happy amos
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 251
- 434
Naombeni ushauri
Nifanyeje mume wangu aniamini kama mwanzo?
Iko hivi:-
Mwanzo mwenzangu alikuwa ananishirikisha mambo yake. Ikifika mwisho wa mwezi ananiambia kimepatikana kadhaa tufanye yafuatayo.
Sikujua kama alikuwa ananishirikisha kwa kunitega au la maana alikuwa anataka robo tatu ya kipato chake awekeze kwao. Sasa akawa akiniomba ushauri namwambia nusu aweke kwao nusu inayobaki tufanye yetu kwa ajili ya familia yetu.
Kumbe nilikuwa nakosea yeye alitaka nimshauri awape zote nyumbani. Alikua kila tukikaa mipango ya maendeleo anapanga ya kwao mi nikawa namshauri asisahau na sisi ndani maana alikua hafanyi chochote kwa ajili yetu.
Mashemeji zangu wanamsumbua sana kumuomba hela, akawa ananishirikisha namwambia angalia shida yenye umuhimu umsaidie mtu, ukiona mtu anakuomba sana hela kama hana kazi mpe mtaji au mtafutie kazi.
Kumbe nilikuwa nategwa tu bila kujua. Siku hizi mwenzangu hanishirikishi kabisa mambo yake Mshahara ukitoka sijui umetumikaje na
likitokea tatizo kwao wala haniambii kama mwanzo.
Moyo unaniuma nashindwa nitairudishaje ile hali ya zamani. Nifanyeje ajue sikuwa na nia mbaya?
Naumia sana ndugu zangu mke na mume ndani hatushirikishani, hatukai tukapanga kama mwanzo kila mmoja anafanya kulingana na kipato chake na maendeleo hakuna.
Nimejaribu kuongea nae na kumuelewesha lakini kama hataki kuelewa hivi. Nisaidien nifanyeje?