cha baba yako na ndio maana hata shule inakushinda sasa, kazi kusingiziz etu waalimu wamegoma........LOL
  Ukiona nimeweka maneno humu JF pita kimya kimya, la sivyooo.........................
   
 8. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,581
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  takwimu zinaonyesha miaka ya tisini ndio ulipata misukosuko mingi zaidi kuliko elfumbili, ..pole! Kweli ujana maji ya moto!
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Miaka ya tisini ndio nilikuwa nimeanza kuujua mji na ujana ulikuwa umeanza kukolea..............Mambo ya totoz na vibinti ndio ilikuwa mwake. Nilikuwa najipambanua kama mwanaume rijali na shababi mwenye siha nzuri..............
   
 10. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  ujana maji ya moto
   
 11. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tatizo baba yangu huwa hujipangi,yani ww likishakuwa ni swala la utukufu unakurupuka tu wala hutengenezi majibu ya maswa yanayoweza kujitokeza!!
  Pole baba,hii ndio ya mwisho nitakua napita kimya kimya hahahaha!
   
 12. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 997
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Vituko vyako vinaonesha ulikuwa hujatulia sana,vp watoto wako wametulia??maanake hata huwezi kuwalaumu kama baba mwenyewe alikuwa hivi!! Duh pole sana!!
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,578
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Hivi mtambuzi wewe ulifaa uitwe Toto tundu maana vituko vyako mmh
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huyu mwanangu aitwae NGADU, nahisi kama amerithi hiki kipaji changu, maana ndio kwanza ana miaka 9 lakini namuona jinsi anavyopigia misele mademu ile kinomanoma mpaka naogopa kwa kweli.....................LOL
   
 15. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  ulitoka nduki kali sana nusura umwage vinywaji vya watu baada ya kuivagaa meza yao. lol
  nice stpry Mtambuzi..
   
 16. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dah mtambuzi naona unacopy na kupaste kwenye Jitambue,hapa ndio nammiss sana Mr Munga Tehenan,
   
 17. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Hahahah.......mtambuzi bana yaani kama vile nakuona!!! Lol
   
 18. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mtambuzi pamoja na kwamba hii mikasa huwa unasema sio yote imekupata wewe ila inaelekea hata wewe mwenyewe enzi hizo ulikuwa moto chini! Ni experience nzuri lkn
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa yako tu ni kwamba, mimi nilikuwa ni mmoja wa waandishi wa visa hivi katika hilo gazeti.............................
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  mmmmmmmmmmmmm
   
Loading...