Kwa tulioa tunajua ambacho huwa kinatokea.
Wanawake huwa wanawishi muwe na maisha ya kizungu(nuclear family).
Sasa hayo maisha wanataka yawe upande wa mwanaume tu. Kwao inakuwa extended family.!!
Yaani ndugu zake wasaidiwe kadiri ya watakavyo ila ndugu wa mwanaume Ni kuwakaushia tu.!! Wameshindwa kulibalance Hilo.
Mimi mambo ya kwetu huwa simshirikishi.
Natunza familia na mambo ya kwetu nayafanya bila kumuambia
Maendeleo yangu binafsi nayafanya.
Kwa hiyo habari za ndugu yangu kuomba visivyokuwa vya maana huwa namalizana nao mwenyewe.!!
Na ili ufanikiwe Hilo mwanaume hutakiwi kumwambia mwanamke Kila kitu unachokipata.
Lazima uwe na mpango wa kando kwa dharula zako.!!
Haya wanayoyafanya mama zetu na dada zetu wameyafanya kwa ndugu wa waume zao.
Mwanaume weka sawa kichwa chako.
Tafuta hela
Tunza familia yako
Usiwasahau ndugu zako(mkeo Ni rafiki tu).
Sent using
Jamii Forums mobile app