Nifanyeje Hataki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nifanyeje Hataki?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, May 6, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,276
  Likes Received: 3,192
  Trophy Points: 280
  Nifanyeje Hataki?


  SWALI


  Swali langu ni kwamba, je utafanyeje kama umeoana na mwanamke ambaye ni mzuri, mkweli, mpole, mwema lakini likija suala la kitandani ni usumbufu usioelezeka, ni boring to death!

  Nampenda sana mke wangu pia naamini na yeye ananipenda.

  Tangu kuoana kwetu tulipanga kuwa ndoa inayompa Mungu utukufu (obeying Christian values) hata katika suala la tendo la ndoa, ingawa ni mwenzangu hakuwa comfortable kulizungumzia.

  Sasa mke hapendi sex, hapendi kuongelea suala la sex (ukitaja tu neno sex anaanza kukunja sura kama ishara kwamba sipo tayari kuongelea hilo na tusipoongea hakuna linalofanyika au kurekebishwa).

  Baada ya kumfuatilia nikagundua kwamba Amekulia kidini sana.

  Naomba msaada nifanyeje?


  JIBU

  Kaka pole sana kwa shida iliyokukuta, hata hivyo Kumbuka hakuna jambo lisilo na mwisho.

  Inaonekana kwamba watu ambao hukulia kwenye imani za dini ambazo zinakuwa na msimamo mkali kuhusiana na masuala ya mahusiano (sexuality) huzaa wanandoa ambao linapokuja suala la sex kuna kuwa na matatizo makubwa.


  Zipo dini ambazo zinafundisha kwamba suala la sexuality lina uhusiano wa moja kwa moja na dhambi.

  Wanafundishwa kwamba dunia na vyote vijazavyo ni vitu vya muda tu na binadamu anatakiwa kushinda majaribu yote ya dunia hii ili kuurithi uzima wa milele ambao ndio matazamio ya nafsi zilizopo duniani.


  Na adhabu ya kushindwa kuyashinda majaribu ni kukosa uzima wa milele na moja ya majaribu makubwa ni suala la sex.

  Wanaamini sex katika ndoa ni kwa ajili ya kuijaza dunia tu (reproduction) na sex inapotumika kama kupeana raha (recreation, pleasure) kati ya mke na mume ni dhambi.

  Hivyo basi mwanamke anaruhusiwa kuwa mke na mama na si kujihusisha na sex kwa ajili ya kumridhisha mume au kupeana raha kati yake na mume wake.


  Anapokuwa mke na mama nyumbani anakuwa amechukua picha kamili ya mama mtakatifu (siyo Bikira Maria tafadhari msije mkanipiga mawe) na anapojihusisha na sex kwa ajili ya raha na kuridhishana na mumewe anakuwa amechukua picha (image) ya Malaya mtaani (prostitute).

  Hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba pamoja na hayo mapokeo na misimamo ya dini ambayo huwa kama malezi ya baadhi ya watu, haiwezi kuzuia hitaji la sex na zaidi hamu ya kuridhishwa kimapenzi katika ndoa.

  Kuhitaji sex ni kitu kimeumbwa ndani yetu (genes) na Mungu mwenyewe, raha ya kufanya mapenzi ndiyo huchochea watu kuzaana katika level ya kawaida.


  Mke wako inawezekana anajikuta kwenye wakati mgumu (guilt) pale unapomuhitaji kimwili, anapokubali kupeana raha ya mapenzi anajikuta inakuja picha ya kuonekana Malaya hasa kutokana na alivyolelewa (aliyokulia & fundishwa) na zaidi kufanya hivyo amefundishwa kwamba ni dhambi na anaweza kukosa ahadi ya milele ile ya kushinda majaribu hapa duniani hivyo hujiona afadhari awe mbali na wewe (kugoma sex zaidi ya suala la kuzaa watoto).


  Ombi lako rahisi la kuridhishwa kimwili ni kitu kingine kabisa kwake kwani kwa mtazamo wake kukubali kupeana raha ya mapenzi huweza kuathiri roho yake na namna anajiona.

  Anachohitaji mke wako ni uhuru au ruhusa ya yeye kuwa mtu wa kimapenzi (sexual) na kujifahamu kwamba kufurahia tendo la ndoa katika ndoa yake ni kitu kizuri na ni kiroho pia na zaidi si dhambi bali ni utakatifu pia kwani wewe na yeye ni mume na mke.


  Hata hivyo ni ngumu sana kwa wewe kumueleza kwamba yupo huru na ajisikie raha kuhusiana na suala la sex bali ni kumpata kiongozi wa dini yake ambaye anao ufahamu wa kutosha kuhusiana na suala la sexuality katika ndoa na kwamba huyo kiongozi wa dini yake anafahamu kwamba tendo la ndoa si kwa kuzaa tu bali faragha ya Adam na Hawa wa sasa na ni jambo zuri kwa wanandoa kufurahia mapenzi kwani wanandoa wanaporidhishana vizuri wanakuwa na furaha na kanisa huanzia nyumbani.

  Zaidi unaweza kuongea na wataalamu wa masuala ya mahusiano ya wanandoa (therapist & counsellors & wachungaji nk) ambao wanaweza kukusaidia wewe na mke wako na hata kulifahamu tatizo lake kwa undani zaidi na kuwasaidia.


  Naamini haya maelezo yameweza kuwa msaada!
   
 2. K

  Kagasheki Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wachangiaji wote hapo juu kuhusu suala la "Unyumba" kwenye Ndoa.Ni kweli kabisa kuwa ngono kwenye Ndoa ni kwa minajili ya kupata watoto lakini pia kutokana na maumbile ya binadamu na mihemko ndio sehemu pekee ambapo mmehalalishwa kuridhishana kimapenzi.Tatizo linakuja pale ambapo baadhi ya watu wanapochukulia tendo la "Unyumba" kuwa stahili yao ya msingi pindi wanapojisikia na kuleteleza wenzi wao kuwa wagumu kuridhia hilo.Hivyo kwa wanandoa ustahimilivu unahitajika sana maana usipokuwapo ndipo tunapoona mwendelezo wa "Nyumba Ndogo" na mengineyo mengi tunayoyashuhudia hivi sasa.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  akina dada wenzangu........................lazima tuwashinde hao nyumba ndogo kwenye suala la tendo la ndoa. (akitaka kwenda nje ende bila ya sababu ya msingi). nafikiri ni jukumu letu muhimu kama vile kumpa heshima mume na kufikiria feelings zake.
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,816
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  Umesema kweli Gaijin; ikiwa kutoka atoke kwa ulafi wake na si kwa kisingizio kuwa humpi!

  Mungu akubariki!
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  May 6, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,054
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  Mke ambaye hamtoshelezi mumewe kimapenzi anajisababishia matatizo kwani ndio mwanzo wa mume kutafuta nyumba ndogo itakayomridhisha kimapenzi. Kwa hiyo wanandoa na hasa akina mama wawe serious hasa linapokuja swala la sex.
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180

  na nyie kama hamtosheki muwe mnasema ..mkikaa kimya sie tutajuaje
  kama unataka dose kutwa mala tatu kama panadol sema
  kuna wengine 2 x 2
  wengine 1 x 1
  nitajuaje dose yako kama no communication in between ???
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  May 6, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,054
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  Ahahahaaaaah FL umenichekesha sana, kwa kweli watu wengi inapokuja suala la sex wanakuwa mabubu na hawawaelezi wenzi wao kuwa wametosheka au la, mwisho wanaamua kutafuta nyumba ndogo.
   
 8. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  aaah mkiongea mnafikia mahali ...
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,602
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  tukisema mnatuona walafi, then mnaanza kuhisi kama hyuyu jamaa anapenda hii kitu hivi, na appetite yake ni ya hali ya juu hivi, si atakuwa anamega nje kweli huyu.
  Siku ukiwa unamawazo kibao, deals hazijaenda sawa perfomance ikishuka kidogo, tena kwa week nzima ataanza kuwaza labda unamaliza mahali!
   
 10. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,816
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  FL1 wababa wanajitahidi sana ku-communicate na wakati mwingine hata wanaenda mbele zaidi kuyaweka mazingira lakini kama nyie wamama mnatuwekea hali ngumu na kutugeuzia migongo ilhali hata hamtuulizi kama tumelizika na huduma zenu ? matokeo yake...................
   
 11. k

  kamaningeweza New Member

  #11
  May 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ongea na shangazi yake au mwone paroko kama wewe ni mkristo..
   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nafkiri kuna mambo mawili ambayo hakika yanaweza kuya ya kweli kuhusu ndoa yako. la kwanza, uyo mdada atakuwa amevamiwa na pepo mahaba, maimuna etc.. watu kama hao, wakati mwingie jini huwa linabana uke, ukijaribu kupenetrate anaona kama unatia msumari, pepo linambadilisha halafu anakuwa hakupendi wewe kuwa naye, ila usiku anakutana nalo kwa kujua au kwa kutokujua, wengine wanajua kabisa na wanaishi nayo yanawafanya kila siku.

  pili, unaweza kuwa haujui kumfanya mwenzio, hivyo hajafurahi. ulimkuta bikira? kama ulimkuta bikira sawa, kama haukumkuta bikira hata kama alikuwa ameokoka, atakuwa alikuwa na lijamaa lililokuwa linamridhisha kwa level fulani, hivyo akija kwako anachukia tendo kwasababu anaona usumbufu tu. hivi kweli unamaana umeshawahi kulala naye, ukamridhisha hadi akatoa makelele asiyoyajua, na mambo mengi ya kuzirai kitandani brabrabraaaa, akafurahi uso wake, halafu bado tu anachukua tendo? hapana bwana, ukifanya vyema, atakuwa anakimbia mbio toka kazini jioni apike chakula haraka kabla haujafika, ili ukirudi tu mle chakula haraka, mwende kwenye uwanja mapema ili kesho muwahi kazini....atakuwa anatamani urudi home haraka ili aendelee kufurahia maisha...lakini kama yeye hafurahiii kwasababu ya udhaifu, basi siku ya kwanza atakuvumilia, ya pili atavumilia ikiendelea atakuchukia kabisa ataona hamna haja ya kulala na wewe....itaumbika tu akilini. sory to speak so open, lakini sisi sote tumeona wajameni.

  hivyo, nafikiri kuna mambo hayo mawili, hakika yake kama atakuwa ameingiliwa na pepo, mtapata shida, kwasababu huwa linabadilisha badala ya kukupenda, anakuchukia, usipookoka, linauaga mimba na hata watoto kwasababu jini hilo lina wivu sana.
   
 13. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,712
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Majibu yote ni ya hisia, maana jibu sahihi analo muhusika. Naongeza jibu lingine la hisia- huenda ameshapitia kwenye sex abuse na hilo linamletea shida kwenye fikra zake. Nadhani jibu zuri ni ushauri kuwa wamuone Mchungaji aliyewafungisha ndoa.
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,816
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  Kula tano! mwanangu mwenyewe!
   
Loading...