Nisikukatishe tamaa ila majuu hata ajira za mabox hakuna, labda ukafanye kazi za kuzibua mifeleji ya maji machafu, maana hata kazi za hovyo wenyewe wanafanya siku hizi..Goodluck.
Ndugu sidhani kama napaswa kukushirikisha mambo mengi yahusuyo faragaha yangu ila kwa taarifa tu mimi ni kijana umri miaka 27.
Lengo kubwa la mimi kutaka kwenda ugahibuni si kwa ajili ya kupata fedha na mali nyingi saaana, hapana!! Nina authentic passion ya kutaka kuishi na jamii yangu tofauti na hapa nyumbani lengo likiwa ni kusikia sauti mpya, lugha mpya, Tamaduni mpya, Imani mpya n.k hii ndio tafsri yangu ya mimi kuwa na furaha ikizingatiwa kila mtu ana tafsri yake linapokuja suala la kuwa na furaha, amani na mafanikio maishani. Mfano kuna baadhi ya makabila hawahitaji kuwa na fedha nyiingi kuwa na furaha na mafanikio maishani bali ng'ombe pekee zinatosha kuwapa furaha na mafanikio.
Sijui umenipata mkuu.
Humble African... nina wasiwasi sana kama kweli hiyo "passion" yako itakamilika ukienda huko "Mashariki ya Mbali" kwa kiwango cha pesa ulichonacho sasa. Umeshaambiwa tiketi tu peke yake ni $2000 na chenchi utabakiwa $2500, lakini pia kule hakuna vijiwe vya kukaa idle na kupiga soga kama huku kwetu ili usikie "sauti mpya na lugha mpya"...
hakuna ngoma za mdundiko barabarani kama huku kwetu ili ujifunze "tamaduni mpya" lakini hata makanisa ama misikiti yao haiingiliki kama ya huku kwetu ili ujifunze "ïmani mpya".
Maana yangu hapa ni kwamba maisha ya "Mashariki ya Mbali" ni gharama mwanzo mwisho. Lolote utakalotaka lifanya litakugharimu. sasa kwa hela uliyonayo ni ndogo sana (achilia mbali maandalizi yoote na mahitaji mengine muhimu mfano nguo za baridi, nauli, visa, n.k) utajikuta umebaki na labda $1500. Hakika furaha unayoitafuta haitapatikana na mwishowe itakuwa karaha..
Ushauri:
Baki nyumbani (Tz), zungusha hiyo hela ili iongezeke na hatimaye ukaifuate "passion" yako.
Habari gani wangugu?
Mimi ni kijana ambae nimehitimu shahada hivi punde, miongoni mwa vitu ninavyopenda saana ni kusafiri na kuishi mashariki ya mbali kabisa tofauti na nyumbani nikakutane na watu wapya, sauti mpya, tamaduni mpya, Lugha mpya n.k
Nimefanya shughuli zangu kwa jitihada na juhudi kubwa na hadi sasa nina kiasi cha tsh mil 7/= ningependa kufika New zealand, Canada, Australia, Finland, US..
Hivyo kwa waliotayari kutoa mualiko au msaada wa kufika majuu karibuni, Na wale washauri pia karibuni, na wale haters nawahitaji sana kwa changamoto.
Karibuni!!
Kaka mimi nipo Nchi moja kati ya ulizozitaja, nimeanza mwaka wa pili sasa,nimekuja kusoma, ajira sio kama unavyodhania,ni ngumu kweli kweli,si rasmi wala zisizo rasmi,hapa naskilizia nimalize shule nirudi faster,kisheria nchi nyingi ili upate uhalali wa kuishi mfano hapa nilipo either uje kwa gia ya kusoma au uwe umeshapata ajira na utoe details za mwajiri wako huku,pia uonyeshe benki statement yenye salio lisilopungua dola 15,000.
