Nifanyeje...Pls Nishaurini

Nelly Huyu

Member
Mar 31, 2011
35
3
Asalam aleykum wadau wote, mimi ni kijana mwezenu na nimeoa miaka 3 iliyopita na nimejaliwa Mtoto mmoja wa Kike wa kuzaa..kilichonisukuma kuandika mada hii ni kupata ushauri kutoka kwenu kwani licha ya kuwa na mke na mtoto pia nina ishi na mtoto wangu wa kufikia. The thing is, wakati nafunga ndoa Mke wangu alikuwa tayari ana mtoto wa miaka mitano (5) nashkuru Mungu kwani hakunificha kuhusu swala hilo I mean ni jambo ambalo nilikuwa nalifahamu tangu tulipokuwa wachumba tu, na wakati tunapanga mipango ya kuishi pamoja alisema katu mtoto hawezi kuwa kikwazo kwetu kwani mtoto yule ni wa babu yaani baba yake mzazi na atakuwa anaishi kwa babu kwani kwani baba wa mtoto si msaada..by then dogo alikuwa anaishi kwa babu..nilitaka kujua kama mtoto atakuwa kikwazo kwasababu baba wa mzazi yupo hai japo si msaada kwa mwanaye licha yakuwa anajimudu kiuchumi lakini alisema hataki kuona mtoto wake analelewa na baba mwingine. Niliamini alichoniambia, tukafunga ndoa na mwaka wa kwanza ulienda vizuri mpaka pale aliponiambia kuwa anata akae na mtoto kwasababu akiangalia afya yake si nzuri kutokana na kukosa uangalizi..nilimkubalia kwani alisema kuwa litakuwa jambo la muda mfupi..sasa nimekuwa nikiishi naye kama mwanangu since then, sina tatizo kuhusu hilo kwani kimsingi yule ni mwanangu..kinachonikwaza ni yeye mke wangu anavyomdekeza mtoto kwani kila anapokosea na ukijaribu kumuongoza kwa kumsema au ikiwezekana kumchapa basi ataingilia kati na kukujengea mazingira kuwa unamchukia mwanaye, hii inapunguza heshima toka kwa mtoto kwenda kwa baba haswa ukichukulia kuwa anamiaka tisa, sasa swali langu ni kwamba kama namchukia mtoto kwanini hataki kumpeleka kwa baba yake..isitoshe jamaa yaani baba wa mtoto anadharau sana, zakujishow off kuwa anauwezo wa kumlea mwanae ila mke hataki, je ni haki kulea mtoto wa mwanaume mwenzio ambaye yupo hai na anadharau....ni vyema kwa mke wangu kunipandikizia chuki kwa mtoto? Nifanyeje?
 
Pole sana ndugu yangu kwa changamoto inayokukabili. Kusema ukweli inahitaj moyo wa ujasiri kukaa na mtoto ambaye si Damu yako. Ninachokushaur mweleze mkeo kwamba hufuraishwi na perception yake pale unapokua una muonya mtoto na kama ikiwezekana mwambie ampeleke mtoto kwa baba yake kwakua anauwezo wa kumudu gharama. Kama ikishndkana muite wazaz wa pande zote mbili mkae nakujadili kwa kina swala hilo ili mpate muafaka
 
dah kaka pole
umetenda mema malipo ndo kama ayo ..pole sana

kaa na mkeo mwelewesha madhara anayoyafanya wakat ukimkanya mtoto mwambie ukweli na umwambie aupend na iweje ili ajirekebshe...

usikae na duku duku moyon cz itazaa chuk pia ta wewe utaanza kumdis mtoto na mama yake na apo ndoa itakua ICU ..

plan b;
nenda kwa wakwe zako waambie vle bnt yao analate autoto kwenye malez ya mtoto na vle wewe unavyojisikia ju a ilo babamkwe atakuelewa

dzain MKEO NA JAMAA ALIYEZAA NAE WANACHAPANA....yess chunguza fresh...:disapointed:
 
