Nifanyeje niweze kuipenda soka?

Nifanyeje niweze kuipenda soka?

TRIPLE H

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
651
Reaction score
351
Wakuu, salaam!

Soka ni mchezo unaopendwa sana na watu wengi duniani kiasi kwamba hata afghanistan wanaamua kusitisha mapigano kwa ajili ya kuangalia mechi za kombe la dunia zinazoendelea kutimua vumbi nchini Brazil.

Lakini pamoja na hayo yote mimi nimeshawishiwa sana na wanajeshi wenzangu wanaotoka tanzania ili nishabikie timu za nchi fulani fulani kama brazil,argentina,croatia,japan,ghana,cameroon,england,france nk,lakini kila nikiangalia sichukui round usingizi hunijia hasa hizi mechi za usiku na ninaposinzia huibuliwa na makelele ya mashangilio ya wenzangu.

Lakini kama kuna live events za mieleka ya wwe huwa siwezi kutulia hata kama nimechoka kiasi gani kwa purukushani hizi za vita!

Sasa nifanyeje ili nipate desire ya mchezo huu?

Nawasilisha!
 
Wakuu,salaam!

The best solution, anza kufuatilia mechi za germany..... from this weekend na kuendelea
 
una miaka mingapi sasa? kama ushavuka 21, na hujawahi kuwa na mzuka na mpira wa miguu basi sidhani kama utakuja kuupenda ni bora tuu ukabaki huko kwenye mieleka na masumbwi
 
Mimi kwenye soccer huniambii kitu lakini hayo ma mieleka hata yaoneshwe samoja siwezi kuangalia tupo tofauti. Kwako ndio imetoka hiyo ikirudi pancha kamaa wwe.
 
Wakuu,salaam!
Soka ni mchezo unaopendwa sana na watu wengi duniani kiasi kwamba hata afghanistan wanaamua kusitisha mapigano kwa ajili ya kuangalia mechi za kombe la dunia zinazoendelea kutimua vumbi nchini Brazil.
Lakini pamoja na hayo yote mimi nimeshawishiwa sana na wanajeshi wenzangu wanaotoka tanzania ili nishabikie timu za nchi fulani fulani kama brazil,argentina,croatia,japan,ghana,cameroon,england,france nk,lakini kila nikiangalia sichukui round usingizi hunijia hasa hizi mechi za usiku na ninaposinzia huibuliwa na makelele ya mashangilio ya wenzangu.
Lakini kama kuna live events za mieleka ya wwe huwa siwezi kutulia hata kama nimechoka kiasi gani kwa purukushani hizi za vita!
Sasa nifanyeje ili nipate desire ya mchezo huu?
Nawasilisha!

Endelea kukaa na dada zko kuangalia mara clara na isindingo
 
Angalia Ratiba ya leo ya mechi
 
Attachments

  • ratiba ya mechi.jpg
    ratiba ya mechi.jpg
    72.7 KB · Views: 126
Kuupenda mchezo ambao hata huujui hata kidogo ni kazi sana,lakini ukianza kufuatilia taratibu na kuuliza maswali pale ambapo huelewi kilichotokea basi baada ya muda utaanza kuufahamu na kuupenda. Siku moja tulikuwa tunaangalia na marafiki mechi ya league kati ya Simba na Majimaji pale Songea basi tulikaa jirani na njemba ambayo nadhani alikuwa mara ya kwanza kuhudhuria mechi ya mpira wa miguu basi akatoa akatoa comment wakati mpira unaendelea, "Hawa kwa nini wanagombania mpira mmoja? Si wangempa kila mtu mpira wake ili waache kugombania mpira mmoja.?" Jinsi alivyokatwa macho na watu waliokuwa wamekaa jirani yake alijua kabofoa. Kila la heri katika jitihada zako za kuupenda mpira.
 
kuna mtu mmoja hivi miaka yake kama 30 ananiuliza kombe la dunia real madrid wanacheza lini
 
Tafuta clabu yoyote ya uengreza hasa arsenal na uanze kuipendelea, baada ya mwezi tu utajikuta unabishana na watu mpaka asubuhi
 
Mimi nkimuona mtu anaangalia meleka naona anatupa muda tu bora akalale kama hana kazi
miereka niliwacha kutizama na miaka 10yrs old ni mchezo naona wa watoto kutizama hasa sababu ndio wanamazoezi ila uongo tu hata ile mieleka ya Olympic sitizami angesema UFC sawa. Ila Yakkina undertaker sijui ah waachie watoto.
 
Mimi bado sijaelewa tatizo lako ni nini. Kwani ni lazima uipende soka. Kwanza ni bora hata zingekuwa mechi za mchana, wewe kama hupendi sio ndio poa unakula zako mbonji tu au?
 
Sio lazima mkuu... Ndio maana tuko tofauti. Wako wanaopenda soka, mieleka, ndondi n.k.

So wewe endelea kupenda mieleka sie tutapenda soka
 
Fuata ushauri wa BAK. Ukianza kufuatilia na kuuelewa mchezo utaupenda. Ila usitishwe na usingizi, ni kwa sababu ya kuchoka tu, unaweza angalia marudio aka viporo
 
Last edited by a moderator:
Swala la kupenda na kukesha kuangalia mpira Ni vitu viwili tofauti, Mimi Ni shabiki mkubwa WA mpira lakini siwezi acha kupumzika nikeshe kuangalia mpira
 
Back
Top Bottom