Nifanyeje na mimi niwe na furaha

Nifanyeje na mimi niwe na furaha

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,886
Reaction score
40,065
Wasaalamu wandugu na majamaa nipo kwenye wakati mgumu sana sasa hivi kimaisha....................kiasi kwamba najiona kama mtu aliyekosa raha maishani....najikuta muda mwingi nipo mpweke na mwenye mawazo tele......muda napenda kukaa alone...............MSAAAAAAAAAAAADA PLEAAAAAAAAAAAAASE
:confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::madgrin::madgrin:
 
lazima ujue ni kitu gani kinakunyima furaha ?

ukikaa alone unafanya nini? me napenda kukaa alone mda mwingi lakini nakuwa nipo busssy na internet na aangalia movie like that... wewe je?

je kitu gani unahisi ukipata utapata ? furaha ukiweza pata jibu ya hili na kiasi gani umejitahidi kupata hiyo kitu?
 
wakati mgumu kiaje........Not everything can be perfect, and some days are gonna suck more than others.

You just have to give life a fair chance. Not thinking "Tomorrow is gonna be a horrible day" its hell


have fun,go out,shinda JF,watch movie na vitu ka hivo
 
pole mdau ni stress inakusumbua inatakiwa ukubali hali iliyopo baada ya mda mfupi itakaa level
 
Ugonjwa wa "SONONA" unakunyemelea

1. sikiliza nyimbo uzipendazo
2. usipende kuka mazingira ya kimwenyewe mwenyewe
3. Huenda matarajio yako yameyeyuka ...ongeza juhudi katika ibada
4. .......
 
Angalia usiishie kujinyonga mkuu....this is just life meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen...just cheer up
 
inawezekana unayo furaha lakini hujui kui2mia vzr. ni sawa na kumtengea chakula mtu mwenye njaa halafu asichukue hatua ya kula chakula hicho--ataishia kulia njaa tu. hiyo unayoiona huzuni au sonona, kwa mwingine hiyo ni furaha.

pia ikiwa kuwa lonely kunakukosesha amani, kwanini usijichanganye na wengine? una tatizo gani?
tafakari, chukua hatua!
 
Mathayo 6:25-34
25‘‘Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi? 26Waangalieni ndege wa angani, wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege? 27Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake aweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake au kuongeza dhiraa mojab kwenye kimo chake ?
28‘‘Nanyi kwa nini kujitaabisha kwa ajili ya mavazi? Fikirini maua ya shambani yameavyo. Hayafanyi kazi wala hayafumi. 29Lakini nawaambia, hata mfalme Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa kama mojawapo ya hayo maua. 30Lakini ikiwa Mungu anayavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba? 31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?' Au ‘Tutakunywa nini?' Au ‘Tutavaa nini?' 32Kwa maana watu wasiomjua Mungu ndio wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji hayo yote. 33Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake na haya yote mtaongezewa. 34Kwa hiyo msiwe na wasi wasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.''

Ilani:

Mpokee Yesu Kristo kuwa Bwana na dereva wa maisha yako!
 
Lazima ujue kitu gani kinakunyima furaha

Ukishajua then tutaanzia hapo namna ya kukusaidia

Maana kujua tatizo ni nusu ya kulifumbua
 
Lazima ujue kitu gani kinakunyima furaha

Ukishajua then tutaanzia hapo namna ya kukusaidia

Maana kujua tatizo ni nusu ya kulifumbua
Nakosa furaha..coz maisha yangu yamekuwa magumu baada ya wezi kunivunjia kibanda changu cha biashara ndogo ndogo na kukomba kila kitu..ikiwemo na mauzo ya siku hiyo na hela flani nilikopa ili nikuze mtaji wangu....yaani nifull majanga majanga......
 
hilo tu? au kuna jingine? Changamka mwambie Mungu asante maana wale wezi hawakuchukuwa uhai wangu, mikono na mwili wangu viko salama, maisha yaendelee acha kujizidishia maumivu kwa kuwaza hata kama huo mtaji uliupata kwa mkopo..... panga pangua utapata pa kuanzia ..... shukuru kwanza hawajakugusa, wangekubaka je? si ungetuletea msiba hapa!!!? ....... binadamu tumeumbwa kuchacharika hasa vidume KUKULAchochako
 
Last edited by a moderator:
Nakosa furaha..coz maisha yangu yamekuwa magumu baada ya wezi kunivunjia kibanda changu cha biashara ndogo ndogo na kukomba kila kitu..ikiwemo na mauzo ya siku hiyo na hela flani nilikopa ili nikuze mtaji wangu....yaani nifull majanga majanga......

dah! pole sana hukuchukua tahadhari before? na plan b je? kila kitu kinatokea kwasababu!
 
Back
Top Bottom