Nigeria: Ajikata nyeti akiwa anaota anachinja mbuzi ndotoni

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
808
1,542
#FAHAMU Mwanaume mmoja nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 42 anapambania kuokoa maisha yake baada ya kuzikata sehemu zake za siri na kisu ndotoni, baada ya kuota anachinja mbuzi kwa ajili ya kumsaidia mke wake kuandaa chakula cha jioni.

#EastAfricaRadio
 
IMG_20220305_171647.jpg
 
Wataalam na wabobezi WA mambo naombeni ufafanuzi
IMG-20220816-WA0003.jpg


---
Mwanaume mmoja nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 42 anapambania kuokoa maisha yake baada ya kuzikata sehemu zake za siri na kisu ndotoni, baada ya kuota anachinja mbuzi kwa ajili ya kumsaidia mke wake kuandaa chakula cha jioni.

Tukio hilo limetokea Agosti 12, 2022, na kusema kwamba baadaye alikuja kushtuka na kugundua kwamba alikuwa akizikata sehemu zake za siri badala ya mbuzi kama alivyokuwa anaota.

Imeelezwa kwamba mke wa mwanaume huyo hakuwepo nyumbani na ndipo alipopigiwa simu na majirani zake kumuarifu kwamba mume wake amejeruhiwa na ndipo alipowahi kurudi nyumbani na kumkuta amezishikilia sehemu zake za siri na kisha kumpeleka hospitali.
 
Ndoto zingine ni za ajabu sana, Ina maana alilala na kisu mkononi? Kuna ndoto unaota unaogelea mtoni raha kumbe unakojoa kitandani na godoro limelowa mkojo
 
Daah watu wanashangaa wakati tukio la hivi lina ukweli na hutokea, sema halijakukuta.

Heshimu kitu kinaitwa ndoto.

Mi nimewahi kubonyeza nyeti zangu hivi hivi kama huyu jamaa eti naota naua limnyama gani kushutuka nina maumivu makali kwenye korodani zangu, kumbe nilibonyeza kwa mikono korodani.

Mimi ndoto ya hivi imewahi nitokea mwaka 2020 na ndoto zina intensity na strength yake, kwa kipimo cha jamaa ameota kwa kipimo kikubwa sana yaani anaamka anaenda kabatini na anachukua kisu anakata nyeti huku bado yupo usingizini kwenye ndoto. Ndoto ya hivi ni nzito kidogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom