Nifanyeje ili mpenzi wangu aniamini?

Swenailie

JF-Expert Member
Feb 15, 2016
240
229
Habarini ndugu zangu,

Niko tena pamoja nanyi tuelekezane zaidi.Ninampenzi wangu kweli nampenda Ila tatizo kubwa haniamini. Ninapata wakati mgumu sana na inafikia kipindi najuta uhusiano huu.

Kwanza swala la simu. Mm simu yangu iko wazi masaa yote yake inapasword. Nikiwa nae anashika simu yangu mda wote mimi sishiki yake kwani najua ninawivu naogopa kukutana na nisiyoyatarajia yakaniumiza na siwezi kumuacha ila yeye yangu anakagua kila saa kitu kidogo hata mtu kanisalomia maswali mengi sa nyingine ugomvi.

Pili ni kwanini sihoji na sikatazi mtu outing. Mimi najua mwanaume ni tofauti na mwanamke. Niko mbali hatuishi mkoa mmoja. Anapenda kunywa. Sasa mtu akikwambia niko na washikaji nakunywa hapa kuna haja ya kusema rudi home usinywe au nipe simu niongee nao nihakikishe au sitaki utoke sa hii angali uko mbali je akinidanganya. Na je hao rafiki zake wanachukuliaje nikianza kuhoji hivo. Nikikubali sawa enjoy naonekana sijui kucare au kuna mwingine nakuwa attention nae.

Kumlimit baadhi ya marafiki. Hivi mwanaume mtu mzima unaweza mpangia marafiki.? Nachojua unaweza mshauri mtu uwe macho kwa hili na hili apambanue yeye. Siku nikiwa kwake akirudi kalewa akalala kesho anaamka anasema hii company hapana aisee anakugeuzia kibao wewe kama mwanamke unatakiwa unihimize niachane na hii company unatakiwa hata tugombane.

Huna mpango na mimi ndo maana unaniacha acha tu. Hivi jamani mtu mzima unaweza gombana nae kisa company au yeye anatakiwa achuje. Najua kwa mwanamke ni rahisi mwanaume kuweka limit kwa baadhi ya marafiki mwanaume ni ngumu. Au mimi ndo sijui kutunza mume.

Eti kwa miaka mitatu niliyokaaa nae natakuwa niwe nimejua kipato chake na siulizi. Ningekuwa najua nafatilia kinatumikaje asingekuwa anakunywa Hivi. Jamani mimi nafanya kazi na yeye anafanya kazi hivi nilazma kuweka wazi haya mambo kabla hatujaoana wala kutambulishana nyumbani. Mimi sijahoji coz pia sitaki anihoji kwa sasa labda badae tukiridhia kuoana.

Ninaona inafikia wakati haniamini kama niko seriously na imepelekea tunapishana sana tunapojadili hizi tofauti zetu naishia kuonekana ninamakosa mwanamke kuna mambo ni wajibu wangu kuyafatilia.

Hebu nisaidieni labda sielewi ni nini natakiwa nifanye kwa mtu nilie na mpango wa kuishi nae. Najihisi ninamadhaifu sana. Nakosa hadi ujasiri.
 
Hajitambui huyo, kunywa anywe yeye halafu akulaumu wewe. Ukianza kuja juu kuhusu unywaji wake atakwambia wewe mwanamke una wivu sana. STUKA hakuna future hapo mwambie ajirekebishe na umechoka na lawama zake kwako, kama bado hasomeki basi ingia mitini bado mapema.
 
05969945a7c71d598473a6e08200131e.jpg
 
Aah anafanya vitu makusudically ili aonewe wivu eti. Mkimfuatilia utasikia "huyu mwanamke hanipi space"; khaaa hawana jema binadamu wengine
Ndohivo my dear, unaloona kero kwako kwa mwingine burudani... Sio uko na mtu kama huko nae vile,we chochote fanya wala haulizi
 
Ndohivo my dear, unaloona kero kwako kwa mwingine burudani... Sio uko na mtu kama huko nae vile,we chochote fanya wala haulizi
Hahaha me naona anamuonea tu dada wa watu, umeaga unaenda kunywa, nikikukataza ni nongwa, basi nakwambia tu "enjoy baby".

On a serious note, baby wake huyu anapenda ufilipino, anapenda kudekezwa, so shosti ajitahidi tu kumdekeza. Kweli wanaume hawatabiriki khaaa
 
Hahaha me naona anamuonea tu dada wa watu, umeaga unaenda kunywa, nikikukataza ni nongwa, basi nakwambia tu "enjoy baby".

On a serious note, baby wake huyu anapenda ufilipino, anapenda kudekezwa, so shosti ajitahidi tu kumdekeza. Kweli wanaume hawatabiriki khaaa
Hapo kwenye kudekezwa ndo penyewe sasa
 
Habarini ndugu zangu,
Niko tena pamoja nanyi tuelekezane zaidi.
Ninampenzi wangu kweli nampenda Ila tatizo kubwa haniamini. Ninapata wakati mgumu sana na inafkia kipindi najuta uhusiano huu.

Kwanzaa swala la simu. Mm simu yangu iko wazi masaa yote yake inapasword. Nikiwa nae anashika smu yangu mda wote mm sishiki yake kwani Najua ninawivu naogopa kukutana na nisiyoyatarajia yakaniumiza na siwezi kumuacha Ila yeye yangu anakagua Kila saa kitu kidg hata mtu kanisalmia maswali mengi sa nyingine ugomvi.

Pili Ni kwanini sihoji na sikatazi mtu outing. Mm Najua mwanaume Ni tofauti na mwanamke. Nko mbali hatuishi mkoa mmoja. Anapenda kunywa. Sasa mtu akikwambia Niko na washikaji nakunywa hapa Kuna haja ya kusema rudi home usinywe Au nipe simu niongee nao nihakikishe Au staki utoke sa hiii angali uko Mbali je akinidanganya. Na je hao rafk zake wanachukuliaje nikianza kuhoji hivo. Nikikubali sawa enjoy Naonekana sijui kucare Au Kuna mwingine nakuwa attention nae.

Kumlimit baadhi ya marafiki. Hivi mwanaume mtu mzma unaweza mpangia marafiki.? Nachojua unaweza mshauri mtu uwe macho kwa hili na hili apambanue yeye. Siku Nikiwa kwake akirudi kalewa akalala kesho anaamka anasema hii company hapana aisee anakugeuzia kibao wewe kama mwanamke unatakiwa unihimize niachane na hii company unatakiwa hata tugombane. Huna mpango na mm ndo maana unaniacha acha tu. Hivi jaman mtu mzma unaweza gombana nae kisa company Au yeye anatakiwa achuje. Najua kwa mwanamke Ni rahis mwanaume kuweka limit kwa baadhi ya marafiki mwanaume Ni ngumu. Au mm ndo sijui kutunza mume.

Eti kwa miaka mitatu niliyokaaa nae natakuwa niwe nimejua kipato chake na siulizi. Ningekuwa Najua nafatilia kinatumikaje asingekuwa anakunywa Hivi. Jaman mm nafanya kazi na yeye anafanya kazi Hivi nilazma kuweka wazi haya mambo kabla hatujaoana wala kutambulishana nyumbani. Mm sijahoji coz pia staki anihoji kwa sasa labda badae tukiridhia kuoana.

Ninaona inafkia wakati haniamini kama Niko seriously na imepelekea tunapishana sana tunapojadili hizi tofauti zetu naishia kuonekana ninamakosa mwanamke Kuna mambo Ni wajibu wangu kuyafatilia.

Hebu nsaidieni labda sielewi Ni nn natakiwa nifanye kwa mtu nilienampango wa kuishi nae. Najihis ninamadhaifu sana. Nakosa hadi ujasiri

Sounds to me like you are a hopeless romantic!
 
Unajiskiaje unapokua na mtu anaekucha free iliyopitiliza eti?
Vale swts, binadamu tunatofautiana mnoo, mjue mtu wako then go with the flow. Kuna mtu ukimfuatilia hivyo, jiandae kwa kibuti, humpi space. Me naamini mtu kutokukufuatilia sana, Kuna matatu

1. Kaona umeshindikana, kukufuatilia wewe ni kutafuta presha tu, so kakuacha ufanye utakavyojisikia. Huonagi kuna baadhi ya men wanajisifia humu kuwa wake zao "hawajali, hawawafuatilii", na utawasikia kabisa "eeh huyo mke ndo ashakomaa kwa ndoa" teh. Kuna muda it's better u-save efforts zako kwa vitu vingine more useful, jaribu kumshauri mtu ambaye bado ana akili za kivulana arudi home mapema instead of saa 8 sijui, uone mziki wake. Sasa mtu anajua ana kampani mbaya ila wewe ndo u-deal nayo, unafanyaje kwa mfano? Sio yeye ndo a-take actions?

2. Unajitambua na anakuamini sana. If I trust a person aisee anaweza hisi simpendi labda. Mtu anajitambua, ana ratiba zake za kujitambua, na cha muhimu anatoa taarifa kwamba this time naingia hapa, natokea kule, naanzaje kumuuliza uliza maswali mob? Najua hana kibaya anachokifanya na hata kama anafanya, hajanioneshea, nampe space bana afanye vitu vyake ila tu taarifa iwepo.

3. Kuna watu sijui ndo niwaite "cold", anawezekana akawa anakujali mno ila ndo haoneshi hata iweje. Yupo tu kimya most of the time, unless umefanya balaa zito ndo utahojiwa. Sasa mtu wa hivi unaweza hisi hakupendi kabisa.

Vitu vingine kama unaona ni via muhimu mpenzi wako kujua, unaweza tu kumwambia wewe mwenyewe bila kusubiri akuulize. Mimi kama mimi kuulizia mshahara wa mtu ni wito mkubwa kwangu, labda ifike stage we wanna get married ndo itabidi nijue mapema ili nijue naingia vipi, ila yeye akiwiwa kuniambia it's ok. Afu issue ya simu kuna watu wanajijua roho zao ndogo, asije kufa kwa presha bure, so hagusi simu yako hata kama haina password. Mjue tu mtu wako alivyo na anataka nini, basi
 
That's a mama's boy, in every sense of the phrase. Blame his up-bringing. Some of us look for our mums' kinda affection from our ladies. So if anything, you should be grateful that he sees, or rather expects his mum's in you.

Adjust your game, or he'll adjust to the next one.
 
Back
Top Bottom