Ukija kwa gia ya kusoma ndio unatakiwa uwe na mshiko mrefu zaidi maana certificate tu ya mwaka mmoja itakucost si chini ya dola 10000
Bado hujalipa kodi ya nyumba, hapa napoishi ni bei ya chini dola 135 kwa wiki na ni chumba sio nyumba nzima.
Bado hujala bado hujalipa nauli! Komaa na bongo tengeneza pesa ukienda huko unakotaka uende kutembea na kurudi, kuna wabongo wapo huku zaidi ya miaka 10 hakuna cha maana wamefanya, mafanikio makubwa kununua magari tu ambayo yapo ya bei rahisi.
Cc. Nyani Ngabu
Umepotea sanaaaaaKabisaaaaaaa. Kama hana papers sheriff hana mzaha
Kutokana na hali ya uchumi ulivyo duniani kaka kazi unayo, maana kuna nchi ulizotaja hapo juu kama Canada, Australia, New Zealand zimeanza kunung'unika kumlipa Queen Elizabeth kila mwaka, kama kodi fulani au upkeep zake! Mambo yamebana kote kote, kwanza ufike huko, pili utafute kibali cha kazi, tatu uzoee maisha na tamaduni zao, hapo ushakata miaka 3 au 4, tayari kamgonga kashaanza kupinda, haya unaendelea weee, ikifika 15yrs ukijiangalia una vi raba mtoni, vi tshirts na vi jeans, na makoti mazito kibao sababu ya baridi, home sana sana wapeleka vipicha picha na vihela vya hapa na pale, ujakaa sawa 20yrs! Kibanda home huna wala nini, na kamgongo kanauma kishenzi, hatari aise, waulize wajuzi watakwambia...
Kwa 7m/- mbona waanzisha biashara ya chakula, kilimo kidogo fresh tu?! Ila uamuzi juu yako mkuu..
Unataka kwenda kuishi Nchi za Scandnavia kwa miaka kadhaa na mfukoni una Milioni 7, endelea kuota kijana!!
Hivi kabla ya kutoa hizi comments zenu mmesoma hii thread imeandikwa lini?Ukibaki hapa nchini, kwa nguvu na juhudi hizo, baada ya miaka miwili utakuwa na M50 kibindoni.
Ndiyo! Mleta mada anataka aende ughaibuni kufanya kazi za kubeba box. Sasa ndio namshauri abaki hapa hapa nchini maana kama kaweza kuzichanga M7 kwa kipindi kifupi, hii inaashiria kuwa uwezo wa kutengeneza pesa hapa hapaHivi kabla ya kutoa hizi comments zenu mmesoma hii thread imeandikwa lini?
Hii thread ni ya kitambo, ni ya miaka kama 3 iliyopita. Na wewe inaonekana tu hata hujasoma au umesoma lakini hujaelewa na hicho ulicho comment ni hisia zako ambazo ni irrelevant kwenye post hii.Ndiyo! Mleta mada anataka aende ughaibuni kufanya kazi za kubeba box. Sasa ndio namshauri abaki hapa hapa nchini maana kama kaweza kuzichanga M7 kwa kipindi kifupi, hii inaashiria kuwa uwezo wa kutengeneza pesa hapa hapa
Bongo anao...
Habari gani wangugu?
Mimi ni kijana ambae nimehitimu shahada hivi punde, miongoni mwa vitu ninavyopenda saana ni kusafiri na kuishi mashariki ya mbali kabisa tofauti na nyumbani nikakutane na watu wapya, sauti mpya, tamaduni mpya, Lugha mpya n.k
Nimefanya shughuli zangu kwa jitihada na juhudi kubwa na hadi sasa nina kiasi cha tsh mil 7/= ningependa kufika New zealand, Canada, Australia, Finland, US..
Hivyo kwa waliotayari kutoa mualiko au msaada wa kufika majuu karibuni, Na wale washauri pia karibuni, na wale haters nawahitaji sana kwa changamoto.
Karibuni!!