Nifanyeje

Niliwahi kuwa na BF miaka kama mitano hivi imepita tulipendana sana lakini ikaja swala la dini tukashindwa kuoana yeye alioa dini yake, baada ya kutaka kuoa nilimwambia sina jinsi wazazi hawataki kusikia hiyo habari, nikamruhusu bila kinyongo hata harusi nilihudhuria, tulikuwa na mawasiliano ya kawaida tu bila kufanya chochote maana sipendi kumkosea mwanamke mwenzangu yaani mkewe, sasa limekuja swala kwamba mkewe kajifungua mtoto wa kike yapata miezi kama minne hivi mimi sikujua kumbe yule mwanaume kampa jina langu yule mtoto na mkewe ananifahamu, sasa yaani nimekaa katika mateso makubwa sana ni msg, simu za matusi kutoka kwa mkewe eti iweje mumewe ampe jina langu mtoto wake, niko njia panda mwenzenu, huyo mwanaume nimemuuliza anasema mimi ndio baba mwenye nyumba nimesema mtoto jina lake ni Fanta Face nimemaliza, nisaidieni ushauri wakubwa nifanyeje

Hizo masage za matusi si hujafuta ripot police huo utakuwa ushahidi wako ili aonywe na dola akiendelea tumia hatua nyingine za kisheria hiyo ndo maana ya zoezi la kusajili simu.
 
Back
Top Bottom