wao ni wao
JF-Expert Member
- Dec 23, 2022
- 1,179
- 2,827
Ndugu habari
Direct kwenye mada, ndugu zangu kuna kijana naishi naye karibu sasa ni mwaka mmoja.
Ilikuwa hivi nilipohamia huku vijijini baada ya kuletwa huku kutokana na makosa ya ulevi uliopindukia na pia kuwa mtoro kazini basi nilifika huku nikaendelea na shughuli za serikali huku nikiwa sinywi kama mwanzo.
Baada ya miezi kadhaa hapa kijijini nikajuana na kijana mmoja rika la miaka ishirini na minane, tulikutana bar moja hapa.
Ulikuwa ni usiku mmoja wa jumapili nikiwa nafurahia mziki na pombe yangu pembeni mwa meza , ghafla bin vuu huyu kijana kakaribia mezani kwangu na kuagiza kinywaji chake.
Basi kwakuwa mimi ni mtu wa stori sivungi basi tukawa tunapiga stori za hapa na pale japo alinianza yeye kwa kusema kaka nahisi nakufananisha nikasema na nani ?
Akamtaja mtu sikumjua ila pia akasema ni wa dar es salaam nikasema labda japo dar es salaam ndiyo nyumbani basi naye akadai huko Dar es salaam ndiyo kwao pia na yeye anatokea Kisemvule matembele mawili.
Basi nikasema kumbe niko na home boy basi story zikaendelea ikabidi nimpe ofa mdogo wangu japo na yeye sio kinyonge akaagiza pia
Basi ikawa ni mwendo wa weka niweke ila mida ya saa sita nikabidi niage ili niwahi nyumbani sababu mama la mama hapendi nichelewe sana nyumbani.
Basi ikawa ndiyo mwanzo wa kujuana na yule kijana , basi mara kwa mara tukawa tunakutana sana bar , ananipa salamu zangu mimi kama mzee wake na stori zinaendelea
Mwisho wa siku ikabidi nitake kujua wajihi wake hasa ni lipi au kipi kimemleta pale kijijini japo ilionekana yeye kunijua fika kwa kazi ninayofanya maana aliwahi sema siku nikipata muda nitakuja ofisini kwako maana nina shida fulani.
Alinieleza ya kuwa yeye hana kazi ila kaja kutafuta maisha huku kijijini sikuwaza sana maana maisha ni popote ila akasema pia anataka adeal na kilimo to the maximum.
Basi ikawa hivyo akanizoea sana mpaka kuwa anakuja nyumbani kwangu baada ya kumueleza ni wapi naishi
Wife kamfanya kama kijana wake maana ni mdogo sana kwetu
Ila sasa shida inakuja kuwa wanakijiji hasa wale wenye vyeo vya kijiji yaani mtendaji , mwenyekiti na diwani kumtulia shaka ya kuwa hawana imani naye na hawajui kafuata nini hapa kijijini.
Maana wanasema wanamuona sana usiku wa manane akiwa na watu wengine ambao huwa wanakuja na gari wanaweza kukaa hata kwa masaa mawili matatu alafu wakaondoka hivyo walimuita kutaka kujua huwa ni akina nani wale usiku wa manane na uwa wanazungumza nini?
Ila kijana aliwakanusha ya kuwa hayo ni maisha binafsi na hayawahusu hivyo wananiomba mimi nimueleze kuwa hawamuitaji hapa kijijini.
Kwangu mimi sioni kosa lake lakini pia vijijini kwa haya mambo ni kawaida ila pia shida ni kuwa kijana nikitaka anipeleke kwake uwa ananipanga sana mpaka nilishaacha kumuulizia habari za kwenda kwake.
Ila huyu kijana hapa kijijini uonekana siku ya jumapili na jumatatu na jumanne tu , siku zingine humkuti na haijulikani anakuwa wapi hii ni kwa mujibu wa wapelelezi wa kijiji.
Sasa ndugu zangu wana jamiiforum nauliza huyu kijana nimtenge niachane naye japo ni homeboy kwa maelezo yake au niendelee naye maana wanakijiji hawana imani naye kwa minajiri ya kuwa anaweza kuwa jambazi.
Nimeshindwa kumuelewa kijana wangu , jana nimekaa naye nikajaribu kumueleza hali halisi ya watu wa kijijini yeye hajali lakini pia ameonekana kutopenda mimi kuzungumzia hizo habari zaidi ya kuniambia mzee hayo achana nayo watajua wenyewe.
Ushauri wako ni muhimu