kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,247
- 16,169
Uko sahihi, mtafute ba ako ili usahihishe makosa yaliyopita yaliyotendwa na wazazi wako, ni vema ukaiandika upya historia na asili yako kwa manufaa ya vizazi vyako vijavyo. wewe unaweza kuignore lakini wajao huwezi kuwasemea. How to do this, kaa na mama yako kwa upole na unyenyekevu muongee juu ya swala la baba yako halisi, ukimuonyesha kuwa huna nia mbaya na swala hilo ila unataka kuiweka sawa historia yako na ya watoto wako hata wajukuu, kwani ni wewe mwenye uwezo wa kuirekebisha historia hiyo. Tumia watu wazima waliopo kama vile mama yako mkubwa, mjomba, babu, bibi zako ili wakuonyeshe njia. siku hizi vipo hata vipimo vya DNA kama baba yako atakataa wewe si mwanae. Mwambie baba yako kuwa huna nia ya kutaka mali zake ila unataka kuweka sawa historia yako.