Mkeo anakosea jambo moja tu, nalo ni kukujengea chuki kwa mtoto.
Halafu wewe unaonekana una hasira na huyo baba mtoto, halafu hizo hasira kama vile unazipeleka kwa mtoto kidogo kidogo.
Hebu kuwa karibu na huyo mtoto, mwoneshe upendo. Siku za weekend jaribu kumchukua mkatembee hata kama ni maeneo hayo hayo. Mpe mahitaji yake yote kama mtoto, uwe unampelekea vizawadi siku mojamoja.
Nina uhakika kama utakuwa unayafanya hayo kwa moyo wako, siku mtoto akikosea hata ukimuazibu mama yake hatomaind, na hata mtoto ataona humuadhibu kwa kumuonea.
Nahisi wewe ushatengeneza gap kati yako na mtoto. Ni kitu kibaya sana. Watoto huwa wanajua wapi wanapendwa wapi hawapendwi.
Usiishie kutoa miadhabu tu, show love japo kidogo.
Kama anasoma onesha kuwa anajali maendeleo yake ya shule.
Nitarudi b'dae kwa ushauri wa pili.
 
wanawake wengi walioolewa wakiwa na watoto au wale wanaolea watoto bila baba huwadekeza watoto....siku zote mama huwa over protective na mtoto wake ambaye anaishi na baba wa kufikia akiamini hana mapenzi kwa yule kwa kuwa si mtoto wake.....ni kitu imejengwa kisaikolojia na ndo maana wanaume wengine hukwepa kuoa wanawake wenye watoto wasio wao....nakuambia hivi umuelewe mkeo na ujaribu kutafuta namna nyingine ya kumlea na kumrekebisha huyo mtoto bila yeye kuona unamfanyia vile kwa kuwa si wako wa kuzaa....njia pekee ni hiyo aliyosema Husninyo,mweke karibu aamini unampenda kama mtoto wake,mwambie makosa yake na kuwa hupendezwi na pale inapobidi mwambie huyo mama yake na amuadhibu yeye kama njia ya kumrekebisha kwa mdomo imeshindikana....kumfundisha mtoto si lazima umpige,waweza mpa adhabu hata ya kukosa vitu vizuri ulivyomzoeza kutokana na tabia yake mbaya....mfano,hakuna kuangalia TV wala kwenda movie kama hafanyi homework,hakuna kwenda beach kama hafanyi usafi wa chumba chake.....etc
 
Kwa Husninyo

Nashkuru kwa ushauri istoshe yote ulisema ni mtazamo I do admit kuwa kama binadamu unaweza ukatenda hayo uliyosema haswa ukiwa umejengwa na hisia za wivu na chuki ndani yake...kwa upande wangu ni tofauti kabisa kwani ninaweza nikasema afadhali mimi ninaweza nikaongea na jamaa "baba wa mtoto" kuliko mke wangu. kwani wao wanachukiana mno kiasi ambacho naona kinamuathiri hata Mtoto..kwani nahisi kutokana na chuki zake jamaa ndio maana hataki kuwajibika kwa mwanae akihisi mwanamke atafaidi sana...hii inamfanya mke wangu anteseka nae mtoto mwenyewe kwa ada za shule hata malazi...siku mwanzo alikuwa hataki kunihusisha kwa kuhofia nitamjibu kuwa si jukumu langu..lakini kuona mkeo anateseka ni jambo gumu...kwani saa nyingine unaona akiomba msaada mathalani wa ada ya shule kwa baba yake yaani babu wa mtoto.....thats why I decided kuwajibika fully, and I dont have probs with..tatizo langu ni malezi na makuzi ya mtoto..mbona nikimrudi mwanangu wa kike huwa haingilii japo ana miaka mitatu kasoro tu. mimi namshkuru Michelle kwa aliyoshauri na ninahisi inawezeka aliyosema kuhusu wanawake wa sampuli kama hii ya mke wangu wanavyopenda kudekeza watoto...Pengine wife anahisi mtoto wake huyu angestahili haki zaidi ya hizi anazozipata kwangu thats why anajitahidi kumpatia only kwa njia ambazo si sahihi.
 
Nelly hongera kwa moyo huo.
Kwasababu umesema unaelewana na huyo baba hebu jaribu siku moja umuite kirafiki, ongeeni mambo mengine halafu chomekea hilo la mtoto (akwambie msimamo wake na ushirikiano wake kwa malezi ya mtoto ni vipi).
Inakera kama anajiweza halafu anashindwa kumuhudumia dogo ingawa pia hatujui kichwani mwake anafikiria nini juu ya mwanae.
Mungu akupe nguvu katika wakati huu mgumu ulionao.
 
