Nigeria wakamata mchele wa plastiki

benghlasis

Member
Nov 29, 2016
49
125
Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.

Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".

Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".

Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.

*****source BBC******
 
Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,910
2,000
Weka picha ya mchele ukiwa haujachemshwa na uliochemshwa.
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,711
2,000
Wachina sio watu wanataka kuwaua waafrika ambao ndiyo soko lao kuu. Smh
 
kkarumekenge

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,710
2,000
Sasa njaa kwisha habari yake. nyama inatengenezwa kiwandani huko Uswisi, mchele wa plastic huko China, imebaki watutengenezee matunda, mihogo, pombe nk vya muundo huohuo. Ama kweli, njaa hiyoooooo, bye bye.....
 
njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,889
2,000
Hapa wa kulaumu Ni waafrika ambao wanakwenda kuweka order huko China
 
KUSHOKA

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
506
250
Mamlaka husika zipige marufuku uingizaji wa vyakula tunavyoweza kuzarisha
 
kinondoniilala

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
599
250
Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.

Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".

Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".

Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.

*****source BBC******
MKUU LAGOS NI MJI WA KIBIASHARA NA SIYO CAPITAL CITY YA NIGERIA...ABUJA NDIYO MJI MKUU WA NIGERIA
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom