Samahani wadau wa jukwaa letu tukufu la MMU,
Kwanza kabisa, naamini mko wazim na mnadunda...Mie pia ni mzima na nimewa-miss kikweli kweli!!
Leo nimejikuta napatwa na mawazo ya ajabu ajabu kuhusu hili jambo ambalo katika makuzi yetu hatukukutana nalo. Enzi zetu mama alikuwa mtu wa shamba na baba anafanya kazi kidogo shamba na kutumia muda wake mwingi kuzunguka mitaa kama jogoo!!
Siku hizi, hiki kizazi kimejikuta kikikabiliwa na changamoto za kimaisha. Ni jambo la kawaida kukuta wanandoa wote wanafanya kazi na mmoja wao au wote wanalazimka kuwa na zamu za usiku.
Kwa wale wenye kazi za namna hiyo au wanafahamu washikaji/jamaa wenye kazi kama hizo, wanaweza kutupatia uzoefu wao kuhusu changamoto za kazi za namna hii especially katika sekta ya MMU??
Wenu awapendaye,
Babu DC!!
madhara ya kuoa nesi:kila mtoto atakayezaliwa utaambiwa kafanana na marehemu babu yake mzaa mama ambaye hujawahi kumtia machoni.
Khaaa.....................!😛eep:...mstaafu vipi? kwema...?
...haya bana, madhali umeyataka ya uvunguni ngoja nikupe akiba yangu ya maneno...
kaka, kwenye mapenzi hakuna kazi mbaya...kazi ni kazi almuradi mama watoto anasaidia
kupunguza makali ya maisha...hiyo kazi iwe ni ya mchana au usiku sawa tu...
...la pili, ikiwa ni mtu mwenye wivu sana, basi ombea mkeo afanyae kazi ya kutangaza Tv, au
radioni...maana kwenye luninga si utakuwa unamuona bana,....na radioni unamsikia...lakini jua
pakiwekwa tangazo la biashara au muziki...hizo dakika tano zinatosha kabisa watu 'kuchimba dawa'...
...la msingi kwenye sekta hii ya 'hamadi kibindoni' ni kuaminiana tu na kumuachia mungu afanye maajabu
yake, ..."ukimchungua kuku hutamla!"
...mstaafu vipi? kwema...?

mtu kama kiwembe ni kiwembe tu hata kama kazi yake ni mchana tu..miye naingia night kama kawaida na bado sijashawishika kumsaliti bby wangu.ila yeye uaminifu zero kabisa,yaani kila mara lazima apige simu hewani.ole wangu niingie operation usiku bila hata kumtext ntakiona cha mtema kuni
Changamoto na vishawishi ni nyingi sana kwa watu wasio waaminifu ktk mahusiano. Wako wanaotumia opportunity hizo kutembea na wafanyakazi wenzao, wapo wanatumia visingizio vya night shifts kwenda kwa nyumba ndogo, wengine kwenda kwenye starehe za ajabu ajabu nk. Cha msingi mi nitasisitiza ni uaminifu ndani ya mahusiano au ndoa. Hapo hizi changamoto haziwezi kuwa kikwazo ktk mahusiano
unataka kusema manesi sio waaminifu..?