Nelly hongera kwa moyo huo.
Kwasababu umesema unaelewana na huyo baba hebu jaribu siku moja umuite kirafiki, ongeeni mambo mengine halafu chomekea hilo la mtoto (akwambie msimamo wake na ushirikiano wake kwa malezi ya mtoto ni vipi).
Inakera kama anajiweza halafu anashindwa kumuhudumia dogo ingawa pia hatujui kichwani mwake anafikiria nini juu ya mwanae.
Mungu akupe nguvu katika wakati huu mgumu ulionao.

Nashkuru kwa ushauri
 
Nawapenda saana watoto, simjui mama yangu alifariki nikiwa 3yrs old na nimeishi na mama wa kambo maisha yangu yote, najua uchungu wa kumkosa mzazi hasa mama jamani, ingawa hii kesi mama yupo lkn nikiona mtoto anapelekwa mbali na mzazi wake napata uchungu saana najua tabu ya kuishi mbali na mzazi! Mkuu umejitolea kukaa na huyo mtoto, kaa naye ingawa majaribu yanakupata na kusababisha taabu lakini piga goti mwombe mungu hizo ni changamoto katika maisha, naamini hiyo ni test anakupa mungu jitahidi uikabili na pengine huko mbeleni mungu akakuzawadia mambo mazuri sana. Usife moyo najua wanawake sometimes wakianza visingizio inakera sana tena sana lkn angalia usije ukaharibu maisha yako na ndoa yako kwa ajili ya huyo mtoto, kama mama yake hawezi kumfunza mwanaye wewe achana naye kazania wa kwako sababu huyo wake analeta ugomvi mwache mkeo atakuja kuona umuhimu wako hapo mtoto atakapokuja kuharibu kwa tabia mbaya
 
Tumesikia kutoka kwako, hatujasikia kutoka kwa mkeo, lakini kwa kuwa hii si mahakama tutakupa ushauri:

Waswahili hunena "Ukipenda boga, upende na ..." Utajaza mwenyewe.
 
Wanaume nyie mkikamata mtoto kumpiga, munampiga hadi karibu kumuua. Nyie wanaume hasiri yenu ni wauwaji. Nyie hamjari awe mtoto wenu au wa mwenzenu, hamjari nyie munavunja tu mtoto. Fikirii baba ako akivokupiga pale utotoni, kama mama ako alikuwa haingilia kati. Wanawake wakati wote uwaami watoto wao wakipigwa na mume wao, haijarishi kazaa na wewe au na mwengine.
Na kuto mtaka kwako huyo mtoto, ndio sababu mkeo anahofia husimulie mwanae kwa wivu wako. Huyo mtoto hana kosa lolote kiumbe cha mungu, mwenye kosa baba ake na mama ake. Na wewe ilibidi umsapoti ako katoto kwa kukataliwa na baba ake. Ukifikiria baba ake hamtaki, na wewe haumtaki, ataenda wapi ? na ikiwa anaitaji upendo kutoka japo kwa mmoja wa wazazi wake ambae ndie mama ake ulie muoa wewe. Jamani kueni na huruma na viumbe vya mungu. Ukimtunza kwa amani na upendo, atakuona wewe ni mungu, na kumzarau baba ake. Fikiria future, kipindi umesha zeeka, na ako katoto kakawa bonge la tajiri, na akijua ukinyanyasa kwa sababu...., sura ako utaiweka wapi? mpende kama mtoto wako, muhurumie na kumcare vizuri, atakusaidia huyo baadae, ondoa wivu na ushangingi kwa yalio pita.
 
Wewe kuwa kama mwanaume uanogopa nini kama unatenda haki na haumuonei huyo mtoto?? Akikosa charaza viboko tu hakuna cha mama yake eti unamuonea mtoto allah kuwa Baba mwenye nyumba akinuna anune salama endeleza adabu tu
 
aheri ya wewe unaweza kuongea na baba wa mtoto huyo kuliko mkeo. hapo kuna jambo mkeo hajakueleza ka undani, hawakuachana kwa wema na wakati huo mmoja wapo bado alikuwa ktk penzi, kaa na mkeo najua hawezi wala hatothubutu kumueleza mzazi mwenzie shida za mtoto nadhani anajitutumua kumuonyesha hata bila ya yeye anaweza kumuhudumuia mtoto , kwa msingi huo ni lazima ili malezi yaende vzr asikuwekee mipaka ktk malezi ya huyo mtoto kama anataka kumuonyesha mwenziwe kuwa hata bila ya yeye mtoto anakuwa. hao wawili wote ni watoto wenu mueleze alijue hilo (jitahidi maana hiyo ni kazi ngumu inaonekana hiyo ni tabia iliyojificha ya mkeo)
 
Dah! Pole sana kaka.
Naninachoweza kukushauri ni kuwa ukipenda ua penda na mti wake.
Just imagine huyo ni mtoto uliyemzaa wewe, dawa ya mtoto ni kuwa naye karibu tu na kumwonyesha upendo. Hapo atakutii. Ukiwa mkali sana kwa mtoto, atashindwa kuwa karibu na wewe.
Huyo mkeo ndo wale ambao wanataka kuingilia malezi ya watoto. Nadhani mpaka mmeoana, ni kwamba mmependana.
Siku zote katika maisha penda kuwa mkweli ili uwe huru. Mweleze ukweli kuwa huna nia mbaya kwa mtoto unapomkanya.
Kama baba mtoto anammaind mwanaye, ana haki ya kumchukua. Mwachie na muanze ukurasa mpya.
 
Wanawake wengine bwana umepata bahati umeolewa japo umezaa na mwanamme mwengine halafu unajifanya kuleta sheria zisizo na mbele wala nyuma, wewe muonye mtoto akikosa sn sana kwa maneno ya busara pia usipende kumpiga course unaweza mpa madhara bre kibao kikakubadilikia. Pia chukua muda wa kutoka nae out mtoto kwenye michezo mkiwa peke yenu ujaribu kubond nae ili mama akuamini. maana mtoto atakapokuwa free na wewe hata mama hatakuwa na matatizo wala mawazo kwamba unamtesa mtoto.
 
Mkuu angalia asije akawa anapandikiza chuki baina yako na mtoto halafu mtoto akaanza kukuchukia ghafla maana suala muda si mrefu litaanza kuonekana kaa na mwanamke chini umueleze hata akichukia there are things you do not need to entertain at all mwisho wa siku utaonekana wewe ndio ulikuwa una makosa kama mtoto akiharibika its your duty.
 
Kwako Nelly

Pole sana kwa matatizo yaliyokukuta hayo ndio maisha yana changamoto nyingi sana na kuzikabili ndio uanaume wenyewe.
Najua kesi yako ni ngumu sana kwa kuwa imekaa kisaikolojia zaidi.

Mie ninachokushauri ni kuwa jaribu kukaa na mke wako na mweleze kwa undani kabisa kuwa unachotaka kufanya ni kumlea huyo mtoto kama mwanao na si kuwa unamwonea au kumpendelea kwa chochote na umweleze jinsi gani unavyokwazika kwa jinsi anavyomfanya na kumdekeza na kuleta mazingira kuwa unamwonea kwa unapotaka kumwadabisha. Kama mwanamke ni mwelewa anaweza kuelewa na maisha yakaendelea vizuri

Jaribu kuishi na mkeo katika misingi ya kufanya vitu vyote kwa pamoja na kuweni wawazi ktk kila jambo na pia ujenge imani kwa mkeo, maana inaonyesha mkeo hakuamini.

Kingine kikubwa ni kuwa kama mmeamua kuchukua jukumu la kumlea huyo mtoto mumlee kwa moyo mmoja na achana kabisa na huyo baba wa mtoto kama umemkubali mtoto lipa na epuka kabisa mkeo kukutana kutana na kuwasiliana na huyo jamaa, maana wanaweza siku wakakugeuka kwani tayari ni wazazi. Naona kitendo cha kumweka karibu wakati yy hana mpango na mtoto wake ni sawa na kumkaribisha shetani nyumbani kwako.

Kuishi na mtoto ambaye si wako ni kazi sana na kama ukiona kila ukichukua hatua mambo bado hayaeleweki jaribu kuita watu wazima wenye uzoefu na mambo kama haya watakushauri vizuri na kukuelekeza nn cha kufanya.
 
Back
Top Bottom